Rais Samia: Wameanza kuandika kwenye vigazeti kwamba sitasimama 2025, nani kawaambia?

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,444
7,808
Rais Samia Suluhu Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani Mkoani Dar amesema wanawake bado hawajamuweka Rais mwanamke bali aliyekuwepo amepatikana kwa kudra ya Mungu na matakwa ya katiba. Amesema walichofanikiwa wanawake ni kusukuma mpaka kumpata makamu wa Rais mwanamke.

"Kufika hapa, kama isingekuwa kudra ya Mungu ingekuwa ngumu sana, sasa ndugu zangu Rais mwanamke tutamuweka 2025. Mwaka 2025 tukifanya vitu vyetu vizuri, tukishikamana, tukimuweka Rais wetu, tutakutana hapa kwa furaha kubwa sana

Wameanza kutuchokoza kuandika kwenye vigazeti kwamba Samia hatasimama, nani kawaambia? Wanawake oyee. Fadhila za mwenyezi Mungu zikija mikononi mwako usiziachie.

Wanawake wamefanya kazi kubwa kuleta uhuru wa nchi hii, Wanawake tumefanya kazi kubwa kujenga siasa za nchi hii, tumebeba sana wanaume katika siasa za nchi hii, leo Mungu ametupa baraka mikononi, tukiiachia Mungu atatulaani.


Alisema Rais Samia Suluhu

Samia 2025.jpg

Mengineyo, Rais Samia amesema ataendeleza mema yote katika awamu zote na watajitahidi kuongeza mema mengine.

Kuhusu usawa wa jinsia amesema hawajafika lakini wanawake wataendelea kuongezeka kwani asipofanya yeye hakuna ambae atafanya.
 
Hayo ameyasema leo akizungumza na wanawake

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amesema hayo akishiriki katika maadhimisho ya siku ya Demokrasia duniani DIAMOND JUBILEE Dodoma kwa kusema wanawake hao wanapaswa kusimika Rais kwa kumchagua na yeye amesema mwaka 2025 ndio mwaka ambao Rais wa kike atachaguliwa.

Amesema hayo baada ya kurejea kwamba Rais mwanamke aliyepo kwa sasa ni kwa kudura za mwenyezi Mungu na matakwa ya katiba.
Hivyo mwaka 2025 wanawake wajitafakari na kuweka/kusimika Rais wa kike.
 
Hayo ameyasema leo akizungumza na wanawake

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amesema hayo akishiriki katika maadhimisho ya siku ya Demokrasia duniani DIAMOND JUBILEE Dodoma kwa ...
Hawa watu ndio maana wanakufaga kibudu. Unahudhuria maadhimisho ya demokrasia gani unayo practice kama sio unafki mkubwa!

Huyo hata ma ccm wenzake wahawezi kukubali arudi madarakani.
 
Back
Top Bottom