St.marry's international school umakini umeondoka-ona hatari hii!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

St.marry's international school umakini umeondoka-ona hatari hii!!!

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Anold, Jul 5, 2012.

 1. A

  Anold JF-Expert Member

  #1
  Jul 5, 2012
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Ni ukweli usiopingika kuwa Miaka kadhaa iliyopita Shule za St. marry's zilijijengea sifa hapa nchini hata nje ya nchi. Kinachoendelea sasa hivi hata sikielewi kwani pamoja na usimamizi hafifu kwa wanafunzi lakini kuna hatari hii ambayo kwa wazazi walio na watoto wanaosoma st. marry Tabata lazima waone hatari hii ambayo kama hatua kali za kisheria hazitachukuliwa basi kilio kinaweza kutokea.

  Baadhi ya magari yanayotumika kubeba wanafunzi wanaoishi maeneo ya segerea/ Kinyerezi ni mabovu na hatari ambayo siamini kama shule yenye hadhi ya kimataifa inaweza kuruhuru hatari hii, ni bahati mbaya tu kuwa namba za magari hayo sijafanikiwa kuzishika(nitarudi tena kuziweka jamvini) ila ni aina ya DCM.

  Wakati wa mvua magari hayo huvuja na hata wiper hazipo hivyo humlazimu dereva kuegesha pembeni ili mvua itulie, si hivyo tu hata tanki za mafuta hazitumiki hivyo kulazimika kutumika vidumu ambavyo hii haikubaliki.

  Hivyo wazazi wa shule hizi wafuatilie jambo hili kama kabla balaa halijatokea
   
 2. M

  Mukalunyoisa Senior Member

  #2
  Jul 5, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 139
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Haya kwa wazai wenye watoto wanasoma st mary thadhari hiyo mmepewa, tafadhali zingatieni sana uhai wa watoto wetu
   
 3. M

  Makupa JF-Expert Member

  #3
  Jul 5, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  mmiliki ni mwanasiasa, mchungaji na ni mjasariliamali , ukijumlisha na kutoa hapo utapata jibu
   
 4. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #4
  Jul 5, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  mi nilidhani unawatahadharisha na jeshi la polisi-usalama barabarani maana wao ndo hujua zaidi, kwani baadhi ya wazazi unaowatahadharisha wao pia magari yao yako hivyohivyo
   
 5. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #5
  Jul 5, 2012
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Vp academic performance? nayo inashuka au inazidi kupaa??
   
 6. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #6
  Jul 5, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  name and shame him/her?? hawa viongozi wetu usipowataja hawatabadilika
   
 7. moniccca

  moniccca JF-Expert Member

  #7
  Feb 13, 2017
  Joined: Nov 15, 2015
  Messages: 2,189
  Likes Received: 3,004
  Trophy Points: 280
  Ajafanya
  Shure
  Hajafanya
  Shule
   
 8. nsanzu

  nsanzu JF-Expert Member

  #8
  Feb 13, 2017
  Joined: Jul 29, 2015
  Messages: 1,975
  Likes Received: 1,192
  Trophy Points: 280
  Nadhan afadhali za St Mary's, kuna za Green Acres ndugu dooooh! Yaan ada na huduma viko kinyume
   
 9. Z

  Zanzibar-ASP JF-Expert Member

  #9
  Feb 13, 2017
  Joined: Nov 28, 2013
  Messages: 4,222
  Likes Received: 5,947
  Trophy Points: 280
  St Mary's ilikuwa enzi zilee, wakati ule English medium schools zilikuwa chache hapa Tanzania, ila kwa sasa St. Mary's imeshoka balaa, wanaunga unga mambo sana. Kielimu iko ovyo sana, Kiimadili ndio inatia kinyaa. Kwa sasa wako kibiashara tu.

  Wakati shule zingine kama Feza, Tusiime nk zinazidi kupaa kielimu, St.Mary wanazidi kufa kabisa kielimu.
   
 10. A

  Anold JF-Expert Member

  #10
  Feb 14, 2017
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Jamani hii post mbona ilikuwa ya miaka 4 iliyopita? kuweni makini kidogo, aidha nilichokiandika kilikuwa sahihi maana baada ya kuona wakati huo iposhida ya ubovu wa gari nilimhamisha mwanangu na kumpeleka TUSIIME. Kwa sasa sielewi chochote kuhusu hiyo shule maana ni miaka mingi wewe ni mgeni sana humu usifukue makaburi ya zamani.
   
Loading...