Sport extra na Maximo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sport extra na Maximo

Discussion in 'Entertainment' started by Mayolela, Nov 7, 2009.

 1. M

  Mayolela JF-Expert Member

  #1
  Nov 7, 2009
  Joined: Sep 21, 2009
  Messages: 383
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nadhani sasa Maximo awezi kubaki kwa kuna kura imeanzishwa kupinga kuwepo kwake na sport extra ya clouds- kuanzia jana saa 3 usiku.
  Piga kura mdau wa mpira wa bongo kwenda no 15551,kwa kuandika neno Maximo - Hafai/hanafaa.
  hima wadau tumtoe kocha huyu mbovu katika karne hii.

  mwanangu.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Nov 7, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180

  Mhhhh....!
  SIDANGANYIKI!....nDO MAANA SIUPENDI MPIRA KABISA...UNA MAJUNGU MENGI SANA...FYUUUUU!
   
 3. Ngomo

  Ngomo Senior Member

  #3
  Nov 7, 2009
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 199
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  maximo anatakiwa kubadilika. hawezi kuimpanga golikipa ambaye hajawahi kucheza mechi hata moja wakati kuna kipa mzuri kama Juma Kaseja. maximo tumemwajili ifike hatua tumlazimishe aunde timu tunavyo taka sisi. naona uwezo wake wa kufundisha umefika kileleni
   
 4. AljuniorTz

  AljuniorTz JF-Expert Member

  #4
  Nov 7, 2009
  Joined: Jan 6, 2009
  Messages: 544
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hilo ndio tatizo la soka ya bongo; hivi ukimuajiri kocha ndio umpangie aunde timu gani??? Basi ni bora hizo fedha anazolipwa tuwape nyinyi wajuaji wa ukocha.
  Yaani kupigwa 5 na Misri ishakuwa nongwa! Stars wangeshinda, mmngesema hakuna kocha kama maximo!!

  Soka la bongo limejaa unafiki mtupu, mnataka kuendesha soka kama vile mnavyoendesha siasa za kibongo, unafiki, majungu, fitna, kuzungukana na matakataka yoote!!!
   
 5. M

  Milindi JF-Expert Member

  #5
  Nov 7, 2009
  Joined: Mar 3, 2009
  Messages: 1,213
  Likes Received: 373
  Trophy Points: 180
  Ndio maana Tanzania maendeleo ya Michezo inakuwa ni ziro,Ni upuuzi wa kufikiria kuwa kila mchezo utashinda.Maximo katutoa mbali na tukiendelea kuwa naye tutafika mbali,Mpira unahitaji maandalizi ya muda mrefu na unahitaji nidhamu ya hali ya juu.Wachezaji wetu wanakuwa na nidhamu mbovu wanapokuwa katika club zao na ndio maana wanapotwa maximo anakuwa kama kaanza mwanzo tena.Inafikia wakati kuwa mchezaji anaonekana taifa stars ndio ansajiliwa na club.Huu ni uvivu wa hali yajuu.kitu muhimu ni kjipanga kimazoezi na nidhamu kuhakikisha tunafika katika fainali mbalimbali.
  Walio karibu na Maximo basi wamwambie abadirike kama kaseja alimzomea kufurahi wakati ivo anafungwa basi asamehewe ili arudishwe na watoto watukutu chuji na mwenzake basi wabadilike ili kulijenga taifa na kuliletea heshima.
  Clouds acheni kuwachochea watanzania kumpigia kura ya kufukuzwa huo ni uzabizabina kitu muhimu waruhusuni watanzania watoe maoni ya kujenga kikosi.

  Maximo hongera kwa kutufikisha tulipo kitu muhimu badirika ili kuimarisha ulinzi kwa kumpanga JkJ
   
 6. AljuniorTz

  AljuniorTz JF-Expert Member

  #6
  Nov 7, 2009
  Joined: Jan 6, 2009
  Messages: 544
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  DISCO na FUTBOL wapi na wapi???? Clouds waendelee kupiga bongo fleva, mipasho, ndombolo at el, Mpira wawaachie wajuzi wa mpira...

