"Stability" ya nchi kisiasa inaliweka Taifa kuwa imara kijamii, kiuchumi na kiteknolojia

winnerian

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
334
530
TATIZO: "Unstable Political Grounds of the Nation"

TATIZO ZAIDI:
"Poverty Among Politicians is the Root Cause of Unstable Political Ground of the Nation"

ZAIDI YA TATIZO: "POVERTY IS A RESULTS OF LOCKED MIND OF GREAT THINKERS IN THE SOCIETY BY THE POOR POLITICIANS FOR THEIR OWN GREED TO STAY IN POWER AND EXPLOIT THE POOR"


Kwanini "unstable Political Grounds of the Nation" ni TATIZO katika nchi kwa maendeleo ya nchi husika (TANZANIA)?
Kwa mfano Chama ni kile kile cha "CCM" lakini kina siasa nyingi na zisizo na faida kwa taifa, yaani kwa urahisi unaweza kusema "CCM" ni mti wenye matawi ambayo yanazaa matunda tofauti tofauti katika kila tawi lake na hayo matunda hayaliki (matunda pori). Fikiria hivi, toka tumepata uhuru tumekuwa na chama kimoja tu kinachoongoza nchi yetu ya Tanzania lakini kila raisi tunaempata anakuwa na maono yake binafsi na kwa namna anavyotaka iwe (sio vile wengi wanavyotaka iwe, la hasha). Kwahivyo kila awamu inavuruga awamu iliyokuwa madarakani na kuhakikisha inauwa kabisa "legacy" ya mtangulizi wake. Angalia mfano hapa chini

Mwalimu Nyerere aliweza kuwa na fikira pamoja na mawazo chanya kwa taifa letu lakini pia alishindwa namna ya kutekeleza fikra zake kwasababu aliamini zaidi katika uwezo wake peke yake na hakupenda mwingine aonekane anaweza zaidi yake hivyo akatengeneza taifa linalotegemea mawazo ya mtu mmoja katika kuliongoza na kulitawala. Mambo mengi alifanikiwa lakini kubwa alilofeli ni kuitoa Tanzania katika ufukara wa fikira, uchumi, kijamii na kiteknolojia, hapa mwalimu aligonga mwamba kwasababu hakutaka kuwapa watu nafasi ya kutenda kwa uhuru na usawa. Mwishoni akatambua kwamba ameongoza nchi kwa miaka 24 bila mafanikio akang'atuka.

Baada ya mwalimu kung'atuka akamwachia Mzee wetu Ali Hassan Mwinyi. Huyu nae akaja na sera zake tofauti kabisa na sera za mtangulizi wake, aliacha watu wafanye wanavyoona ni sahihi bila kuwabughudhi na akajipatia jina maarufu lilodumu mpaka leo, "Mzee wa ruksa" Matokeo yake nchi ilikosa mapato na ikaingia katika umaskini mkubwa huku wachache wakitumia fursa ya "Mzee wa Ruksa” kujinufaisha na kujipatia ukwasi mkubwa. Ni mengi ambayo yalienda mramba kwasababu ya utawala wa kutojali misingi ya sharia na kanuni zilizowekwa kuiongoza nchi. Baada ya “Mzee wa Ruksa” alingia Hayati Benjamin W. Mkapa na sera zake za ubinafsishaji wa taasisi za uma, kwa utashi wake na mawazo yake mwenyewe aliona hili linaweza kuisaidia nchi na kwasababu alisharithi nyendo na hatua za watangulizi wake kwa maana ya kuamua na kufanya mambo kama avyotaka yeye bila kushirikisha wataalumu wa kweli sera zake zote ziligonga mwamba na kuwa sera potofu na zisizolisaidia taifa letu kusonga mbele na watu wake wakapata maendeleo ya kweli.

Nchi ilipitia kwenye maumivu makubwa yasiyoelezeka raisi Mrisho Jakaya Kikwete alipoingia madarakani, kutokana na udhaifu wake wa kusimamia wale wote waliopewa dhamana ya kuliongoza taifa pamoja naye; aliacha kila mmoja aliyepata nafasi kufanya mambo yake bila kumbughudhi wala kukataka kujua kinachoendelea, hapa ndipo tulipopata mafisadi wengi wakubwa na wenye kuiba mali za uma waziwazi bila uoga, shangwe na nderemo kwa wachache zilitawala mtaani maana hakuna uongozi Madhubuti nchini, nyani wanakula mahindi na kuishi humo humo kwenye shamba maana mwenye shamba ameruhusu na yeye mwenye yumo akishirikiana na nyani wenyewe.

