Spika wa wanafunzi ahamia CCM amekihama CHADEMA; Asema kwa sasa CHADEMA hakina dira | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Spika wa wanafunzi ahamia CCM amekihama CHADEMA; Asema kwa sasa CHADEMA hakina dira

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, Apr 25, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 25, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145  Na Rachel Mrisho
  ALIYEKUWA Spika wa Bunge la Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Goodlack Mwangomango, amekihama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

  Akizungumza Dar es Salaam jana, alisema sababu za yeye kuhama zimetokana na ukweli kwamba kwa sasa CHADEMA hakina dira.

  “Nimekihama CHADEMA kwa kuwa sasa hivi kimekosa dira na badala yake kimekuwa kikisimamia ajenda za muda mfupi,” alisema Mwangomango.

  Alisema kwa muda aliokitumikia chama hicho amegundua kuwa hakina mwelekeo wa kuwaendeleza vijana zaidi ya kuwateka wananchi kwa ajenda zao za kuongeza idadi ya wafuasi na si vinginevyo.

  “CCM pekee ndicho chenye dira na mwelekeo wa kupambana na ufisadi, ndicho chama kinachoongoza Serikali inayoweza kumshika yeyote atakayekiuka sheria na si chama kingine chochote.

  “Baada ya CCM kuonyesha dhamira ya dhati ya kupambana na ufisadi, nimeamua kujiunga nacho, kwani ufisadi ni kitu kilichokuwa kinaitafuna na kuwafanya wafuasi wake wengi washindwe kujitokeza kifua mbele kukitetea,” alisema Mwangomango.
  Katika hatua nyingine, aliwashauri wafuasi wa CCM, hasa vijana waliopo vyuo vikuu kutoogopa lolote katika kukitetea chama hicho, kwa kuwa kimejipanga kujiimarisha na kujisafisha kama alivyoeleza Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete.

  “Unajua mimi nilikuwa mwana CHADEMA, kwa hiyo natambua kuwa vyuoni kuna wafuasi wengi wa CCM ila hawajitokezi, jambo ambalo linawapa nafasi wapinzani kujiona kana kwamba wao ndiyo wengi wakati hilo si kweli,” alisema Mwangomango.
   
 2. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #2
  Apr 25, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Mfamaji haachi kutapa tapa
  Angekuwa Mbowe au Slaa tungejari lakini sio huyu kikaragosi :rant::rant:
   
 3. Butho Mtenzi

  Butho Mtenzi JF-Expert Member

  #3
  Apr 25, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 326
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Duuu iyo ndo design ya Wasomi wa tz
   
 4. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #4
  Apr 25, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Labda Chadema hakina pesa za Kumpa Dira...

  Ni lini kujisafisha kwa CCM ni Dira?
   
 5. opwa

  opwa Member

  #5
  Apr 25, 2011
  Joined: Jun 10, 2010
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  asante kwa pakacha mwingine kama huyu kuvuja, iwe nafuu kwetu wabebaji wa haya mapambano, hata ndugu zako pale kiwira wamekulaani kwa kupoka kwa hivyo vilaki ulivyopewa mwangomango umejinyea dogo ntakusubiri kiwira tuone utajificha wapi
   
 6. peck

  peck JF-Expert Member

  #6
  Apr 25, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 220
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  njaa inamsumbua
   
 7. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #7
  Apr 25, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Kwa kua hakufukuzwa talaka kampa nani?..nadhani mlango huo huo aliotokea atautumia kurudi,kwani nani ana allergy na maedeleo bwanaaa! CCM ni cancer ya maendeleo na hili liko wazi!
   
 8. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #8
  Apr 25, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  Jamani njaa hizi zitatufikisha mbali, tupo!
   
 9. K

  Kivia JF-Expert Member

  #9
  Apr 25, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 278
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hizo ndo siasa za wa TZ-bara wanafiki wanatia kichefuchefu.,wakishapewa vipesa wana wanahama. Hawa ni wasomi uchwara. Nashindwa kuwaelewa hivi ccm wamejisafisha kwa lipi ? Maana mafisadi bado wapo, hawajajiuzulu ,nashindwa kuwaelewa hawa wasomi wetu.
   
