Elections 2010 SS auponda utaratibu wa NEC kutoa matokeo

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
301
Akihojiwa na ITV baada ya kutangazwa mshindi wa ubunge kwenye jimbo la Sikonge aliyekuwa Spika wa bunge SS ameuponda utaratibu wa NEC wa kuchelewesha matokeo kwa kisingizio cha teknolojia mpya, amesema si wengi wanaweza kuutumia hasa maeneo ya vijijini.

Amesema kuchelesha matokeo ni kuongeza usumbufu usio na ulazima na kuongeza tension za bure kwa wananchi hasa kwa wagombea wenyewe. Amesema endapo atafanikiwa kukitetea kiti chake cha uspika ambacho amesema atachukua fomu muda ukifika atajaribu kulivalia njuga suala hili la urasmu.
 
Kinachofanyika katika ucheleweshwaji huu ni kuchakachua matokeo.
 
SS itabidi awe makini sana na bunge lijalo km ataukwaa tena uspika. Maana kuna vipindi alikuwa naye akivaa KOTI LA SERIKALI na kuwauma wabunge. Mchakato wa kumchagua spika nadhani ungeboreshwa na ikiwezekana atokee spika ambaye si mbunge. Mbunge akiwa spika anapoteza nafasi yake ktk kutetea hoja na kutetea maslahi ya jimbo lake.
 
Sheria iko wazi, Spika siyo lazima awe Mbunge. Labda sema kwamba wanatakiwa kubadilisha kwamba ikitokea Spika aliyechaguliwa ni Mbunge, basi kiti chake cha Ubunge inabidi kitangazwe kwamba kiko wazi ili achaguliwe mtu mwingine kujaza nafasi hiyo kama jirani zetu wa Kenya.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom