Stade des Martyrs, Congo: AS Vita Club 5 - 0 Simba SC

Attachments

  • Screenshot_2019-01-20-18-47-42.png
    Screenshot_2019-01-20-18-47-42.png
    68.5 KB · Views: 28
“Simba ni timu nzuri lakini wanacheza mpira
ambao sio wa kasi, wanapiga pasi ambazo
kwenye mashindano hazina faida, wanapoteza
muda mwingi kupiga pasi za hapa na pale
badala ya kwenda mbele kutafuta nafasi. Sisi
tunarudi nyuma tukipata mpira tunacheza kwa
speed.”

Ina maana mcheza mieleka haya mapungufu hayaoni?!
 
Leo tunashuka dimbani kucheza mchezo wa pili wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita Club.

View attachment 999209
Kikosi cha akiba cha Simba
1. Deogratius Munish
2.Paul Bukaba
3.Moahamed Ibrahim
4.Haruna Niyonzima
5. Hassan Dilunga
6. Rashid Juma
7. Shiza Kichuya

Hiki ndio kikosi cha mauaji kitakachoshuka dimbani leo kufanya mauaji

========


Timu ya Simba imepoteza mchezo wake wa pili hatua ya makundi baada ya kukubali kipigo cha mabao 5-0 dhidi ya AS Vita.

Mabao ya mapema ya AS Vita yaliwekwa dakika ya Makusi 14' Bpunga 18 na Fabrice Ngoma 45 kipindi cha kwanza.

Mabao mawili ya AS Vita yaliwekwa wavuni kipindi cha pili huku wakionekana kulifikia lango la Simba mara kwa mara.

Mchezo huo ulionekana mkali huku Paschal Wawa na Jonas Mkude wakipewa kadi za njano.

Kocha wa Simba Patrick Aussems alimtoa Cleoutus Chama na nafasi yake kuchukuliwa na Dilunga dakika ya 61.

Katika Kundi D, AS Vita ipo nafasi ya pili ikiwa na alama 3 huku ikifuatiwa na Simba yenye alama 3 ikizidiwa mabao ya kufunga na kufungwa.

Baada ya mechi ya AS Vita vs Simba kumalizika, nilikutana na kocha msaidizi wa Vita Raoul Shungu ambaye si mgeni kwa watanzania kwa sababu aliwahi kufundisha Yanga.

Shungu amezungumzia mambo mengi kuhusu mchezo wao dhidi ya Simba, amesema kuwa waliangalia mechi kadhaa za Simba na kubaini mapungufu ambayo wameyatumia na kupata ushindi.

“Simba ni timu nzuri lakini wanacheza mpira ambao sio wa kasi, wanapiga pasi ambazo kwenye mashindano hazina faida, wanapoteza muda mwingi kupiga pasi za hapa na pale badala ya kwenda mbele kutafuta nafasi. Sisi tunarudi nyuma tukipata mpira tunacheza kwa speed.”

Shungu amesema katika kipindi chote alichofundiaha Yanga, alishinda mechi zote alizokutana na Simba.
Mechi ijayo acheze Munishi Itapendeza pale golini
 
Nyie kwani mmeshaupata huo ubingwaaa??😂😂😂.....na wewe Malindi unawakumbuka????

Tungemfunga malindi tungeenda kucheza mechi gani ya kimataifa? Ubingwa wa FA na ubingwa wa ligi kuu ndio unaoipeleka timu anga za kimataifa
 
Tungemfunga malindi tungeenda kucheza mechi gani ya kimataifa? Ubingwa wa FA na ubingwa wa ligi kuu ndio unaoipeleka timu anga za kimataifa
Sasa na sisi kwani tungechukua FA tungeenda kucheza mechi gani za kimataifa zaidi ya tunazozicheza leo....kumbe issue ni kucheza mechi za kimataifa...mbona ndo wenzenu tunazicheza sahv...izo anga za kimataifa mnazotafuta kwenda ndo wenzenu tupo sahv
 
Unazeeka sasa na unaanza kupungukiwa akili, simba sc inawakilisha Taifa acha umaandazi!
kwa style hii acha tu nizeeke na hayo maandazi niyanywee chai tu....

sio kwa udhalilishaji ule aisee, mnawakilisha taifa mnarudi na kapu la magoli?
 
Back
Top Bottom