St. Francis Mbeya kufungwa baada ya wazawa kushindwa kuiendesha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

St. Francis Mbeya kufungwa baada ya wazawa kushindwa kuiendesha

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by TIQO, Dec 29, 2011.

 1. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Ile shule maarufu ya wasichana Mbeya St. Francis ipo hatarini kufungwa baada ya wazawa kukabidhiwa toka kwa masister wa shirika la Mtakatifu Karoli Boromeo kwa kile wanacho dai wanaenda kihasara kwani masister hao waliingia mikataba minono na walimu walio kuwa wanafundisha hapo na kuwalipa ujira wa Tsh. 2m. sasa wazawa wamechemka baada ya kugundua wanaendesha kihasara. Serikali imeipigia magoti Jimbo katoriki la Mbeya kutoifunga shule hiyo kwani ilikuwa inautangaza mkoa wa Mbeya.
   
 2. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,200
  Likes Received: 3,810
  Trophy Points: 280
  Wazawa wapi, masista au wanajamii?
   
 3. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #3
  Dec 29, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Mapadre weusi na masista weusi
   
 4. Boniface Evarist

  Boniface Evarist JF-Expert Member

  #4
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 1,100
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Mbona habari haina source au evidence? Nadhan anatania huyu!
   
 5. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #5
  Dec 29, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,200
  Likes Received: 3,810
  Trophy Points: 280
  Kama ni hivyo then that will be a disaster. Historia ya wakatoliki haijawahi kuonyesha kushindwa katika elimu, inakuwaje nao wanaanza kuingiliwa na kirusi kinachoitafuna elimu ya Tanzania
   
 6. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #6
  Dec 29, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Kumbe Masister siyo wazawa??????!!!! najifunza mambo mengi sana hapa JF kwakweli.
   
 7. n

  newazz JF-Expert Member

  #7
  Dec 29, 2011
  Joined: Mar 28, 2009
  Messages: 471
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 60
  Kuna changamoto nyingi sana, kuwapa wazawa madaraka kuendesha mambo. Maeneo ni mengi, ukianzia hapohapo Roman Catholic, parish yeyote iliyokuwa ikiendeshwa na wazungu, wakikabidhi kwa uongozi wa Jimbo ambao ni mapadri, masista weusi,basi kila kitu kinakufa. Kama walikuwa na miradi, mafunzo yoyote vyote hivyo vinakufa. Hata bustani za maua zinakuwa. Tatizo ni uongozi dhaifu wa kulindana, ukabila, umaeneo nk, vyote vinaua taasisi zetu.

  Shule ya Mt. Fransis ni mojawapo ya mifano halisi ya udhaifu wa uongozi, tunapoachiwa sisi wazawa, Je wazawa hatuwezi?

  Sijajua hata ile shule ya Marian- Bagamoyo kama na yenyewe inaendeshwa na mashirika ya kikatoliki ya kimataifa au chini ya Jimbo!!!

  Tanzania, Tanzania kwanini watoto wako wamekuwa hivyo???
   
 8. kingadvisor

  kingadvisor Senior Member

  #8
  Dec 29, 2011
  Joined: Dec 21, 2011
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari hii si nzuri ni mbaya.NGO na shule nyingi za NGO Tanzania hufa zikishakomaa kwa migogoro ya ndani na mashambulizi toka ndani na nje kuwa uongozi unakula pesa n.k.Zinapoanza kwa shida huwa hakuna anayejali.Zikikomaa kwa juhudi za hao waanzilishi mashambulizi huanza.Kila mtu anataka aongoze.Waanzilishi wa mwanzo huwa ni wachapa kazi sana na waliodhamiria lakini wanaofuata baadaye huwa wengine ni watafuta maslahi tu wasiokuwa wachapa kazi na huwa wengi hawajui fund mobilization.Hudhani waliowatangulia walikuwa na uwezo wa kukusanya pesa tu kwa kuchapa kadi na kusambaza vibarua vya kuomba kuchangiwa.

