Stahili za wabunge utata | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Stahili za wabunge utata

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Apr 2, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 421,163
  Trophy Points: 280
  Stahili za wabunge utata

  Imeandikwa na Gloria Tesha; Tarehe: 1st April 2011 @ 23:58 Imesomwa na watu: 108; Jumla ya maoni: 0
  WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, amezindua Tume ya Utumishi wa Bunge na kuitaka pamoja na majukumu mengine, itafutie ufumbuzi suala la malipo ya mishahara, posho na stahili nyingine za wabunge baada ya Bunge kuvunjwa.

  Agizo hilo alilolitoa jana linatokana na alichoeleza kuwa ni utata uliopo kisheria kuhusu ukomo wa malipo hayo kwa wabunge ambao Katiba inaeleza, kuwa ukomo wao ni pale Bunge linapovunjwa na Rais Agosti ya kila baada ya miaka mitano (miezi 58) wakati sheria nyingine zinaeleza ni miezi 60.

  Akizungumza Dar es Salaam kabla ya kuzindua Tume hiyo mpya iliyokabidhiwa mikoba kutoka kwa iliyokuwa ikiongozwa na Samuel Sitta (Spika wa Bunge la Tisa), Pinda alisema, “tumefanya uchunguzi na kupata barua kutoka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) tulipowauliza kuhusu suala hili.

  “Ni kwamba Ibara ya 65 (1) ya Katiba, inasema maisha ya kila Bunge ni miaka mitano, vile vile Ibara ya 65 (2) inafafanua kuwa maisha ya Bunge ni muda wote kuanzia tarehe ambapo Bunge jipya limeitishwa kwa mara ya kwanza baada ya Uchaguzi Mkuu na kwisha tarehe ya kuvunjwa kwa Bunge ili kupisha Uchaguzi Mkuu kufanyika.”

  Pinda alisema imefahamika kuwa baada ya Rais kuvunja Bunge na kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali, ndipo ukomo wa muda wa mbunge unakwisha, suala linalodhihirisha kuwa ukomo pia wa malipo ya mishahara na posho zote zinazolipwa kwa wabunge.

  Mwaka jana, baada ya Rais kuvunja Bunge, wabunge hawakulipwa mishahara ya Septemba na Oktoba kama ilivyokuwa kwa mabunge yaliyopita na kusababisha baadhi ya wabunge kuendelea kudai mishahara na posho zao hadi sasa, kwa kuwa utumishi wao ni wa miezi 60 ikijumlisha Septemba na Oktoba.

  Waziri Mkuu aliitaka Tume hiyo kumshauri Rais kuhusu suala hilo, ili kuona kama kweli upo uhalali wa kuendelea kulipwa wabunge malipo hayo, wakati uwakilishi wao kwa wananchi katika majimbo haupo baada ya Bunge kuvunjwa.

  Aidha, alisema yapo maeneo yenye mgongano wa kisheria wa Katiba na Sheria ya Utumishi wa Bunge ya mwaka 2008 ambapo kifungu cha 7(3) kinaainisha kuwa Tume itapendekeza majina matatu ya watu ambao wanafaa kuteuliwa kuwa Katibu wa Bunge kinyume na Ibara ya 87 ya Katiba inayompa mamlaka Rais kuteua Katibu wa Bunge miongoni mwa watumishi waandamizi.

  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Tume hiyo ambaye pia ni Spika wa Bunge, Anne Makinda, kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu, alisema Tume iliyopita ambayo yeye alikuwa Makamu Mwenyekiti wake, ilifanya kazi kubwa ikiwa ni pamoja na kuwezesha kukubaliwa mpango wa ujenzi na usimamizi wa ofisi za wabunge majimboni na Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo.

  “Hata hivyo changamoto zipo licha ya bajeti ndogo ya uendeshaji wa shughuli za Bunge, kutokamilika kwa mchakato wa kuanzisha Mfuko wa Bunge na Ikama ya Watumishi wa Bunge kutoendana na ongezeko la idadi ya wabunge,” alisema Makinda.

  Takwimu zinaonesha kuwa Bunge lina watumishi 251 wanaohudumia wabunge 357. Hafla hiyo pia ilihusisha ugawaji wa vyeti vya kuthamini mchango wao kwa wajumbe wa Tume iliyomaliza muda wake.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Apr 2, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 421,163
  Trophy Points: 280
  PHP:
  Takwimu zinaonesha kuwa Bunge lina watumishi 251 wanaohudumia  wabunge  357. Hafla hiyo pia ilihusisha ugawaji wa vyeti vya kuthamini  mchango  wao kwa wajumbe wa Tume iliyomaliza muda wake.
  Hii inanikumbusha ATC............................enzi zake.......................kila ndege na bawa lake.................................uwiano wa wabunge na watumishi ni karibu moja kwa moja.............................nionavyo Bungeni there is overemployment............................
   
 3. N

  NIMIMI Senior Member

  #3
  Apr 2, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 170
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hilo liko wazi; ukiwasikia wanavyokomalia posho, fedha za kujikimu na staili zao zote MINAJILI ya watoto wa chekechea wakigombea UJI. hii kweli inatisha cfahamu 2nakwenda wapi na 2tafika vp?
   
Loading...