Kikwete ndio raisi aliweza kuanzisha sera nyingi na zote hazikufanikiwa chache na maarufu zikiwa ni “Kasi Mpya, Nguvu Mpya na Ari Mpya.” “Ari Zaidi, Nguvu Zaidi na Kasi Zaidi”, “Kilimo kwanza” pamoja na “Big results now” zote hizi ni usanii wa kuwalaghai wananchi kuamini kwamba wanapelekwa kwenye maendeleo ya kweli. Baada ya raisi Kikwete tukampata hayati John Joseph Magufuli. Huyu alikuja na kuanza kuangamiza mara moja madudu yote aliyoyafanya mtanguliza wake Mh. Jaka Mrisho Kikwete kwa namna ambayo alipitiliza na kuanza kuliangamiza taifa kwa ujumla.

Alianza vizuri kwa kujinadi Tanzania imechelewa sana kupata maendeleo na kutangaza umoja na mshikamano wa kinafiki na uzandiki huku akiwanyamazisha wapinzania wake wote kwa kuwapiga waziwazi akiamini yeye tu ndio mwenye uchungu wa kweli na taifa letu hakuna mwingine. Alienda mbali na kuwaita wenye nchi yao kwamba ni wanyonge hivyo anawapigania wapate haki kumbe nay eye ni kauli ya unafiki na uongo yenye kumpatia maslai yake binafsi ya kisiasa, amefariki na kuicha nchi katika magawanyika wa ajabu ajabu, amefanikiwa kuanzisha kundi lenye nia mbaya na taifa kwakua aliwatenga na kwaona ni wabaya na wasio na nia njema na taifa hili hali yeye pekee ndio mwenye nia njema.

Sasa tuane Mama, Samia Suluhu Hassan. Huyu naye kaanza kwa gia zile zile za toka mwaka 1985 alipoichukua nchi mikononi mwa Mwalimu Nyerere. Hajataka kuwa mstahimilivu na kuona umuhimu wa kuipa Tanzania dose inayoweza kutibu maradhi yake bali ameenza kwa kuipa dose isiyoeleweka na maradhi yalimo mwilini mwa Tanzania. Nisingeweza kumuongolea sana Mama maana bado hajapata muda wa kutosha kukaa madarakani lakini hata yeye ninaimani ni kati ya matawi yale yale ya mti wa “CCM” yanayozaa matunda yasiyolika.

Kwa mfano huo hapo juu unaona ni kwanamna gani nchi yetu Tanzania, toka ipate uhuru haijawa na siasa iliyokomaa na isiyoyumbayumba kwasababu kila raisi ajaye anakuja na mawazo yake ya mgando na yasiyokuwa na tija kwa taifa. Na hii ni kwasababu kila raisi ajaye anakuja na fikira za kulinda maslahi yake mwenyewe na maslahi ya chama “CCM” na kupoteza mwelekeo wan nchi na mwisho anaondoka madarakani akiwa amefeli kutatua tatizo kuu la Taifa la Tanzania ambalo ni maendeleo ya kifikira, kijamii, kiuchumi na kiteknolojia.

Nakazia sana kifikira maana katika taifa lolote ambalo fikira za watu wake zimefungiwa na kuruhusu fikira za mtu au watu wachache ndizo zitawale nyingine basi hilo taifa halitaweza kusonga mbele daima maaan maono ya mtu mmoja yanaelekea gazani siku zote bali maono ya wengi yaishia penye mwanga na nuru ya kweli.

Tunashindwa kuwa na matajiri maana wote tumepumbazwa na kulishwa sumu ya umaskini chini ya kivuli cha “Tanzania ya Wanyonge”. Wawekezaji watakuja leo lakini kesho atakuja raisi ambaye anawachukia matajiri na kisha watakimbia wote. Yote ni kutokuwa na mfumo imara wa utawala bora na uongo imara wa katiba na sheria.

SULUHISHO KUU LA MATATIZO YA TANZANIA: KATI YA RAISI ALIYEPO MADARANI AU AJAYE KWA CHAMA CHOCHOTE, MMOJA WAPO AJITOE MUHANGA NA KUIPATIA TANZANIA UHURU WA KWELI. UHURU NDIO SOLUHISHO LA KWELI NA DAWA YA KWELI YENYE KUWEZA KUITIBU MARADHI YAKE YOTE KUBWA LIKIWA NI UNAFIKI NA UONGO UNADIDIMIZA NCHI KWENYE UMASKINI USIOISHA.

