Kasomi
JF-Expert Member
- Sep 3, 2014
- 11,036
- 20,337
Mpangilio wa nyimbo katika Album ya msanii ni ubunifu ambao unapaswa kuonekana. Wasanii wengi wanapangilia nyimbo katika Album zao kwa mpangilio maalum; na wanapendelea kuona wasikilizaji wakisikiliza Album katika mpangilio ambao msanii alikusudia.
Adele ametoa Album yake ya “30” ambayo imeshika nafasi ya kwanza kwenye Chat baada ya kutoka. Adele ni moja kati ya wasanii ambao wamekuwa wakipinga Streaming Platforms zinavyolazimisha kuweka button ya “Shuffle” ambayo inapiga nyimbo kuendana na Algorithm inavyopanga na sio kama nyimbo zinavyojipanga katika Album.
Spotify imekubali maombi ya Adele na imetoa alama ya “Shuffle” katika button ya “Play”. Sasa hivi ukibonyesha button ya “Play” katika album yoyote utaweza kusikiliza nyimbo kama zilivyojipanga katika Album. Kama utahitaji Shufle Play itakwepo katika sehemu ya Now Playing na sio katika Album.
Hakuna jambo linatokea kwa bahati mbaya, pia inawezekana ilikuwa ni plan ya Spotify kuondoa Shuffle katika Albums, so imeamua kwenda na kiki ya Adele ili kuonekana inajali na kusikiliza wasanii.