Standing on the shoulders of the giants: Je, unawakumbuka ni watu gani wametufikisha hapa tulipo?

Pure_sapiens

JF-Expert Member
Dec 25, 2016
2,197
2,024
Habari zenu wana JF, natumaini Nyote ni wazima wa afya kwa wale wagonjwa tunazidi kuwaombea.

Standing on the shoulder of the giants ni ukweli usiopingika kuwa mafanikio yetu kwa asilimia kubwa yametokana na juhudi za wazazi, ndugu, marafiki, wapenzi, pengine hata watu baki. Kupitia kwenye mikono ya watu hawa Leo hii tunajivunia mafanikio mbalimbali na hatua tulizopiga katika maisha yetu,huku tukijipongeza kwa kushinda vita nyingi lakini tunawasahau watu waliotubeba kwenye mikono Yao na kuifanya safari yetu kuwa rahisi kwa namna moja au nyingine.

Basi uzi huu ni kuwakumbuka waliotubeba na kutupa matumaini katika changamoto mbalimbali. Mpe pongezi na shukrani Bila kusahau toas kama bado yu hai
 
Kitendo cha kibinadamu kinampasa kila mmoja,ukitendewa vema nawe tenda vema unakuwa umelipa. Utakumbuka wangapi?mbona ni wengi mno.Ulipokuwa mhitaji ulipewa msaada nawe msaidie mhitaji.
 
Back
Top Bottom