UHURUA WA KWELI NI HUU HAPA

KATIBA YENYE KUWAPA HAKI SAWA WANANCHI WOTE
. “All Citizens of Tanzania are Equal Before the Law”. Wananchi wote wakiwa na haki sawa mbele ya sharia hata msafara wa raisi hautaweza kusimimasha magari ya abiria pamoja na binafsi kwa masaa sita yakiwa yanasubiri kiongozi mkubwa serikalini kumaliza mkutano wake apite kisha ndio yaruhusiwe kuendelea na safari.

MIHIMILI YA NCHI ITENGWE NA KUWA “INDEPENDENT” yaani huru na wanaoisimamia wapatikane kwa haki na sifa ziwe za hali ya juu sana kuwezesha kuongoza mihimili hii kwa haki, usawa na bila upendeleo. Ikiwa tutapata mihilimi ya nchi iliyo imara ni wazi kwamba wale wadhaifu wote watakaoshindwa kutopeleka tunapostahili watajihudhulu wenyewe bila kushurutishwa maana watakuwa wanakali kiti cha moto kila siku tofauti na sasa wanakalia kitu cha sofa kisichokuwa na moto wowote. Mihimili ya Taifa la Tanzania ni mitatu tu nayo 1. SERIKALI KUU, CHINI YA RAIS
2. MAHAKAMA CHINI YA JAJI MKUU
3. BUNGE CHINI YA SPIKA,
lakini ni wazi raisi amewashikilia hawa wengine wote na kuwadhohofisha sana wasiweze kutenda kwa uhuru na usawa katika nafasi zao.

TUME HURU YA UCHAGUZI NA UTARATIBU WA WAZI KATIKA CHAGUZI ZOTE ZA NCHI italeta tunda la haki katika taifa let na wale wote wanachaguliwa kwa nguvu ya uma watakuwa na uwezo wa kutenda na kusimamia maslahi ya wananchi waliowachagua tofauti na sasa wengi karibia wote wamepata nafasi za uwakilishi kwa kukingiwa kifua na nguvu ya dola kwa shikinikoz la raisi aliyekuwepo madarakani kipindi cha uchaguzi. Wananchi wakipewa uhuru wa kuchagua hawatafanya makosa hata kidogo lakini wakichaguliwa watachaguliwa mtu ambaye sio pendekezo lao na yule aliyechaguliwa atafanya kwa mapenzi ya yule aliemsaidia kupata nafasi ile, hatakuwa na uwezo wa kuhoji pale mapungufu yanapojitokeza

SIFA ZA WAGOMBEA WA NAFASI ZA KISIASA ZIUNDWE UPYA ili tupate viongozi ambao wana utashi na uchu wa kuyaweka maslahi ya taifa mbele kuliko matumbo yao, kuliko mawazo yao mgando, kuliko vyama vyao vya siasa na zaidi kuliko umaskini wao. Tofauti na sasa ambapo sifa ni mbili tu ajue kusoma na kuandika, sifa hizi ziongezwe hata zifikie sifa hamsini ili kutoa mwanya kwa wasomi, wazalendo, na wenye haki kuliongoza taifa bila uchu wa madaraka wala ubaguzi wakishikisha wananchi wake na kutoa fursa mbalimbali za watu wote kuwa na uhuru katika kulijenga taifa lao.

NA MWISHO KABISA SHERIA ZOTE KANDAMIZI ZIDI WATANZANIA ZIFUTWE na kuwaacha watanzania huru katika kuishi, kujenga na kumiliki taifa lao. Zipo sharia ambazo zimetungwa kwa maslahi ya wachache na zinakandamiza walio wengi, na kwa hakika sharia hizi ni nyingi na zimetufunga funga kama vile kuku aliefungwa fungwa miguu na mabawa asiweze kwenda popote wala kuruka popote. Tumekuwa kama watumwa katika taifa la ugenini ili hali sisi watu wenye uhuru kutoka kwa mkoloni toka mwaka 1961 taree 9 mwezi wa kumi na mbili saa sita kamili usiku benderea ikapandishwa.

MAMA SAMIA SULUHU HASSAN JITOE MUHANGA UTUPE TANZANIA UHURU NA MAENDELEO YATAKUJA YENYEWE BILA KULAZIMISHWA.
 
Nimesema mahali pengine kuwa 17th March iwe siku ya uhuru kutoka kwa mweusi mwenzetu. Tuliteseka saaaana!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom