SSRA Kuwalipa Wafanyakazi wa Geita Gold Mine Mafao yao ya kujitoa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SSRA Kuwalipa Wafanyakazi wa Geita Gold Mine Mafao yao ya kujitoa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by da50v1, Aug 3, 2012.

 1. d

  da50v1 Member

  #1
  Aug 3, 2012
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kwanini SSRA ikubali kuwalipa mafao wafanyakazi wa GGM na sio wafanyakazi wote ambao wako kwenye mifuko ya jamii?

  >>>>>

  Kumb. Na. CB.75/396/VOL.II/16 DATE: 30/07/ 2012
  Meneja Mkuu,
  Geita Gold Mining Ltd,
  P.O.Box 532,
  GEITA.
  YAH: UFAFANUZI WA SSRA KWA WAFANYAKAZI WA MGODI WA GEITA
  GOLD KUHUSU FAO LA KUJITOA
  Tafadhali husika na kichwa cha habari hapo juu. Pamoja na kikao kilicho fanyika tarehe
  25/07/2012 katika Mgodi wa Geita Gold na kuhudhuriwa na kiongozi wa Mamlaka ya
  Usimamizi wa Sekta ya hifadhi ya Jamii (SSRA) na wafanyakazi wa Mgodi wa Geita
  Kwanza kabisa tunatoa shukrani zetu za dhati kwa kupata nafasi ya kutoa ufafanuzi
  kuhusu kusitishwa kwa fao la kujitoa. Katika kikao hicho mliitaka Mamlaka kutoa majibu
  ya hoja zenu. Hoja ambazo zimekuwa sababu za wafanyakazi kupinga Sheria inayozuia
  kuwepo kwa fao la kujitoa:
  Napenda kuwafahamisha kwamba hoja zote zilizotolewa ni za msingi sana na
  zitatusaidia kuja kwenu mara mtakapotupangia ili kutoa ufafanuzi zaidi. Hata hivyo hoja
  inayohitaji ufafanuzi wa haraka ni inayouliza; kutokana na hali na mazingira ya kazi je
  wafanyakazi wa mgodi wenu wataendelea kupata fao la kujitoa baada ya marekebisho ya
  Sheria? Jibu lake ni ndiyo. Kutokana na mazingira ya kazi na aina za mikataba
  mliyokuwa nayo, mfanyakazi atakuwa na uhuru wa kuchagua kuendelea na pensheni au
  kupewa fao la kujitoa. Kama mlivyofananuliwa na SSRA wakati wa kikao, wale wote
  ambao waliingia mikataba kabla ya mabadiliko ya S heria watalipwa fao la kujitoa mara
  mikataba yao itakapoiva. Wafanyakazi wapya watashuriwa kujiunga na Mfuko wa Akiba
  unaruhusu wenye fao la kujitoa.
  Kwa vile kwa mujibu wa Sheria, Mfuko wa msingi (mandatory Scheme) unaotoa fao la
  kujitoa ni GEPF, Mamlaka itawashauri wafanyakazi wapya kujiunga na Mfuko huo. Hii ni
  Barua zote za Kiofisi zitumwe kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka
  Page 2
  baada ya kutoa miongozo pamoja na kutoa elimu kwa kushirikisha Mifuko yote ili
  wafanyakazi wa Mgodi wa Geita Gold waweze kuelewa aina za Mifuko na aina za mafao
  ili kufanya maamuzi sahihi.
  Vile vile kwa kuzingatia hali halisi na ugumu wa mazingira ya kazi za migodini, Mamlaka
  itaangalia wakati wa kuandaa miongozo, uwezekano wa kuwa na skimu inayoendana na
  mahitaji ya wafanyakazi hao katika Mifuko Mingine kama vile NSSF,PPF,LAPF na PSPF.
  Hivyo tunachukua fursa hii kuwafahamisha kuwa wafanyakazi wa Mgodi wa Geita Gold
  kwamba watalipwa mafao yao ya kujitoa mara mikataba yao itakapoiva na kuruhusiwa
  kuchagua kujiunga na Mifuko ya Pensheni au Mfuko wa Akiba.
  Shukrani za dhati kwa ushirikiano wenu.
  Wenu,
  MAMLAKA YA USIMAMIZI NA UDHIBITI WA HIFADHI YA JAMII
  Irene Isaka
  MKURUGENZI MKUU
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,921
  Likes Received: 83,430
  Trophy Points: 280
  Dah! Kumbe wakitikiswa kidogo tu wanaanza kutapatatapa na kubadilisha maamuzi yao. Wafanyakazi wote wa Tanzania wangekuwa na msimamo kama hawa basi hiyo sheria ya kuwadhulumu Wafanyakazi mafao yao eti hadi wafike miaka 55/60 ingefutwa mara moja.
   