  Hawajui kuwa mtu kuchangia haangalii tu barua au kadi iliyoandikwa vizuri bali na mtu mwenyewe.Hakuna kitu kigumu duniani kama kumchomoa mtu pesa yake akuchangie.Hao walioondoka waliaminiwa ndani na nje ya nchi.Watanzania wengi kuaminiwa kwetu wengine hata kwenye kata bado.Sasa ukiIchukua shule kama ST Francis wakati kiwango cha kuaminiwa pengine hata mkoa wa mbeya bado kidogo hizo pesa za kuliendesha shule hilo utatoa wapi? Maamuzi mengine hata kama ni ya kanisa si sahihi.Warudisheni hao masista wageni.Hata kama mna tofauti zenu warudisheni kwa manufaa ya watanzania msiangalie manufaa ya kanisa katoliki mbeya tu si sahihi.Hata kama wana jeuri au viburi ni kitu cha kawaida kwa binadamu akifanikiwa kuwa jeuri na kiburi ni haki yake kwa kuwa kafikia mafanikio.

  Hata kama ingekuwa hao wageni walikuwa wanakula hela ni bora wangebaki .Ni heri kuwa na Baba Mzambi aliye mkulima hodari kuliko kuwa na baba mtakatifu mvivu shambani anayeshinda akipiga sala bila kulima.Kukosa pesa za kuiendesha inawezekana hao waliopokea sasa hivi muda mwingi wanautumia kusali shambani badala ya kulima shambani yaani kutumia muda mwingi kutafuta pesa na kusimamia miradi ya kuiendesha hiyo shule

  Naogopa isije kuwa St francis imepata watakatifu ambao uwezo wa kuiendesha hawana .Heri warudi hao masista wageni.
   
 9. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #9
  Dec 29, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  LILE sakata la walimu wa shule ya wasichana ya Mtakatifu Fransisco wa Azizi Mbeya (St.Francis) kugomea ndani ya nyumba limechukuwa sura mpya baada ya Serikali mkoani hapa kuingilia kati na kuliangukia kanisa Katoliki kutoifunga shule hiyo kama ilivyotarajiwa baada ya masista wenye asili ya kiasia wa Shirika la Mt.Karoli Boromeo ambao ndiyo viongozi na waendeshaji wa shule kuitwa mara moja na mama yao mkuu kurudia haraka nchini Ubelgiji kuhofia kuvamiwa na walimu hao.


  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Abbas Kandoro akizungumza katika kikao na viongozi wa kanisa katoliki Jimbo la Mbeya alichokiitisha ofisini kwake jana amemsihi Askofu Evaristo Chengula wa kanisa jimbo ambaye ndiye mmiliki wa shule hiyo kuvuta subira na kubadilisha wazo la kuifunga shule hiyo kwani serikali imeamua kuingilia katika kulishughulikia suala hilo haraka iwezekanavyo.


  "Tunampa pole Baba Askofu tunajuwa anaumia na krismas kwake imepita bure,avute subira lakini ajuwe anashughulika na binadamu aendelee kuwa mvumilivu hasifunge shule…shule hii inatuletea sifa katika Mkoa na taifa kwa ujumla na kutokana na ubora wa elimu inayotoa imekuwa ni tegemeo na kimbilio la wengi, wanafunzi zaidi ya 360 wanaosoma hapo watayumba,wazazi watachanganyikiwa,nawaagiza pande zote mbili na wanasheria wenu mketi kwa pamoja na kulimaliza suala hili kwa amani na utulivu…ila siingilii masuala ya kisheria,"alisema.


  Hata hivyo Mkuu wa Mkoa Kandoro alituma ujumbe wake ulioongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya,Evans Balama kwenda kwa Askofu Chengula kufikisha salamu hizo na kuahidi kulishughulikia tatizo hilo mapema ambapo kwa wake Askofu Chengula aliiomba serikali kulishughuliki suala hilo kabla ya januari,8 siku ya kufungua shule za bweni kabla masista hao ambao ndiyo Meneja wa shule hawajaondoka nchini ili aweze kuwasihi kurejea shuleni vinginevyo ataifunga shule kutokana na kukosa walimu na Uongozi wa kuiendesha.


