franklin12xx
Member
- Sep 24, 2014
- 28
- 31
Hii nchi kila kukicha kuna mambo ambayo mtu ukiwaza huwa kichwa kinauma sana. Kila nikitafakati nashindwa kupata jibu sahihi kuwa either huu ujinga ni kwetu tu au pia ujinga huu upo katika mataifa mengine yanayojinasibu kuwa yameendelea au yako katika category ya nchi zinazoendelea.
Sakata la viongozi wanaoumwa na kukaa nje ya nchi kwa miezi na miezi kwa kivuli cha kuuguza ugonjwa walionao huku bado wakishika wadhifa ule ule waliokuwa nao. Hapa ntatolea mfano Spika wa nchi yetu, ni muda sasa yuko nje ya nchi na nafasi yake kukaimiwa na Naibu wake mpaka hapo atakapopona.
Hivi katiba yetu haina kipengelea kuwa kiongozi anaposhindwa kuwa katika nafasi yake na kutekeleza majukumu yake ya kila siku, apigiwe kura of incapacitation na uchaguzi uitishwe ndani ya kipindi flani kuchukua nafasi yake.
Maana tunaona yapata miezi sasa spika huyu tunaambiwa anaumwa huku hatujui anatarajia kupona lini. Kiongozi wa juu wa nafasi hiyo huwa anatokana na kura za wananchi pamoja na wajumbe wanaomkubali katika mhimili wake, sasa anaposhindwa kutimiza wajibu wake inapaswa awe declared incapacitated na uchaguzi wa spika uitishwe upya kwa manufaa ya nchi.
Maana haya ni matumizi mabaya ya fedha za umma, yaani mtu anaendelea kugharimikiwa na serikali huku hatekelezi majukumu yake ya kila siku na anayekaimu anatumika tu kama tv, huku remote iko kwingine.
Au katiba yetu inasemaje? kwa wanaijua vyema watujuze.