Ni muda sasa tangu kuwepo kwa taarifa kuwa Spika wa Bunge letu la Jamhuri, Job Ndugai anaumwa na kwamba amesafirishwa kwenda India kwa matibabu zaidi.
Lakini ajabu - siyo Bunge wala Serikali wanaotueleza anasumbuliwa na ugonjwa gani. Pamoja na kwamba ugonjwa ni siri ya anayeugua, lakini kwa nafasi ya kiongozi wa mhimili; Bunge la Jamhuri, hakuna haja ya kuficha wananchi juu ya kinachomsumbua kiongozi wetu. Tuambiwe tu, hata kama ni "juujuu."
Sisi wananchi ndiyo tunalipia matibabu yake, so siyo vyema hata kidogo kutojua yuko hospitali gani, ili na sisi tunaofanya shughuli zetu hapa India tumtembelee na kumjulia hali.