Stanbic bank Tanzania: Wizi wenu umetuchosha!

Reginald L. Ishala

JF-Expert Member
Jun 18, 2011
3,811
6,780
Habari, Wanajamvi!

Kama nilivyosema hapo juu kuhusiana na Stanbic Bank TZ...

Watueleze wapi wanaipeleka pesa yetu inayosalia kama kilinda a/c baada ya kuhamisha,kutoa, ama kutuma pesa wakati wanakuwa wameshakata SH 3,000 kama makato yao ya mwezi?

Nachukia sana na wanakera sana kwa wizi huo, Naomba Wizara husika iwashughulikie.

Karibuni kwa nyongeza.
 
Kwani Jiwe anasemaje kuhusu hili?
Nchi hii ukiwa mlipa kodi mzuri unaweza kuwageuza wakaji(wateja) kadri upendavyo.
 
Makato yao ni elfu tatu kwa mwezi sawa, Sasa iweje tena akiba yangu ya kulinda account ikatwe wakati nimeshakatwa tozo hiyo?!
Kwani ukiamua kufunga account utakuwa na uwezo wa kuchukua pesa yako yote itakayokuwepo kwenye account yako muda huo?!! Jibu haiwezekani , huo ni utaratibu wa bank zote, kwani unaposikia bank charges huwa unafikiria ni nini?kama unaona wanakudhurumu kaweke nyumbani tu!!vitu vingine jamani!!kama unakwenda tu kuomba mkopo kwenye taasisi yoyote ile lakini humo humo ndani ya mkopo utakutana na gharama za kuushughurikia mkopo huo!!sembuse kukutunzia pesa!!
 
Huo ni wizi kwa maana inafanya kinyume na maelezo walotupatia wakati tunafungua a/c. "Inunue kweli wala usiiuze" 23:23 Mithali. Mizani ya hila na udanganyifu.
 
Ukipiga namba yao ya huduma kwa wateja ukawabana sana kwamba kulikuwa na kiasi fulani kwenye a/c yangu, Je, Kimeenda wapi mbona hakimwo?! Wanakukatia simu hupewi mrejesho sahihi jinsi kiasi hicho kilivyokatwa.
 
White Wizard ikikatwa pesa yako shilingi elfu 2 utasema bank charges sawa, Ukakatwa tena shilingi elfu 3 ndani ya mwezi huo huo mmoja. Je utakaa kimya usihoji? Bank charges gani hizo zinakatwa mara mbili ndani ya mwezi mmoja?!
Mwezi wa 3 tu nilikwanguliwa shilingi elfu 6. Kwa hiyo nikae kimya nisihoji eti bank charges?
 
Mwajiri wetu hutulipa mshahara kupitia Stanbic Bank TZ, Lakini pia wanakera sana mshahara ukishaingia ukataka kuutoa wanasema kuna tatizo la kiufundi kwa masaa 24.

Kwa nini tatizo la kiufundi liwepo tu kila tarehe ya mshahara na si nyingineyo?

Na kama kuna tatizo la kiufundi, Kwa nini hamkututaarifu mapema kwamba tarehe fulani kutakuwa na tatizo la kiufundi ili hali mawasiliano yetu mnayo?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom