St. Florence Academy: Watoto kuibiana na utukutu ni moja ya somo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

St. Florence Academy: Watoto kuibiana na utukutu ni moja ya somo

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by jongoo, Jun 3, 2012.

 1. j

  jongoo Member

  #1
  Jun 3, 2012
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Japokuwa maadili na tabia njema huanzia nyumbani ila shule naamini ina mchango mkubwa wa kuwafunza watoto hayo. Wizi baina ya watoto umekithir shule hii ukimpa mtoto kitu uhakika wa kurudi nacho mdogo. Na watoto kupigana nahisi labda ni mmoja wa michezo shuleni hapo. Nimeripoti kwa walimu na kuandika barua naona as if walimu wanapenda tabia hizo. Au niseme wizi ni moja ya somo katika shule ya mmiliki mchaga? Inakeraaaa!
   
 2. Amina Thomas

  Amina Thomas JF-Expert Member

  #2
  Jun 3, 2012
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 272
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  nakuunga mkono asilimia 200! Shule hii kwa wizi imekithiri. Kila siku unanunua vitabu vinaibiwa. Mimi nilifuatilia nikagundua kua walimu pia ni wezi. Tena ndio wanaongoza. Kuna watoto wezi na walimu pia. Inakera sana!
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,468
  Trophy Points: 280
  poleni na bado tabia zingine mbovu
  kama kutembea na wanafunzi
  huku unalipa malaki na mamilioni ya pesa
   
 4. S

  Shangazi JF-Expert Member

  #4
  Jun 3, 2012
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 307
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Duh! nilijua matatizo haya ni kwangu tu kumbe wengi. Inaelekea shule kuna kitu haifanyi. Ingekuwa serious kukemea kila siku kwa watoto na kuwaathibu watoto vibaka na wanaopiga wenzao tatizo lingeisha ila shule kama vile haijali iko kifedha zaidi. Mwanangu anaibiwa na kubondwa mpaka akaomba kuhama shule. Je wanaoibiwa wakiamua kuiba si inakuwa wamepta somo tayari kama alivyosema jongoo. Ukiwauliza waalimu wanasema ni shauri ya watoto wa boarding. Saa nyingine mtoto anakimbia akicheza anategewa nyuma anaanguka, mara anapigwa vibao bila kosa. Duh, Mama Assey do something we are tired ooo!
   
 5. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,265
  Trophy Points: 280
  And I thought that was the best school kati ya akademia zisizo international! Fundisheni wenenu wrestling, natangaza rasmi twisheni
   
 6. j

  jongoo Member

  #6
  Jun 4, 2012
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  watoto wanaoiba wanajulikana kwa wanafunzi na walimu coz saa nyingine wanadokoa wakiwa wanaonekana. Wizi ni haza pale wanapokuwa mapunziko na mabegi wametindika madarasani kwao. Mtoto akitaka kwenda kusema kwa mwalimu anachimbwa mkwara mzito wa kubondwa. Yaani uswahiliiiiii kama zile shule za kanumba. Tunalipa ada kubwa ili iweje sasa wewe mkuu wa shule? Kaeni ongeeni na watoto, shirikisheni wazazi wa watoto watukutu. Aaaaaaghhhhhhhrrrrrrrrrrr!
   
 7. Liz Senior

  Liz Senior JF-Expert Member

  #7
  Jun 4, 2012
  Joined: Apr 19, 2007
  Messages: 485
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nafikiri kama wazazi mnapaswa kuongea kwa hasira hizi katika vikao vya PTA kama vipo. Na mliweke hili katika agenda muhimu na kumweleza huyo mmiliki wa shule wazi linavyokera. Mara nyingi vikao kama hivi utakuta mzazi mmoja au wawili tu ndio wanaoongea kukiwa na jambo, wengine wanalalamika chini kwa chini ili kuepusha watoto wao wasionekane wapo against uongozi. Mzazi una wajibu maana unalipa ada na mara nyingine hata mwanao anaweza kuwa ndie anayewa-bull wenzie.
   
