Sportpesa: Mkenya ashinda dola Milioni 2 shindano la bahati nasibu

mwathadan

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
3,054
4,101
cb073aed13ba7682bef7e9cd1d7cf4bf.jpg

Mkenya aliyefanikiwa kubashiri kwa ufasaha matokeo ya mechi 17 mwishoni mwa wiki amejishindia jumla ya Sh221m za Kenya, ambazo ni sawa na dola 2.2m za Marekani.

Kijana huyo wa umri wa miaka 28 ambaye ni mzaliwa wa Kakamega, magharibi mwa Kenya ndiye wa kwanza kujishindia kiasi kikubwa hivyo cha pesa.

Mshindi huyo wa Mega Jackpot ya kampuni ya Sportpesa alianza kushiriki mashindano ya bahati nasibu ya kubashiri matokeo mwaka jana baada ya kutambulishwa kwa mchezo huo na nduguye.

Taarifa zinasema yeye ni mzaliwa wa pili kutoka mwisho katika familia yenye watoto 12.

Amekuwa akiishi katika mtaa wa Eastlands, Nairobi kwa jamaa yake lakini kwa sasa amepelekwa eneo salama kutokana na wasiwasi kwamba huenda watu wakafika kwa wingi kumpongeza au pengine kutaka kufahamu siri yake.

Kijana huyo alikuwa tayari ameanza kusherehekea alipogundua kwamba alikuwa amebashiri vilivyo matokeo ya mechi 14 kati ya 17 zilizokuwa kwenye Mega Jackpot pale alipopigiwa simu na afisa mkuu mtendaji wa Sportpesa Ronald Karauri muda mfupi baada ya saa sita usiku.

SportPesa, kupitia taarifa, wamesema mshindi huyo alikuwa ameweka dau mara mbili kwa Sh200, kila dau ikiwa ya Sh100.

Alifahamu kwamba mema yalimsubiri baada ya mechi ya Ligi Kuu ya Ufaransa Ligue 1 kati ya Dijon FCO na Bordeaux kumalizika sare 0-0 kama alivyokuwa ametabiri.

Hakuweza kujituliza kutazama mechi mbili zilizokuwa zimesalia kati ya Tottenham Hotspur na Arsenal na mchezo wa Serie A kati ya Inter Milan na Napoli.

"Alienda kwenye klabu viungani mwa mji wa Nairobi ambayo yeye na mwenzake hucheza SportPesa na walikuwa wanajadiliana watafanyia nini mamilioni ya pesa ambayo wangepata pale simu kutoka kwa namba ya simu ambayo hawakuwa wameihifadhi ilipopigwa," taarifa ya SpostPesa inaeleza.

Maafisa wa Sportpesa wamesema watamtambulisha rasmi Jumanne.
 
kwa hivyo watu wa United Kingdom ni vichaa kwa sababu nadani wanaongoza kwa michezo ya bahati nasibu..wacha ujinga wewe...hongera to this man $2M sio pesa za mchezo mchezo
Akili yake mbovu hawezi jiongeza akajua hyo ni lucky
 
kwa hivyo watu wa United Kingdom ni vichaa kwa sababu nadani wanaongoza kwa michezo ya bahati nasibu..wacha ujinga wewe...hongera to this man $2M sio pesa za mchezo mchezo
Hata kama ni watu wa mbinguni kama wanacheza huo ujinga wenu ni vichaa tu, ujinga wa kiwango cha lami ni kuamini kila anachofanya mzungu hicho kitu chema
 
If ur a farmer and Plant hoping for the rain and not to irrigate ur farm, how different are you from a person who places a bet?? Inartia ? Miafrika mnakuwanga na majifanyo hayana mwelekeo ....unamwita mjinga alafu sasa utaenda ulime shamba upande vyakula in hopes of Rain ...what happens if the rains fail? What happens if a team loses???
 
Hii ni dalili ya SportPesa kufilisika na kujaribu kujiinua kwa kumwaga pesa ili watu wengi wazidi ku-''bet'', ni vigumu sana kampuni za ''betting'' kuwa na uwezo wa kutoa kiasi kikubwa cha fedha namna hiyo bila kutumia njia zingine haramu.

Kwa mahesabu kampuni hii haitaweza kudumu zaidi ya mwaka toka sasa maana mfano SportPesa inatoa udhamini wa Ksh. 350 million kwa klabu ya Gor kwa miaka mitatu na inaweza kumlipa mshindi wa mmoja binafsi wa 'bet'' Kshs. 221 milioni http://www.nation.co.ke/news/Kenyan...o-earn-money-/1056-3323738-yinu1qz/index.html . Lazima vikosi vya kuzuia uhalifu usio na mipaka (duniani) na watoza ushuru (tax) kote ulimwenguni watakuja mbio kukagua vitabu vya kampuni hii.