  Nwasilisha :mad:
   
 7. A

  AmaniGK JF-Expert Member

  #7
  Nov 7, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,101
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Hamna lolote haka ni kamchezo kakuwaibia watu mia tatu zao kila wakituma message! Acheni huu wizi bana
   
 8. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #8
  Nov 8, 2009
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,276
  Likes Received: 4,260
  Trophy Points: 280
  Afadhali hata mkubwa umegundua ,matatizo yetu hayataisha hata Kaseja akiitwa timu ya Taifa au Maximo akiondoka .Mkwasa amesema hata akija Ferguson still kwa mfumo huu tutaendelea kuwa wasindikizaji
  Hao wanaosema MAXIMO hafai wapendekeze kocha anaefaa maana anamalizia mkataba wake mwakani
   
 9. Manda

  Manda JF-Expert Member

  #9
  Nov 9, 2009
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 2,075
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Ppple the likes of this dude ndio ambao hadi leo wamenifanya NIUCHUKIE mpira wa bongo hadi KESHO......politiks....politiks....politiking....politics...politics...politiks....politics...poooooolitis!!!
   
 10. M

  Mayolela JF-Expert Member

  #10
  Nov 9, 2009
  Joined: Sep 21, 2009
  Messages: 383
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hima piga kura aondoke Maximo.
   
 11. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #11
  Nov 10, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Nilijua tu waswahili lazima wataanza..."angepangwa kaseja pale tusingefungwa"....

  Utafikiri Tanzania nzima hakuna kipa mwingine isipokuwa yeye!!!
   
 12. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #12
  Nov 10, 2009
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Huu mjadala wote kisa eti kaseja hakupangwa basi MAXIMO hafai, wale Egypt kiwango chao ni kma ulaya tu mnakumbuka kwenye conf cup kule sauzi mambo waliyoyafanya? halafu eti mnataka mshinde pale massr na kiwango chetu. Maximo kalibadilisha sana soka la bongo. kati ya watu wanaomchukia maximo ni huyu Kocha mziray,, yeye alishapewa hii timu akaifundisha mafanikio yake ni yapi ?
   
 13. edwinito

  edwinito JF-Expert Member

  #13
  Nov 10, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 211
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mziray anajivunia lile kombe la challenge mwaka 1994, wakati n Mkwasa ambaye alifanya mambo. Fuatilia: kila Mziray alipochaguliwa kufundisha timu ya taifa, lazima aliwaita "MAKOCHA", Mkwasa au Kibadeni kama si Sunday Kayuni!
  Jana (09/11/2009), kupitia kituo cha redio cha Magic FM, Mziray alitukana sana! Alidiriki kuziita kampuni zinazoifadhili Taifa Stars (Serengeti Breweries, NMB, nk.), eti ni "vijikampuni", akadiriki hata kuwaita wachezaji wa T. Stars ni "wachezaji uchwara"; huyu anayejiita msomi anavurumisha mitusi LIVE kwenye redio, halafu bado watangazaji wa hicho kituo (Cyprian Musiba, Clifford Ndimbo na Said Kilumanga), wanashabikia ujinga badala hata ya ku-hariri mahojiano yale ( hawakuelewa, hata wao walitukanwa)! Hivi watanzania tunataka nini hasa? Ni kweli Maximo kumpanga Ali Mustapha akae golini, hilo lilikuwa kosa kubwa (maana hajacheza mechi yoyote tangu msimu huu wa ligi umeanza). Lakini je, tulitegemea tungeweza kuwafunga wamisri walio na Aboutreika, Amri Zakhi, Barakat na wengineo??
  Ni kutokana na chuki zisizo na msingi ndo maana jamaa wanachukia kukosa ulaji kama wakati ule.
  Maoni yangu ni kuwa timu iliyopo itunzwe, kama ni mabadiliko ya wachezaji yawe machache kulingana na mahitaji! Vinginevyo tuendeleze vijana ili miaka michache ijayo tuwe na timu nzuri na imara! Siyo tukishinda; Maximo Hoyeee, tukifungwa Maximo Hovyooo!
  Tusipochafuka tutajifunzaje???????
   
Loading...