staili hii ya ndoa inavyonichosha!!

kwa kweli kama walivyosema wengine yataka moyo wa chuma. nishaona watu wameoana style yako. baada ya honeymoon ambayo ilifanyika mkoa tofauti na wote wawili wanapoishi, bwana harusi alirudi na kukita kwenye nyumba ndogo yake, akamaliza mwezi ndio akarudi kwenye kibanda chake. mke yuko Lindi anajua hubby anakaa kwake, kumbe yuko kwa nyumba ndogo anapikiwa na kupakuliwa. sitaeleza mengi hapa ila be careful kijana. mmoja ni bora asamehe kazi amfuate mwenzie. Kazi atapata tu. kila la kheri...
 
Hiyo aina ya ndoa haijakaa vizuri, haikuwa na haja ya kuoana ili mkae mbali, maisha yenyewe ndo haya kwanza mafupi! Msimpe shetani nafasi ya kuwapepeta msijejuta mambo yatakapokuwa tofauti.
 
Jamani kuna kitu kiitwacho sacrifice na compromising! Kama hamuwezi kusacrifice basi mjitahidi kuweka utaratibu wa kuonana mara kwa mara.
 
riziki popote mkuu,na maisha ndiyo haya sasa kuishi na distance mariage haina maana hata kidogo mwisho wake sio mzuri
 
Maisha hayo ni ya kawaida tu hasa uliza experience ya Watoto wa Mangi ambao huacha wake zao na kufuata biashara popote hapa nchini na hata nchi za nje. Wakati wa Krismasi hukutana pamoja huko milimani na kupeana mimba kisha hu-sepa na wakirejea hukuta watoto tu.

Kwa upande mwingine kama mwenzio haoni shida inawezekana ana 'dummy lover' ambao hupoza ashiki zake hivyo haoni haja ya kukufuata. Kama wewe ndilo hitaji lako, fanya utaratibu umfuate mkeo. Chagua ndoa au kazi.
 
ndugu yangu,mtatafuta maisha wote wawili sawa ila upande wa pili wa uhusiano wenu kwa vyovyote utaathirika sana na matokeo hayo maendeleo yenu kiuchumi yatakuwa hayana maana.cha msingi mmoja wenu aamue kacha kaz na amfute mwenzie na kama ni kazi atafutie ulipo/alipo.vinginevyo kwa hali ya sasa na kwa record zilizopo,mtakuja laumiana bure kama sio kuumizana tu! stuka!
 
Back
Top Bottom