  Kwa mujibu wa maelezo ya Mkurugenzi wa idara ya elimu Jimbo Katoliki la Mbeya,Padri Innocent sanga alisema awali masista wa shirika la Mtakatifu Fancisco wa Asizi waliendesha shule hiyo kwa makubaliano ya mikataba mizuri na walimu hao kuwalipa mishahara minono iliyofikia wastani wa Tsh.Mil.2 ,lakini baada ya kumaliza mkataba wao na kuikabidhi shule kwa Askofu Chengula, Jimbo lilishindwa kuiendesha kutokana na kutumia fedha nyingi kuwalipa walimu.


  "Wenzetu walikuwa na fedha nyingi lakini sisi hatuna chanzo kingine cha kuendesha shule zaidi ya kutegemea ada kwani shule tunaiendesha kama huduma na siyo kibiashara,tuliamua kukaa nao kuwaeleza kusudio leo la kubadilisha mikataba mipya, tuliangalia tunatumia zaidi ya Sh.Mil.548,000,000 kulipa mishahara ya walimu sawa na asilimia 76 ya mapato ya shule na Sh.Mil176,000,000 sawa na asilimia 24 ndiyo inasalia na tunalazimika kutumia fedha za gharama ya bweni na chakula ili kufidia mishahara mikubwa na ndiyo maana ilipofika mwaka huu tulishindwa kabisa kuiendesha shule"alisema.


  Aliongeza,"Askofu aliamua kuwaeleza adhma ya kufuta mikataba mipya ya walimu wa kudumu,kulipa haki zao zote stahili kwa mujibu wa sheria,kuajiri upya walimu waliopo na wapya katika mikataba ya muda maalum na masharti mapya ilimradi yakubaliwe na mwajiri,kufuta marupurupu yote ya walimu ambayo si ya kisheria.


  Alitaja marekebisho mengine ya mikataba kuwa kulipa mishahara kadri ya ‘scheme of service and salary structure' mpya ambayo jimbo limeandaa,kuanzisha malipo na marupurupu mapya kadri ya uwezo wa shule na kwa mwaka 2011 shule isipandishe ada kufikia Tsh.Mil.2 kama ilivyokusudia ili kuendelea kuwalipa walimu miashahara minono na badala yake walimu walipwe wastani wa Sh.600,000 na ada ibakie Sh.Mil.1.7.


  Padre sanga alisema hata hivyo walimu hao hawakuwa tayari kupokea marekebisho hayo na hivyo kanisa kuamua kuwaachisha kazi na kuwataka wahame ifikapo Januari,28,2011 ndani ya nyumba za shule walizokuwa wakiishi kuwapisha walimu wengine wapya walioajiriwa hali ambayo ilipingwa na walimu hao kwa kuomba hati maalum katika baraza la nyumba kuzuia wasitokea hadi kesi yao ya msingi iliyopo Tume ya usuluhishi kesi za ajira na kazi (CMA) itakapomalizika.


  Alisema walimu hao pia walipinga kuhama kupitia wakili wao wa awali Mwakolo and Company kuwa watakuwa tayari kuhama wakati watakapolipwa madai yao ‘repatrition expenses',yaani gharama za kuwarudisha makwao ambapo baada ya kila mmoja kuorodhesha madai yake katika walimu tisa zaidi ya Sh.Mil.31.9 zilipatikana na kanisa lilikuwa tayari kuwalipa lakini baadaye waligoma na kuachana na wakili huyo.


  Amewataja walimu hao wanaolidai kanisa na idadi ya kiasi cha fedha katika mabano ni Rozalia Kimario aliyedai zaidi ya Sh.Mil.6.7,Mary Njele (Sh.Mil.6.6),Yessaya Musyani (Sh.336,000),Lenadina Kagero(Sh.263,000),Ernest Njole (Sh.332,000),Benezer Msangi (Sh.Mil.6.5),Ursula Ndeki (Sh.Mil.7.5),Agatha Nyagimba (Sh.328,000) na Simon Mapunda (Sh.Mil.3.2).


  Ametaja madai mengine ya walimu ambayo kanisa lilikuwa tayari kulipa kwa mujibu wa sheria ni pamoja na mshahara wa mwezi mmoja badala ya notisi ambapo Askofu alikuwa tayari kuwalipa mishahara ya miezi sita,'disturbance allowances','severance allowance' na ‘Certificate of service cause of termination(Redundance)'.


