St.Kayumba wote tukutane hapa Wazee wa kidumu na Maji

Zero IQ

JF-Expert Member
Dec 21, 2016
13,941
24,816
Wale wenzangu tuliosoma st.Kayumba wazee wa kidumu na Maji mje tukutane hapa. Usisahau kueleza kile ambacho kila ukikumbuka unajifunia kusoma hizo shule iwe kizuri au kibaya ilimladi tu ukikumbuka kinakufanya uwe proud kusoma hizo shule
Vituko,matokeo michezo yote tuweke hapa tuwatamanishe wale wanaojifanya wa ki international school kumbe walikosa mengi.
b986ef08be2196930385a5a531618eb4.jpg
 
Tulikua tunaagizwa kuleta kuni moja moja hasa wakat wa sherehe za shule, kuwahi namba pia ukipiga kelele unapelekwa mbele kupiga magoti na kunyoosha mikono juu kama unaita mtu.
Ila st kayumba zimetusaidia kutukomaza tunaishi maisha yoyote maana mvua ilikua yetu jua letu hahahaaaa
 
Ze Mimi ze i don't know speak Swahili
Aaaaahhaaaah
Cc:shilole

Haha, ila me nimewahi wakimbiza hata st. hawakutoboa.
Nakumbuka ilikuwa ni English forum competition ilifanyika mbeya miaka hiyo.
St.Francis, st.Mary's na st.Aggrey walikaa.
Niliwashindia kwenye kuweka viunganishi na mbwembwe za kiinglishi zote unazozifahamu
 
Shule nilosoma kitu kimoja nakichukia kila nikikumbuka ni pale mwalim wa Elimu ya kujitegemea E/K alipoanzisha mradi wa kilimo cha mapapai na mapassion.

Kila mwanafunzi alikabidhiwa miche yake daa mimi miche yangu ikafa yote maana kila siku kumwagilia maji asubuhi na jioni. Mimi nikawa simwagilii maji kabisaa.

Ile kitu nilikuwa sipendi sana...nikacharazwa sana.
 
Huwa napata taabu sana nikikutana na mzungu huwa nahisi kufa kufa
Kuna kaka mmoja alikuwa kipanga kweli enzi tunasoma, alimaliza UDSM na kwenda USA kwa Masters. Nilipokutana nae ananiambia wazungu walipata shida kumwelewa pronunciation yake, tulikumbuka alivyokua anatuacha darasani. Kwakweli debates clubs zirudishwe zilitupa confidance.
 
Aseee....!
Shule ni kwetu ilikuwa kila alhamis unapikwa uji Wa mchele na wapishi ni ss wanafinzi
Huu uji Wa mchele mi naupenda sana kwahiyo nilikuwa kila unapopikwa nilipenda niwe mmoja Wa wapishi ili niufaidi vizuri kule kule jikoni
Kingine kipindi cha masika ule muda Wa kuridi mvua ikianza kunyesha ilikuwa bonge LA raaahaaaa tukikuta kidimbwi tu tunakigeuza bwawa aisee basi hapo ni kuogelea na kupiga mbizi kwenye maji ya ugoko
Jioni tunakuwa na kazi ya kuanika daftali kwenye moto
Da, nna mengi ya kuelezea aisee ...
 
Nakumbuka enzi za darasa la sita, mpaka darasa la saba; kitu cha "tag question" ilikuwa balaa tupu.

"You took my pen"
"________________"
(Malizia mwenyewe)
Msondo ngoma ilikuwa na raha yake asee.
 
Back
Top Bottom