squid game series inaonyesha maisha ya asili ya tamaa ya pesa

Hii series mbona haina shida yoyote ni nzuri mno na humo ndani wameweka kama wanaongea kingereza kwaiyo inaeleweka, nimetokea kuikubali sana hapa nilipo nipo ep ya 5 ndo nimekwama,
 
Ni Wasouth Korea Mkuu siyo Wajapan lakini mimi nimeamua kuwapotezea. Iko Netflix.

hii series ukimaliza yote na japo inaendelea
View attachment 1973426

toka s1-9.

kiukweli wajapani wanasoma ulimwengu ulivo kuliko sisi tunavo jisoma.

ukisikia mtu kuwa jambazi,mkatili,mfanyabiashara,tamaa,kuchoka kutafuta,kukubali liwe na liwe,kujilipua,kujitoa muhanga na n.k

hivi vyote vina sababishwa na watu kukata tamaa au maangaiko ya mda mrefu bila mafanikio.

hii series kiukweli inaonyesha vitu vingi kuanzia uchu wa kufika malengo,tamaa,udanganyifu,utapeli,kujichoka,kujitoa na n.k


tunaweza kujadili
 
Aise hautajutia.Binafsi nilikutana na status za watu zimejaa Trailer ,nikaipuuza coz mbali na kua si mpenzi wa Korea movie lakini pia ni mvivu wa kusoma Subtitle kumbuka Movie ni Lugha ya Kikorea basi nikasema wala sitaingalia.Badae mdau mmoja wa movie kali akaniambia Itizame siwezi kukushawish uangalie movie mbove nakujua ,aise Eps ya kwanza tu nikaanza kucheka ,nilitizama yotee non stop kwa usiku mmoja,ni nzuri sana na inaakisi maisha halisi ya utafutaji na namna tunavyopaswa kuthamini maisha na utu kuliko pesa.
Squid game ni imeingia kwenye kati ya Series zangu kali nnazozipenda hadi sasa

1.Breaking Bad
2.Prison Break
3.Squid Game
4.Money Heist
5.ZeroZeroZero
6.Homeland
7.Terrant
8.Queen of South
9.The haves and have not
10.The Oval
Hapo kwenye QUEEN OF SOUTH sasa
 
Kuna mdau humu ana channel yake telegram binafsi nili download kule..mzigo wote uko kule..na movie latest sasa inshu ya link nadhani mnajua sheria za JF.
 
Back
Top Bottom