Stan Katabalo: Tunauhitaji mzimu wako wa habari za Uchunguzi!

Nakumbuka wakati niko mdogo ingawa nilikuwa najua kusoma na kuandika wakati huo,kulikuwa na kashfa moja kubwa sana iliyoitingisha nchi,kashfa ya loliondo,kipindi hicho kuna mwandishi mmoja alikuwa anaitwa Stan Katabalo,nadhani alikuwa anaandikia gazeti la Mfanyakazi au.....kwa baadhi yenu huyu jamvini aidha mlikuwa wadogo sana au bado kuzaliwa lakini natumai wapo wengi waliokuwa wakubwa na walikuwa wanafuatilia kisa hiki kitakatifu,huyu jamaa mwandishi Stan Katabalo alikuwa anapambana na system na mbaya zaidi alikuwa peke yake katika kutetea masilahi ya nchi yetu,nakumbuka watu kama Ndolanga na wenzake.

Pamoja na Rais wa kipindi kile walikuwa wanahusika sana kwenye ile kashfa ya Loliondo,huyu jamaa mwandishi shujaa huyu alikuja kufa katika mazingira ya ajabu sana na mpaka leo sijasikia hata akienziwa,inauma sana...huyu jamaa alikuwa si tu shujaa bali alifungua njia kwenye tasnia nzima ya investigative journalism hapa nchini,hivi kwanini isianzishwe hata tuzo kwa jina lake?najua kuna watu na viongozi hatapenda kuusoma huu uzi kwa sababu kombe lilishafunikwa na mwanaharamu alishapita but huyu mtu anadeserve heshima ya pekee sana katika suala hili,kwa sababu hizi kashfa zote mnazoziona leo zikiwemo Richmond,IPTL,ESCROW

Sio kwamba zimeanza jana au juzi katika nchi hii,ni tangu kipindi hichoo cha Mwinyi sema tu watu hawakuwa makini kama ilivyo sasa na matokeo yake kwa wale waliokuwa conscious kama Stan Katabalo waliishia kupotezwa kusikojulikana,REST IN PEACE STAN KATABALO, HAKIKA WEWE ULIKUWA JABALI NA MZALENDO HALISI WA NCHI HII.
 
LOLIONDO GATE, kashfa kubwa iliyotikisa miaka ya mwanzo ya 90 na ndio chimbuko la mgogoro uliopo mpaka leo hii huyu bwana alikufa, na kwa alivyokuwa amejitolea kufatilia ili suala ni kweli anatakiwa kuenziwa, sijui waandishi wanalichukuiliaje suala hili.

Huyu bwana alichimbua kashfa hii kuanzia mwanzo wake mikataba yote iliyoingiwa na namna IKULU ilivyohusika katika kashfa iyo, wakubwa wakauchukua uhai wake, lakini hakufa mwenyewe kuna watu wengine pia walifuata nyuma yake kufuta ushahidi!
 
Huyu jamaa alikiuwa jembe kwerikweri, alikuwa akiliandikia gazeti la mfanyakazi na baadaye akanzisha la kwake motomoto.

Naweza kumfananisha na Kubenea ila huyu alikuwa akivuaka mipaka pia. Licha ya kashfa ya Loliondo, pia aliibua kashfa ya mchele mbovu wa mohamed interprises na hata ya mauaji ya Ouko waziri wa mambo ya nje wa Kenya kipindi cha Moi.

Lakini ndio hivyo kipindi hicho ukicheza na wenye madaraka na fedha maisha yako yanakuwa mafupi. Kaka umenikumbusha mbali sana!
 
Kashfa ya Loliondo.muhusika alokuwa waziri wa maliasiri na utalii sasa marehemu Abubakar Mgumia,Stan Katabaro alikuwa anaandika kupitia gazeti la mfanyakazi kila jumamosi jinsi mkataba huo wa magumashi ulivyoingiwa Kati ya serikali na waarabu ilikuwa kipindi cha mzee Mwinyi...Stan Katabaro alikufa na kuacha simanzi kubwa...
 
Huyu jamaa alikiuwa jembe kwerikweri, alikuwa akiliandikia gazeti la mfanyakazi na baadaye akanzisha la kwake motomoto. Naweza kumfananisha na Kubenea ila huyu alikuwa akivuaka mipaka pia. Licha ya kashfa ya Loliondo, pia aliibua kashfa ya mchele mbovu wa mohamed interprises na hata ya mauaji ya Ouko waziri wa mambo ya nje wa Kenya kipindi cha Moi. Lakini ndio hivyo kipindi hicho ukicheza na wenye madaraka na fedha maisha yako yanakuwa mafupi. Kaka umenikumbusha mbali sana!

Asante mkuu kwa kumuelewa huyu mpambanaji wa miaka hiyo,aliitetea Tanzania ila ndio hivyo tena wenye nchi yao hawakupendezwa na yale aliyokuwa akiyapigania,na pia sidhani kama jamii kipindi kile ilimuelewa?
 
Hii kiti nilisoma nikiwa mdg zamani stan katabalo...napenda mtu anayekumbuka vzr atuelezea vzr na kwa ufasaha...

Kuna ile pia kashfa ya kuuzwa kwa uwanja wa mnazi mmoja...ukazungushiwa mabati...kisha ikaamuliwe yatolewe wamachinga wakasafisha yote..hii nayo ya muda kdg
 
Loliondogate,kashfa kubwa kuwahi kutokea katika Taifa hili enzi za utawala wa Rais Mwinyi ilipelekea mwandishi mahiri wa habari Comrade Stan Katabalo apoteze uhai wake kwa jinsi alivyokuwa akiandika pasipo kumung'unya maneno kadhia hiyo.

Sasa tumebaki kuwa na waandishi wa habari vibaraka wa wanasiasa na wanaolamba viatu vy wanasiasa.

Kifo cha Stan hakijawahi kuchunguzwa na taarifa yake kuwekwa hadharani maana hakikuwa cha kawaida.

Natoa wito kwa UKAWA kuchunguza upya kifo cha Stan na kukomesha uporaji wa raslimali za taifa unaoendelea Loliondo - Mungu akiwajaalia wakashinda uchaguzi.
 
umeongea ukweli mkuu,Stan Katabalo ni aina ya pekee katika uandishi wa habari,alipigina ile vita peke yake na hatimaye akapotezwa na walafi wa nchi hii,ikiwezekana afukuliwe upya apimwe na kijulikane kilichomuua.......inaumiza sana kumpoteza kirahisi yule mpambanaji!
 
Back
Top Bottom