 8. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #8
  Jun 4, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  ulitaka mwenywe Academy, wakati ww ulisomea UPE matokeo ndi hayo .....
   
 9. j

  jongoo Member

  #9
  Jun 4, 2012
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watu ningejua unakopatikana wallahi ningekutumia daktari wa Akili aje akupime.
   
 10. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #10
  Jun 4, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,527
  Likes Received: 19,947
  Trophy Points: 280
  hamisheni watoto ...kabla hawajaharibiwa ..mtakuja kusikia siku shule imeanza mambo ya kimombasa itakuwa ni too late tayarri
   
 11. S

  Shangazi JF-Expert Member

  #11
  Jun 4, 2012
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 307
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  ninachokiona hapa ni watoto wasio wezi watajifunza na wasio wababe watataka kujilinda na ndio mwanzo wa kuwafanya watoto wetu vibaka.
   
 12. o

  opportunist2012 Member

  #12
  Jun 4, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 92
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hiyo shule inawaandaa majambazi watakaohatarisha maisha yetu na mali zetu.Kwa kuwa wazaz wanafumbia macho madudu haya hayamkuniki hao watoto wakaanzia kwa wazaz wao kupoka mali na hata kuwapiga.
   
 13. S

  Shangazi JF-Expert Member

  #13
  Jun 5, 2012
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 307
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Opportunist, Mimi binafsi nimesha piga simu weeeeee, nimeandika msg weeeeee, nimekwenda shule na kusema weeeeee ila hakuna bailiko. Last time mtoto aliibiwa swimming costume inaingia akilini hiyo. mwee!
   
 14. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #14
  Jun 5, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Shule ziko nyingi hamisheni watoto wenu!
  Au mumelogwa?
   
 15. S

  Shangazi JF-Expert Member

  #15
  Jun 5, 2012
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 307
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Another problem ni transport mwe! migari mibovu mara nyingi watoto huchelewa kurudi. Chelewa kulipa ada wewe, mtoto anarudishwa home first day no discussion
   
 16. Kurzweil

  Kurzweil JF-Expert Member

  #16
  Jun 5, 2012
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 4,903
  Likes Received: 4,759
  Trophy Points: 280
  Ha ha ha ha hiyo kiboko.
   
 17. M

  MKABESA Member

  #17
  Jun 6, 2012
  Joined: Oct 15, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bora hiyo . Wa kwangu aliibiwa biblia mpya. Niliandika na namba za simu page ya kwanza. Ina maana hata mzazi hajaziona anirudishie?, je mwalimu, je mfagizi?, je mpishi? je mlinzi, je dereva .Nilipiga simu ola. nikaanika kwenye diary ola; nikafika shuleni ola. hata leo naiomba kwa kuwa bado naihitaji .
   
 18. j

  jongoo Member

  #18
  Jun 6, 2012
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh hii kali zaidi. Malalamiko ni mengi ila mkuu wa shule akiona yamezidi najua atampa hela kidogo Kibonde wa Clouds FM amsafishe kwenye jahazi kwa maneno ya kipuuzi bila kushughulikia tatizo. Niseme wazi shule ile ina watoto watukutu na wa kukemea ni shule kwa sababu inawezekana home hawafanyi hayo. wamiliki msifananishe kuendesha shule na Bar ya Rose Garden mwe!
   
 19. b

  buguruni Member

  #19
  Jun 6, 2012
  Joined: Feb 5, 2010
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KUMBE TUKO WENGI? WANGU ALITEGEWAGA AKAANGUKA NA KUUMIA NILIPOTAKA MAELEZO ZAIDI NIKAAMBIWA WANAFATILIA MPAKA KESHO. MTOTO ANASEMA ALITEGEWA MAKUSUDI NA MVULANA.Plus vimbwanga vya wizi ndio usiseme.
   
 20. j

  jongoo Member

  #20
  Jun 8, 2012
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Buguruni pole sana. Kweli malezi ya shule hii sifuri. Wanapaswa kutambua muda mwingi wa watoto huutumia shuleni wakirudi ni home works na kulala hivyo walimu wanalo jukumu nkubwa la malezi
   
Loading...