 10. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #10
  Apr 25, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  KIVIA mbona uyo hatazami mbali,kwanza ni bora ameutia doa ujanani uanachama wake ili asije sumbua ukubwani
   
 11. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #11
  Apr 25, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Nani kamwambia aingie siasani? Jmdag.a@¥jmadtjag!¿
   
 12. mwankuga

  mwankuga JF-Expert Member

  #12
  Apr 25, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Waswahili wanasema "ukiwa mnafikiri ukiwa kijana,ukizeeka unakuwa mchawi".Pole rafiki yangu Mwangomango.Mara ya kwanza ulipokuwa unaongea kwenye runinga kuhusu kuhamia CCM,nilishangaa kiana na nikakutumia sms ikisema "hongera rafiki yangu kwa urudi CCM".Najua kinachokupeleka CCM sio dira ila unataka kupunguza makali ya maisha.Kutokana na maisha kuwa mazonge na vijana kutotaka kujihangaisha matokeo yake na kama alivyofanya Mwangomango.CHADEMA haiwezi kuyumba kwa kuondoka kwake.Simdharau,lakini Mwangomango ni nani katika siasa za bongo?Kinachoniuma mimi ni jinsi tunavyodhalilisha taaluma zetu,na kuonenya kuwa madarasa mengi tuliyoyapitia ni kupoteza muda.Nenda Mwangomango,Nenda.
   
 13. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #13
  Apr 25, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 362
  Trophy Points: 180
  hiyo ndo design ya wasomi tulionao! Just think ! Hivi CCM wamebadilika nini mpaka wakakubalika kwako! Nina uhakika kabisa hiyo ni njaa and Im sorry to call you a blind and short sighted hufai kuwa anywhere near kwenye watu wa std kama CHADEMA. Nenda kwa wjinga wenzako huko!
   
 14. Mfatiliaji

  Mfatiliaji Senior Member

  #14
  Apr 25, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Bora kaondoka mapema,angekuwa anavujisha siri kwa ccm,tunapenda wengine wasaliti wenye kuona karibu zaidi kuliko mbeleni wajitoe tubaki wachache wenye spirit na uchungu na TZ
   
 15. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #15
  Apr 25, 2011
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,985
  Likes Received: 20,380
  Trophy Points: 280
  Unafuata dira ccm!! usomi wa kipuuzi wa kutofanya rejea, kolimba hakuiona dira huko ulikoenda, hata hivyo umetumia haki yako ya kuamua bila kubugudhiwa hata kama ni tumbo ndo limekuongoza katika maamuzi badala ya kichwa.
  Najua ccm wana dira inayozungunka bila kujua inaelekea wapi:A S shade:
   
 16. Nicas Mtei

  Nicas Mtei JF-Expert Member

  #16
  Apr 25, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 11,569
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Afadhal umejitoa mapema kama mwenzako kishitambala... Afadhal ya adui kuliko mnafiki. So me nashukuru umekuwa adui wa cdm kuliko ungeendlea kubak halafu uwe mnafiki..... Go to hell you f**k .
   
 17. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #17
  Apr 25, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Hivi nyie mngejua ni kiasi gani cha pesa kinatumika kuwavuta hawa vijana wala msingesema

  Hongera spika kwa kukubali pesa......... chonde usije kesho ukasema na ccm hawana dira, utautema mzigo wote uliopokea
   
 18. LWAKAPISI

  LWAKAPISI Member

  #18
  Apr 25, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ukweli ndo huo ccm kwasasa kina tumia pesa nyingi kuwarubuni wasomi wapumbavu kama huyo eti wajifanye wamehama cdm,hata tar16.04 walikuwa na kikao pale ofisi kuu dodoma waliyopanga ndo hayo eti wajiandikishe wanavyuo wote wa ccm baada ya masomo watawapa kazi,na sanasana wanawatumia viongozi kama maraisi,maspika n.k wa vyuo.Ila msomi ambaye bado ana mawazo mgando ya kiccm huyo ni zuzu tena ni wa kuponda kwa mawe hadi afe:-*
   
 19. Nanyaro Ephata

  Nanyaro Ephata Verified User

  #19
  Apr 25, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 979
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  Wewe ndio umepoteza dira,wakati wewe ukitoka kuna mamilioni wanaingia
   
 20. katabu

  katabu JF-Expert Member

  #20
  Apr 25, 2011
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 307
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hiv kumbe hata chuo kikuu kuna mbumbumbu!!!!! Huku kwetu bush tunajua wafuac wa ccm ni wale wasiojua hali ya hii nch ikoje kwa japo kidogo, wazee wazee ama wale wanao nufaika na uchakachuaji, mf. Wazabuni na wengine kama watoto wa makada wa ccm. Ama jamaa kaogopa jalamba mambo yake yasiharibike. C unajua kama ww ni mpinzani, afu mfanyabiash TRA wajue, kila cku uko nao. Au huenda katishiwa uhai kuondolewa maana hawa jamaa balaa!! Msiombe yakawafika ga! Hah!! We acha tu. Yatakamoyo cyo nguvu ya soda ka' jamaa.
   
Loading...