  "Hapo ndipo ilipoanza mivutano na walimu kulifikisha kanisa katika baraza la ardhi na nyumba pamoja na Tume ya usuluhishi ambapo ‘order' ilitolewa januari,17,2011 walimu walikaa katika nyumba hizo kwa kufuata amri ya baraza la ardhi na nyumba hadi kesi ilipokwisha disemba,22 ,2011 kesi yao ilipotupiliwa mbali,na kesi nyingine walimu waliyofungua (CMA) kuitaka tume itamke kuwa "walimu hao hawakuachishwa kazi kihalali na waendelee na kazi" ilitupilia mbali pia,"alisema Padri Sanga.


  Padri huyo alisema kutokana na maamuzi ya baraza la ardhi na nyumba kanisa liliiomba kampuni ya Yono auction mart & Cout broker kuwaondoa walimu hao jambo lililoleta mgongano wa maamuzi baada ya Mwenyekiti wa tume ya usuluhishi Boniphace Nyambo kuliandikia Jeshi la Polisi hati ya kuwarudisha ndani ya nyumba majira ya saa 12 jioni jambo lililopelekea kuhoji uhalali wa Tume hiyo kuandika ‘order' wakati awali suala la nyumba lilishughulikiwa na baraza la ardhi na nyumba na kutoa hati iliyokwisha muda wake baada ya kutupilia mbali shauri hilo.


  Alisema Jeshi la polisi liligonga ukuta kupata ufunguo za kuwafungulia walimu hao ndipo walimu walipochukuwa hatua ya kuvunja makufuli ya nyumba zao na kuingia ndani ya nyumba hizo kuendelea kuishi hali ambayo iliwashtua masista ambao nao wanaishi ndani ya shule hiyo na hivyo kuhofia kuvamiwa na walimu na hivyo kuamua kumpigia simu mama yao mkubwa huko nchini Ubelgiji ambaye aliwataka waondoke haraka na hivyo walimuaga Askofu Chengula na kuondoka siku ya pili wakiiacha shule peke yake.


  Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wa habari hizi akiwa safarini kuelekea mkoani Iringa walipo masista wenzao wa Shirika hilo,mmoja wa viongozi wa masista hao,Sr.Sagaya alisema amesikitishwa na kitendo kilichofanywa na walimu hao kutishia amani na utulivu na kwamba alilazimika usiku huo kumpigia simu Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya,Advocate kumuelezea hali hiyo lakini katika hatua ya kushangaza Kamanda Nyombi alibariki kitendo hicho na kumuahidi kuwa watakuwa salama na hakutakuwa na uvunjifu wowote wa amani.


  "Sisi tulijiuliza Polisi wanabariki walimu kuvunja nyumba?,lakini pili tukahoji kama walimu hao wamekaidi kumsikiliza Baba Askofu ambaye ndiyo mwajiri wao,je watatusikiliza sisi?, watakuja kutuvamia kwa maana zile sauti za nyundo zilitunyima raha na hamu ya kuendelea kuishi,tukampigia mama mkubwa Ubelgiji akasema tukimbilie kwa wenzetu Iringa tupo Iringa na amesema hali ikizidi kuwa mbaya turudi Ubelgiji,"alisema Sr.Sagaya.
  Thompson Mpanji, Redio Maria Mbeya Desemba 28, 2011
   
 10. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #10
  Dec 29, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Hao waliopewa kuendesha ni mapadre na masista weusi na wazaliwa wa hapa hapa Tanzania hatuwezi waita wazawa?
   
 11. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #11
  Dec 29, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Nimejitahidi kusoma habari yote! inavyoonekana walimu hawataki kupambana na changamoto mpya za kazi watakapoachishwa. Ni mtazamo wangu! Kuna makampuni mengi duniani hukaa chini na wafanyakazi wao kuzungumzia hali ya kampuni kifedha nk, na wakati mwingine wadau wote hufikia hatua ya kujibana/hata kupunguziana mishahara kwa malengo ya kuisaidia kampuni hadi itakapotengemaa kiuchumi na baadae wote wanafaidika.
  Kwa nini basi walimu na wenye shule wasikae chini, wakakubaliana na hali ya mambo ilivyo kwa kuelezana ukweli zikiwemo vielelezo vya namna ambavyo pesa inavyotumika nk ili wote kwa pamoja wajiridhishe na mwisho kukubaliana kwa ajili ya maendeleo ya shule, elimu na taifa kwa ujumla? Kuna kitu inawezekana hakijakaa sawa na watu hawataki kusema wazi.
   
 12. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #12
  Dec 29, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  ....Bahati mbaya wandishi ameandika habari kwa kuangalia maelezo ya upande mmoja, ingeuwa vyema sana kama angepata pia maelezo ya upande wa walimu..

  ..Waalimu wangu sana Mama Kagoro na Msyani aka Boxer wasingeweza kufanya ukorofi wa aina hiyo, lazima watakuwa na hoja za msingi, by the way Tsh. 200,000/Tsh 300,000 tu za kuwawezesha kurudi makwao? haijakaa vizuri...
   
 13. YEYE

  YEYE JF-Expert Member

  #13
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 440
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu kwani ye mwenyewe hawezi kuwa source!?
   
 14. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #14
  Dec 29, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Bongo bana, yaani mtu alikuwa analipwa 2mn halafu uje umpe 600,000???????????? To be frank, hiyo gharama ya uendeshaji ingepelekwa kwa wateja (wanafunzi) na si kupunguza mshahara wa walimu. Si ndio kanuni ya biashara hiyo? Hata kodi huwa zikiongezwa kwa wafanyabiashara siku zote zinarushiwa wateja. Watu wanalipa mpaka 5mn hapo Tanzania kwa ada kwa shule za ajabu ajabu tu! sasa kwa nini wasilipe say 2.5mn hapo st Francis halafu watoto kadhaa wakapigwa mtindo wa scholarship? Lakini wazo la kufunga shule si sahihi hata kidogo!
   
 15. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #15
  Dec 29, 2011
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Nadhani baba askofu hana busara za kidini.

  Huwezi kurudisha nyuma mshahara. Ongezea ada kwa wanafunzi.
   
 16. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #16
  Dec 29, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,940
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Inanikumbusha Loyola ,alipokuwepo yule mzungu kabla hajafa ilikuwa niu shule yenye muelekeo saa hizi ndio imekuwa kama shule za kata ,ngoma imeshikwa na mswahili,sijui sisi ngozi nyeusi tuna tatizo gani Grrrrrrrrrrrr
   
 17. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #17
  Dec 29, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,713
  Trophy Points: 280
  habari imenisikitisha sana
  shule ilikuwa kwenye kiwango kizuri cha elimu
  naomba kujuzwa hivi serikali huwa inatoa ruzuku kwenye shule
  binafsi/mashirika kama inavyotoa kwa vyama vya siasa?!!
   
 18. MKUNGA

  MKUNGA JF-Expert Member

  #18
  Dec 29, 2011
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 443
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mshahara siku zote unapanda haushuki hata 50/-
   
 19. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #19
  Dec 29, 2011
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,445
  Likes Received: 7,183
  Trophy Points: 280
  Shule ya watoto wa vibosile,enzi zile
   
 20. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #20
  Dec 30, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  "Alitaja marekebisho mengine ya mikataba kuwa kulipa mishahara kadri ya ‘scheme of service and salary structure' mpya ambayo jimbo limeandaa,kuanzisha malipo na marupurupu mapya kadri ya uwezo wa shule na kwa mwaka 2011 shule isipandishe ada kufikia Tsh.Mil.2 kama ilivyokusudia ili kuendelea kuwalipa walimu miashahara minono na badala yake walimu walipwe wastani wa Sh.600,000 na ada ibakie Sh.Mil.1.7.
  "

  u mean furahisha walimu 40 umiza wanafunzai/wazazi 360? hapa naona kanisa lipo sawa kabisa, sote tunafahamu kipato cha mtanzania hapa naona wazazi wengi itawashinda kulipa kiasi kikubwa cha ada. ili kumatch standards ni kweli ada lazima iongezwe
   
Loading...