St. Florence Academy: Mabasi mabovu, Wanafunzi kusimama katika school bus si halali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

St. Florence Academy: Mabasi mabovu, Wanafunzi kusimama katika school bus si halali

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Shangazi, Jun 18, 2012.

 1. S

  Shangazi JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2012
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 307
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kwanza, mabasi ya wanafunzi ya shule hii ni mabovu kiasi cha kushangaza kiasi cha kutishia usalama wa watoto wetu.

  Pili, Wanafunzi wanajaa sana kwenye mabasi kinyume na sheria za usalama barabarani ilhali wote wamelipa hela sawa ya usafiri. Pata picha mtoto mdogo wa darasa la kwanza au pili aliyeamka saa 11 alfajiri akiwa anarudi nyumbani saa kumi jioni amechoka huku amesimama na gari ikitumbukia katika barabara mbovu za sinza zenye mahandaki. This is not fair!

  Je? huu ni uungwana?
   
 2. UPOPO

  UPOPO JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 1,371
  Likes Received: 718
  Trophy Points: 280
  nENDA KAMWELE MKUU WA SHULE ,USIANDIKE HAPA UNLESS UNATAKA KUMWARIBIA BIASHARA.NENDA STRAIGHT SHULENI KWAO PELEKA MALALAMIKO
   
 3. S

  Shangazi JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2012
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 307
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Nipeleke malalamiko mara ngapi ndio nije kuandika hapa. Malalamiko kwa maandishi na mdomo wala si mara moja. Hapa ni just ku share na wazazi wenzangu na wewe si lazima uchangie
   
 4. UPOPO

  UPOPO JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 1,371
  Likes Received: 718
  Trophy Points: 280
  Pole basi kama shule yenyewe haisikilizi malalamiko ya wazazi inabidi uchukue hatua ,ama kumwamisha mtoto au kuripoti polisi pindi uonapo gari limejaa na watoto wamesimama.Watoto ni kama abiria wengine tu sheria inasema wote wanatakiwa wawe kwenye vitu .Sasa hapo kwa jeshi letu huwa wawazingatii hii sheria kabisa watakuambia kuna upungufu wa mabasi au rasilimali
   
 5. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,284
  Likes Received: 1,432
  Trophy Points: 280
  hapa mzazi na wewe utakuwa na matatizo, unakubalije mtoto wa darasa la kwanza aamke saa 11 na kurudi saa 10 jioni?

  Je ni lazima umpeleke mtoto shule hiyo? kwa nini hukufanya utafiti wa kutosha kabla ya kumpeleka shule hiyo? Unakubalije mwanao kutumia gari mbayo unajua fika usalama ni mdogo/

  Sisi wazazi kuna wakati hatutimizi majukumu yetu kama wazazi halafu tuwanatupia lawama mashuleni.

  Assume wazazi wote wagome kutumia huo usafiri, unadhani mwenye shule ataendelea na hiyo service sijui biashara?

  Ninatoa huduma ya kuwapeleka watoto shule na kuwarudisha nyumbani kwa cost ya Tshs 20,000 kwa siku kama unaishi maeneo ya Mikocheni, Sinza, Makumbusho, Kijitonyama, Mwenge.
   
 6. S

  Shangazi JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2012
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 307
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Niseme ni mpangilio mbaya tu wa route na gari kuwajibika kuwapitia watoto weeengi. Nilimpeleka mtoto shule hiyo nikijua sinza na mikocheni ni karibu hivyo hataamka mapema matokeo anachukuliwa saa 12 kamili na anazunguka kwenye gari mpaka 1.30 ndio anafika shule. Na mashimo ya sinza basi ni balaa. Naamini kama gari ingebeba wanafunzi wachache maana yake angechukuliwa hata moja kasoro ila ndio shule iko kibiashara zaidi na si haki.
   
 7. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #7
  Jun 18, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,284
  Likes Received: 1,432
  Trophy Points: 280
  gari ikibeba wanafunzi wachache means you have to pay more to cover the fixed running costs.

  Halfu issue nyingine wazazi pia muwajibike, kwani ni lazima utumie school bus kupeleka mwanao shule? Je umeshawasiliana na wazazi wenzio wenye watoto shuleni hapo mkajadiliana cha kufanya kuepukana na matatzio hayo ya usafiri? Au mnaendelea kuvumilia hadi janga litokee?
   
 8. S

  Shangazi JF-Expert Member

  #8
  Jun 18, 2012
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 307
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Ushauri mzuri wa kuunganisha nguvu wanafunzi wa jirani. Its too much for the kids!
   
 9. S

  Shangazi JF-Expert Member

  #9
  Jun 18, 2012
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 307
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  wamiliki wa shule waige kwa shule nyinginezo jinsi walivyo makini ktk usafiri
   
 10. b

  buguruni Member

  #10
  Jun 22, 2012
  Joined: Feb 5, 2010
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Issue ya usafiri shule hii hata mimi kwangu ni kero. Mwanangu wa kwanza kuchukuliwa na wa mwisho kurudishwa na wale wanafunzi wakubwa wakati wa kurudi huweka mabegi kuwahi seat na mwanangu ananiambia everyday wakati wa kurudi husimama na one day alisinzia na kuanguka ndani ya basi. Nilimwambia transport officer akasema atashughulikia lakina wapi. Nimeshakumbushia wee lakini kaputi mpaka leo. Yaani inaniuma sana sana hapa nalia mwenzenu:A S confused:
   
Loading...