 3. tonnyalmeida

  tonnyalmeida JF-Expert Member

  #3
  Aug 3, 2012
  Joined: Feb 1, 2012
  Messages: 226
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Hakuna sababu ya msingi ya kutufanya watanzania kama mazuzu... Kifupi hilo Jambo la kuchukua mafao when am 55 halina mashiko na haihitaji ufike chuo kikuu ili utambue Hili.

  Nlishasema katika moja ya Post zangu kuwa Haya yoye na migogoro yote hii kati ya wafanyakazi na serikali inaletwa na Serikali yenyewe..

  Tuliwahi kuwekewa hapa Jamvini Taarifa ya ofisi ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa Hesabu za Serikali inayoonyesha Jinsi Serikali "ILIVYOKOPA" Kutoka kwenye hayo mashirika huku ikisema 'NI UWEKEZAJI WAKAWAIDA" wa hiyo mifuko na sasa wameshindwa kulipa wanataka sisi wafanyakazi tunaolipa kodi tukiwa na vimishahara vyetu vidogo ndio Tufidie hasara ya Pesa ilotumiwa na serikali kuweka miradi ya anasa bila Mipangilio.. HILI JAMBO HALIWEZEKANI

  Ukienda UDOM kwenye Collage ya HUMANITY utakutana na Majengo kama CAFETERIA, LECTURE THEATRES na HOSTEL ambazo hazina watu wa kuzitumia wakati LECTURES hawana nyumba za Kutosha wengine wamepangishiwa Chumba kimoja kimoja na wengine wamepanga wenyewe.


  WAPENDE WASIPENDE PESA ZETU WATATUPATIA TU UNLESS WANAHITAJI MAPINDUZI..
   
 4. fmlyimo

  fmlyimo JF-Expert Member

  #4
  Aug 3, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 271
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 45
  Hiyo ndiyo nguvu ya umoja. Sekta nyingine mnangoja nini? Jifunzeni kwa wenzenu. Au mmeridhika?
   
 5. Lawrence Luanda

  Lawrence Luanda JF-Expert Member

  #5
  Aug 3, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 706
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wao wanamikataba ya muda ndo mana wanaruhusiwa so wengine ndo hadi tufe familia zetu zirithi sio?
   
 6. Utotole

  Utotole JF-Expert Member

  #6
  Aug 3, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 6,344
  Likes Received: 3,178
  Trophy Points: 280
  Nadhani inawezekana kabisa kuwalazimisha wabadili sheria hii japo itakuwa ngumu sana hasa kama ni kweli pesa yote wameshatumia
   
 7. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #7
  Aug 3, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Yaani sielewi elewi ina maana wa migodini tu ndiyo watakao lipwa na si wote...
   
 8. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #8
  Aug 3, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Mikataba ya muda maana yake nini? wengine tuna mikataba ya nini?
   
 9. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #9
  Aug 3, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,320
  Likes Received: 5,611
  Trophy Points: 280
  Sote tukachukue pesa zetu!!tuanze upya kwa manufaa ya chama cha manyonyaji!!!
   
 10. t

  tusichoke JF-Expert Member

  #10
  Aug 3, 2012
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 1,286
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Nakuunga mkono hakuna cha GEITA GOLD MINE wala nini wanatufanya watanzania mazuzu ,walipe mafao km zamani na hiyo serikali ya dhaifu irudishe fedha walizokopa vinginevyo serikali hii kandamizi itamaliza muda wake vibaya,serikali gani hii kila inachofanya hakifai na si ajabu itakimbilia mahakamani km kawaida yake,shame on them
   
 11. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #11
  Aug 3, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  wazungu walisema: "Divide and rule"
  wazungu weusi kutoka tz wamefanya innovation na kusema: "Divide and exploit"

  Wewe tu kajifilie zako huko!! ..poleni sama Watanzania na sasa Malawi ndio haoooooooo wako mlangoni!

   
 12. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #12
  Aug 3, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Watu wa migodini wala msishangilie.
  Jiulizeni wanaposema Mtalipwa mpaka MIKATABA YENU 'ITAKAPOIVA'
  Mnaelewa wanamaanisha nini?
  Mkataba 'KUIVA' wanamaanisha mikataba gani?
  Baadhi ya migodi waliwauliza SSRA hilo swali lakini walishindwa kulijibu zaidi ya kujikanyaga kanyaga tuu.
   
 13. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #13
  Aug 3, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  mkuu, naona wewe hujaelewa hata somo. Hizo pesa uwezekano wa kuzipata ni 5% out of 100%. Hii inathibitishwa na hapo on red/underline kwamba pesa zilishaharibika.
  Wahenga walisema: ....maziwa yakimwagika hayazoleki! Kaa utulie mpaka hiyo miaka 55 au unywe sumu. Poleni sana

   
 14. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #14
  Aug 3, 2012
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mapinduzi siku zote huletwa na vitu vidogo kama hivi vinapopuuziwa - hii inaweza kuwa fursa kwani nikiwasikia waathirika wa hili naona hata kama ni ule alioita Mtikila 'ukondoo' utaisha - wanacheza na maisha ya watu
   
 15. tonnyalmeida

  tonnyalmeida JF-Expert Member

  #15
  Aug 3, 2012
  Joined: Feb 1, 2012
  Messages: 226
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unaweza ukaweka Hoja za kama utani au kebehi hivi lakini uzito wake tunaujaua sisi wafanyakazi.. THERE IS NO FREE LUNCH katika dunia ya sasa . wetha zinalipika au hapana nadhani hilo haliwahusu wafanyakazi.. wao watafute wanapojua ila mwisho wa siku watatuelewa..

  TANZANIA YA LEO SIO YA JUZI.
   
 16. tonnyalmeida

  tonnyalmeida JF-Expert Member

  #16
  Aug 3, 2012
  Joined: Feb 1, 2012
  Messages: 226
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Halafu kuna maagent wao humu wakisikia TUCTA inaandaa maandamano kupinga hii sheria utawasikia wanaleta propaganda ETI KUNA WATU WANATAKA NCHI ISITAWALIKE...... hivi kunamtu aliilazimisha serikali kukopa bila mipango? wala ushauri wa kiuchumi, Nimekuwa nikisikia Mwigulu ndo anajigamba kuwa mshauri wa Rais wa masuala ya Kiuchumi na Kujigamba ana 1st Class ya Degree ya Uchumi.. ndo haya matokeo?? kunamtu alimlazimisha rais na timu yake kutokulipa madeni ya hiyo mifuko?

  Ni nani aliyempa ushauri wa kusain sheria ya kipuuzi kama hiyo halafu yanapotokea madhara ya uamzi wao utasikia kuna watu wanaihujumu serikali... YANI KUNA VIONGOZI KATIKA TAIFA HILI NI MAPOMPOMPO HAKUNA MFANO.
   
 17. M

  Memory Senior Member

  #17
  Aug 3, 2012
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 108
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Hiyo barua imeandikwa kuwagawa wafanyakazi. Lakini pia haina nakala iliyoenda NSSF wala PPF. Ukweli ni kwamba SSRA hawako juu ya sheria na kama rais kweli alisaini basi hakuna mkurugenzi wa SSRA mwenye mamlaka ya kuwalazimisha NSSF au PPF kuwalipa wafanyakazi mafao kinyume na sheria bali mamlaka ya SSRA ni kusimamia mifuko ya hifadhi za jamii kwa mujibu wa sheria! Hapa kinachofanyika ni sawa na kuzima moto wa petrol kwa maji..ukiripuka unasambaratisha kila kitu. Kama kweli huyo Irene anamaanisha basi awambie NSSF na PPF watoe walaka katika mistari yake. TUTAJUTA TUSIPOSHIKAMANA KUDAI HAKI YETU. Japo mimi nilisema nisipopewa pesa yangu ni bora kufa na mmoja wao kuliko kuishi kwa tabu hadi nifike miaka 55 na kuchukua cheaque yenye thamani ya shilingi moja wakati nimeweka 10mil.

  Lakini aibu kubwa ni kwamba hiyo barua imesambazwa karibu migodi yote na baadhi ya viwanda kwa maneno yale yale. Uongo wa mchana kweupe ili kuwafool wafanyakazi na bunge letu TUK.. TUKU.. TUK.. TUKUF. TUKUFUUU..
   
 18. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #18
  Aug 3, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 305
  Trophy Points: 160
  Naibu waziri wa nishati na madini alisema atajitahidi sheria hii isiwahusu wafanyakazi wa sekta ya madini kulingana na mazingira ya kazi zao hasa ukizingatia 'regulations' bado hazijaandaliwa.

  Swali nililobaki nalo, hivi sheria inaweza kuanza kutumika kabla ya regulations kuwa tayari? na bila kuwa gazetted?

  Hebu wanasheria mtusaidie hapa, naona kuna technical loop hole ya kuvuta mafao yangu.
   
 19. M

  Mwanaharakatihuru JF-Expert Member

  #19
  Aug 3, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Du hawa jamaa wa ssra ni masaburi kweli walifikiria kila mtua ana ajira za until death do us apart?
   
 20. papason

  papason JF-Expert Member

  #20
  Aug 4, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Sekta zingine tukilala kwenye hii issue tutalaliwa, tuamke tuchangamke kama walivyo changamka wafanyakazi wa migodin
   
Loading...