More info:
The firms’ growing financial muscle is further made possible by the fact that although sports betting is a big money business, the money that the firms generate is not taxed because of a lacuna in the existing law.

“This money is not taxed because of a funny taxation model we have. There has been a disagreement whether to tax the winnings or the operators. The operators favour taxing the winnings,” a former betting board member told the Sunday Nation. http://www.nation.co.ke/news/Kenyan...o-earn-money-/1056-3323738-yinu1qz/index.html
Shadrack Kitur is new Sportpesa jackpot winner

Source: The Star Kenya
Car wash attendant wins Ksh 36m Sport Pesa jackpot

Source: Kenya NTV
 
Akili yake mbovu hawezi jiongeza akajua hyo ni lucky
Nyinyi msifanye kazi tu endeleeni na huo ujinga wenu, halafu mnalaumu serikali, jinga kabisa, mnapenda mteremko! Mwisho wa siku mtageuzwa na wanaume wenzenu
 
Hii ni dalili ya SportPesa kufilisika na kujaribu kujiinua kwa kumwaga pesa ili watu wengi wazidi ku-''bet'', ni vigumu sana kampuni za ''betting'' kuwa na uwezo wa kutoa kiasi kikubwa cha fedha namna hiyo bila kutumia njia zingine haramu.

Kwa mahesabu kampuni hii haitaweza kudumu zaidi ya mwaka toka sasa maana mfano SportPesa inatoa udhamini wa Ksh. 350 million kwa klabu ya Gor kwa miaka mitatu na inaweza kumlipa mshindi wa mmoja binafsi wa 'bet'' Kshs. 221 milioni http://www.nation.co.ke/news/Kenyan...o-earn-money-/1056-3323738-yinu1qz/index.html . Lazima vikosi vya kuzuia uhalifu usio na mipaka (duniani) na watoza ushuru (tax) kote ulimwenguni watakuja mbio kukagua vitabu vya kampuni hii.

More info:
The firms’ growing financial muscle is further made possible by the fact that although sports betting is a big money business, the money that the firms generate is not taxed because of a lacuna in the existing law.

“This money is not taxed because of a funny taxation model we have. There has been a disagreement whether to tax the winnings or the operators. The operators favour taxing the winnings,” a former betting board member told the Sunday Nation. http://www.nation.co.ke/news/Kenyan...o-earn-money-/1056-3323738-yinu1qz/index.html
Shadrack Kitur is new Sportpesa jackpot winner

Source: The Star Kenya
Car wash attendant wins Ksh 36m Sport Pesa jackpot

Source: Kenya NTV

Mjinga sana wewe. SportPesa revenue yake ni over Sh30 billion a year. Ile pesa inalipa kama winnings ni less than Sh5 billion a year.
For a betting firm to calculate the jackpot money, they base it on how much they actually make. Lakini kama unakumbuka juzi tulifahamishwa kwamba Tanzania haina acturial scientist, so hesabu kubwa za risk kama hizi hamuwezi.

In a nut shell, pesa inayolipwa kama winnings ni pesa mliyonayo. You're just taking a portion of your revenue.
Sportpesa is not a public company, but from rumours out there, they make over 100 million Kenya Shillings a day.
 
Mbona umekuwa mkali sana, kamari /betting ni mbaya fanya kazi. Nchini Ufaransa na Bulgaria wanaangali mwenedo wa hii kampuni, maana duniani hakuna kampuni ya betting yenye uwezo wa kumwaga pesa namna hiyo. Muda utatupa ukweli. Pia acturial scientist (aliyesoma Actuarial Mathematics) inakwenda zaidi na mifuko ya wafanyakazi wa pensheni au insurance wakati sports betting ni statistics zaidi.
 
Mbona umekuwa mkali sana, kamari /betting ni mbaya fanya kazi. Nchini Ufaransa na Bulgari wanaangali mwenedo wa hii kampuni, maana duniani hakuna kampuni ya betting yenye uwezo wa kumwaga pesa namna hiyo. Muda utatupa ukweli. Pia acturial scientist (aliyesoma Actuarial Mathematics) inakwenda zaidi na mifuko ya wafanyakazi wa pensheni au insurance wakati sports betting ni statistics zaidi.
Sportpesa ni a very rich company. A company that is able to sponsor a club kwa EPL. The CEO has a Lamborghini. Very few people actually win their bets and thats what makes betting sites very profitable.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom