Squid Game imesukwa haswa

Daah yani watu wanaifananisha money heist na series wale walamba kashata za sukari pamoja na kucheza goroli???


Squid Game imepewa ujiko usioendana nayo aseee
SQUAD GAMES pia hata sie tumeicheza sana utotoni,mambo haya watoto wa Jakaya hawayajui.
Sina mpango wa kuendelea kutazama kabisa.
 
Season 2_game limekua modified yaan kama hufanyi kazi unapelekwa katik dunia ingine huko nikazaazaa hatar
 
Mimi hata huwa siwaelewi na hilo likitu lenu, naona linatajwa sana siku hizi...
Basi walioangalia hiyo kitu wanajikuta na kujiona wao ndo wana akili saana kuliko sisi
 
Niliposoma comment za humu na baada ya kuiangalia ni vitu viwili tofauti.

Naanza kuuamini ule msemo wa “Usiombe mbongo asifie kitu”
 
Mimi silinganishi na series nyingine mana hii na maudhui yake tofauti..kimsingi jamaa walijipanga sana na nimeilewea sana..nasubiri season 2 kwa hamu.

Pia mwakani inakuja house of the dragons...ni full shangwe.

#MaendeleoHayanaChama
 
Nilisikitika kale kadada kufa vile alikuwa amemuahidi maisha mazuri mdogo wake,

Lakini nimeipenda character ya yule Mama mkorofi anayekataa kuitwa Mama anataka aitwe mtoto kwa kweli anastahili tuzo ameitendea haki sana ile character na alinifurahisha alivyodondoka na yule jamaa katili wakafa wote,

Main character historia yake ilikua inasisimua lakini nimesikitika Mama yake hakuweza kuona matunda ya mwanae na vile alivyoona pesa si kitu kama hana furaha akagoma kuchukua pesa alizoshinda,

Wakorea hua wana story nzuri sana nawapenda kwa hilo, natumaini Season 2 itakua bora zaidi.


PS: Mtu kuifananisha Squid Game na Money Heist ni uzuzu wa hali ya juu sababu ni story mbili tofautiii,

SG ifananishwe na SAW na kweli story zimefanana lakini SG naipa kongole zaidi sababu watu walienda kwenye Game wenyewe hawakulazimishwa.
Ata Mimi huyu mama nlimkubali Sana ameitendea haki ile nafasi

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Watu wengi wanajiuliza hii series imependewa nini wakati inastory ya kawaida sana ,hii series watu wengi wameipenda sababu inaelezea maisha ya uhalisia wa maisha ya mtaani mfano humo ndani kuna issue ya vijana kukosa kazi, betting tunaona episode ya kwanza mshikaji kaingia kwenye kibanda cha kubeti dunia ya saa asilimia kubwa ya vijana tunabeti, sasa mtu ukimtajia kuna series fulani ni kali yeye anaibeba na kwenda kuilinganisha na series yake pendwa
 
Uangaliaji wako wa series nakupa 0.01/10.. Kama ndio hivyo... Tafuta series hiyo SG utajikuta ulipoteza muda....ila ni nzuri...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom