Spika wa Bunge Nigeria atiwa nguvuni kwa ufisadi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Spika wa Bunge Nigeria atiwa nguvuni kwa ufisadi.

Discussion in 'International Forum' started by Indume Yene, Jun 6, 2011.

 1. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Spika wa bunge la wawakilishi linalomaliza muda wake Dimeji Bankole alizuiliwa kuhusiana na madai ya ubadhilifu wa mamilioni ya dola,fedha za serikali.
  Alikamatwa baada ya makao yake katika mji mkuu Abuja kuzingirwa.

  Atakamatwa
  Alipoapishwa kuchukua madaraka wiki iliyopita, Rais Goodluck Jonathan aliahidi kukabiliana ufisadi uliokita mizizi nchini Nigeria.
  Mwandishi wa BBC Jonah Fisher anasema kukamatwa kwa Bw Bankole si suala ambalo halikutarajiwa, baada ya wiki kadhaa za tetesi zilizochapishwa katika magazeti ya nchi hiyo kwamba atakamatwa.
  Msemaji wa tume ya kukabiliana na uhalifu wa kiuchumi na kifedha nchini humo(EFCC),alisema kuwa tume hiyo ilipokea taarifa kwamba Bw Bankole alikuwa akipanga kutoroka nchini.

  Shutma
  Sawa na wabunge wengine, muhula wa Bw Bankole unamalizika Ijumaa- na bunge jipya linatarajiwa kuapishwa Jumatatu.
  Alipoteza kiti chake katika uchaguzi wa mwezi Aprili.
  taarifa ya EFCC inasema Bw Bankole anatafutwa kujibu shutma zinazomkabili.
  Miongoni mwa shutma hizo ni pamoja na matumizi mabaya ya dola milioni 60, na kuchukua dola milioni 65 kama mkopo binafsi akitumia akaunti ya bunge kama dhamana.
  Awali msemaji wa Bankole Idowu Bakare, alitoa taarifa akisema kuwa "hakuwahi kunufaika" kwa kutumia nafasi yake.

  [​IMG]

  Source: Associated Press.

  My Take: JK bado anarembusha meno yake kuonyesha ulimbwende wake wa kutabasamu wakati FISADIZ wanaendelea kutanua mitaani huku wananchi wakitaabika. Tunajua dental formula yake is cutie lakini atambue kuwa watanzania wanahitaji JK kuwajibika na si kucheka au negotiate na Fisadiz.
   
 2. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Nchi zinatuacha taratibu ivyo! Sisi tunabaki longolongo na watu wajinga wanaodhani ccm itabadilika!hahahaha
   
 3. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #3
  Jun 6, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,127
  Trophy Points: 280
  Huku kwetu haya mambo hayawezekani, sisi tupo dunia nyingine tofauti na wenzetu.
   
 4. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #4
  Jun 7, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Huku ukiwa fisadi ni nembo ya kuwa juu na tiketi ya kugombea vyeo vya kisiasa
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  Jun 7, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,267
  Likes Received: 19,407
  Trophy Points: 280
  Ili nchi iendelee lazima kuwe na haki usawa na uwazi, sasa nani hajui kuwa jk aliiba kura?ndio aliiba na kama mnabisha waambieni kina mods wanipige ban
  jk kaiba kura
   
Loading...