Sports HQ ni kipindi cha matangazo tuu

PintoG

JF-Expert Member
Jun 12, 2017
612
731
Kwa wapenzi wa michezo naamini huwa wanaskiliza vipindi vya michezo redio tofauti tofauti hapa inchini.
Binafsi nilipenda sana kusikiliza kipindi hicho cha EFM sports HQ,wakati yupo kitenge, kwa sasahivi kioindi kinaboa sanaaaa na nimesikia watu wengi wanalalama kuhusu matangazo ya biashara.

Ni kweli matangazo ndo yanadrive kipindi maana ni.pesa hiyo.lakini usipobalance kipindi kinaweza kuanza kupoteza wasikilizaji ambao ndo target ya matangazo. kipindi chao kuanzia ile saa tatu hadi saa nne, mazungumzo ni kidogo lakini matangazo dahh hadi yanaboa, na nina imani watu wengi wamehamia wasafi sports arena ambako matangazo ni kidogo sana.

Wachambuzi pia pale kuna wachache wenye kumfanya msikilizaji afurahie kuwasikiliza kama Jeff na Osca ,ila wasipojirekibisha kweny matangazo watazidi kukimbiwa na wasikilizaji.

Kwa wasafi kama wataweza kusajili Jeff ktk timu yao au wakithubutu kumng'oa mwl KASHASHA toka TBS watakuwa wameua kabisaaaa .

Kwako ni kipindi gani cha michezo bora kabisa,ni mchambuzi gani bora kabisa wa michezo hapa inchini??
 
Samahani huu 'Uzi' wako umekaa 'Kipopoma' sana kwani haueleweki unataka 'tujadili' nini hapa kwakuwa umechanganya Sukari na Mchele katika Ungo mmoja. Ni Wewe huyu huyu umehoji kuhusu 'Matangazo' kuwa mengi halafu hapo hapo 'umejichanganya' kwa kusema sijui Jeff Lea anatakiwa aende 'Kuchambua' Wasafi FM. Kifupi tu unaonekana una 'Chuki' zako na EFM halafu Wewe ni 'Mshabiki' mno wa Wasafi FM.

Acha 'Kutupotezea' muda wetu hapa tafadhali.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom