STAMICO tumieni fursa hii kujenga kinu cha kuchakata huu mchanga

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
15,983
11,399
Kama tuna mtambo mpya wa umeme wa Kinyerezi tuna bomba jipya la gesi, tuna makontena ya kutosha ya mchanga. Kwanini stamico kupitia stamigold msijenge kinu cha kuchakata huu mchanga?

Miaka ya themanini tuliambiwa hatuwezi kuwa na kituo cha television kwani ni ghali na viko viwili tu BBC na CNN, Mengi akajenga na sasa viko kila kona nchini.

Tujenge kinu chetu hayo tutayachaka na wachimbaji wadogowadogo watayapeleka pale badala ya kuyamwaga kwenye mito na kuharibu mazingira.
 
Tunaweza kuzalisha tani 150,000 za mchanga kwa mwaka kulisha mtambo??

Buzwagi na Barrick kwa ubabe wao wote wanazalisha tani elfu 40 tu kwa mwaka.
 
Asigwa, mtu mmoja ana tani elfu 40, nenda GGM ndio balaa yako kama mlima kitonga, bado wachimbaji wadogo wadogo, utashangaa hata huo mmoja hautoshi.

Bhakresa ana kinu cha kusaga ngano kikubwa africa mashariki lakini kuna mashine ndogo za kukoboa na kusaga sembe.

Kuna vituo vikubwa kama cnn bbc na aljazeera lakini vipo vidogo kama clouds sibuka na radio maria, tukisema kituo cha tv lazima kiwe kama cnn wakati vipo vingine vidogo kama millard ayo tv tutaonekana majuha.
 
Back
Top Bottom