Spika wa Bunge la Zambia amewatimua bungeni, wapinzani wote wa Chama cha UPND kwa muda wa siku 30.

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
upload_2017-6-14_10-38-3.png


Spika wa Bunge la Zambia amewatimua bungeni, wapinzani wote wa Chama cha UPND kwa muda wa siku 30.

Hivyo bunge hilo litakosa uwakilishi wa chama hicho cha UPND (United Party for National Development) ambacho ndicho Kikuu cha Upinzani nchini humo.

Spika wa Bunge hilo, Patrick Matibini amesema, ameamua kuchukua hatua hiyo kwa kuwa wapinzani hawamtii, Rais Edgar Lungu.

Mwezi Machi, mwaka huu, wapinzani waligomea hotuba ya Rais Lungu Bungeni.

Spika huyo wa Bunge anasema kwamba kabla hajawatimua wapinzani hao, aliwataka kujiuzulu nyadhifa zao kama hawataki kuitambua Serikali iliyochaguliwa na watu.

Chama cha UPND kimeendelea kuhoji uhalali wa Rais Lungu ambaye alishinda Uchaguzi Mkuu uliofanyika Agosti, 2016.

Kiongozi wa chama hicho, Hakainde Hichilema kwa sasa yumo gerezani, akituhumiwa kutenda kosa la uhaini, mara baada ya kuzuia msafara wa Rais Lungu na hivyo kudaiwa kuhatarisha maisha ya Rais.

Chanzo: Azam news
 
Hahahhaha haoo awakomeshe si walikuwa chama tawala ...fungaaaa tena miaka 100000 ..haoo mafisi maji
 
Back
Top Bottom