Stand mpya ya Nyamhongolo kuanza kutumika rasmi Augost 16

Sexer

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
8,215
7,906
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela Mhandisi. Modest Apolinary amewataka Wananchi na wote na wanaopata huduma za usafiri kwenda mikoani kwa kutumia stendi ya mabasi ya Buzuruga Manispaa ya Ilemela kujiandaa na mabadiliko ya kuanza kutumia stendi mpya ya Nyamhongolo kuanza August 16, 2022.

Modest amesema kwa Wananchi ambao hawatakuwa na tiketi watalipia 1,000 ikiwa na gharama za uendeshaji wa stendi mpya.

“Wananchi wote wanaopata huduma za usafiri kwenda mikoani August 16, tunaanza kutumia stendi yetu mpya ya Nyamhongolo, nikuchukue nafasi hii kumshukuru Rais Samia kwa kutufanikishia kukamilika, stendi hii imegharimu kiasi cha Bilioni 26. 6 hadi kukamilika kwake”.

Chanzo: Millard Ayo
 
I am proud to be involved kwenye hii project upande wa security,,, concern yangu ni moja hapo kwenye kiingilio cha elfu moja ni kikubwa sana kwa sisi wasukuma mbona Rockcity mall ambapo panavutia kuliko hapo tunaingia bure ? Wangeweka hata mia tatu maana hapa tutaishia nje tu ndani itakua ni kwa wasafiri na watalii.
 
Mwanza ni nzuri shida vitu vingi ni design za kisukuma
Shida ni wewe mwenyewe, kuhoji design nyingi za kichina nchini china, kuhoji design nyingi za kinigeria nchini Nigeria, kuhoji design nyingi za kimasai umasaini.
 
Hivi Buzuga palikuwepo na uasifi gani wa mikoani zaidi ya kwenda Mara tu? Kwahiyo hiyo stand mpya ni kwa ajili ya mabasi ya kwenda mkoa wa Mara tu?
 
Arusha nao wajengewe stand mpya ya mabasi ya mikoani.

Serikali iwe serious kuingilia kati kuhakikisha mabishano yaliyopo kila wakati yanamalizwa standi ianze kujengwa kwa manufaa ya watu wa Arusha Mjini.
 
Kuna Hostel pia na stand ya Malory makubwa ya mizigo, ni multipurpose ukijumlisha na viamba vya biashara.
 
Huna uzoefu, so swali lako lisingekuwa na generalization, lilitakiwa kubaki wazi.

Acheni ujuaji usio na tija, nenda pale upate routes zilizopo.
Hivi Buzuga palikuwepo na uasifi gani wa mikoani zaidi ya kwenda Mara tu? Kwahiyo hiyo stand mpya ni kwa ajili ya mabasi ya kwenda mkoa wa Mara tu?
 
Arusha nao wajengewe stand mpya ya mabasi ya mikoani.

Serikali iwe serious kuingilia kati kuhakikisha mabishano yaliyopo kila wakati yanamalizwa standi ianze kujengwa kwa manufaa ya watu wa Arusha Mjini.
waka paki Airport
 
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela Mhandisi. Modest Apolinary amewataka Wananchi na wote na wanaopata huduma za usafiri kwenda mikoani kwa kutumia stendi ya mabasi ya Buzuruga Manispaa ya Ilemela kujiandaa na mabadiliko ya kuanza kutumia stendi mpya ya Nyamhongolo kuanza August 16, 2022.

Modest amesema kwa Wananchi ambao hawatakuwa na tiketi watalipia 1,000 ikiwa na gharama za uendeshaji wa stendi mpya.

“Wananchi wote wanaopata huduma za usafiri kwenda mikoani August 16, tunaanza kutumia stendi yetu mpya ya Nyamhongolo, nikuchukue nafasi hii kumshukuru Rais Samia kwa kutufanikishia kukamilika, stendi hii imegharimu kiasi cha Bilioni 26. 6 hadi kukamilika kwake”.

Chanzo: Millard Ayo
Hebu weka picha tuone hiyo stand inayofanana na thamani ya mkataba wa Simba na m bet
 
Back
Top Bottom