Spika wa Bunge la DRC Congo kutoka chama cha Kabila aondolewa madarakani

Uzalendo Wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
671
1,000
Spika wa Bunge la DRC Jeanine Mabunda ameondolewa katika nafasi yake baada ya wabunge kupiga kura ya maoni dhidi yake iliyowasilishwa bungeni na Upinzani.

Miongini mwa wabunge 484 katika Bunge hilo kura 281 zilisema kwamba kiongozi huyo wa muhimili huyo aondoke katika nafasi yake.

Zaidi ya wanabunge mia mbili kati ya wabunge mia tano waalifanya kikoa cha kupiga kura ya kumuondoa madarakani Spika wa bunge Jeanine Mabunda kutoka chama cha Joseph kabila.

Mwandishi wa BBC, nchini DRC anasema ; Upande wa chama cha Kabila tayari kulikuwa na mzozo katika vyama vilivyokuwa vinamuunga mkono, hivyo hiyo inaweza kuwa sababu ya kuanguka kwao.

Na hatua inayofuata ni waziri mkuu kujiuzulu sasa kwasababu rais atamchagua mtu atakayeunganisha vyama bungeni hivyo nia ya rais kuvunja muungano huo.

Lakini kinachoshangaza inakuwaje spika huyo ashindwe kupata kura za kutosha kumtetea kupata kura za kutosha wakati wabunge wa chama chake ni wengi zaidi.

Kwanini hasa kimesababisha chama cha Rais wa zamani chenye idadi kubwa ya wabunge Bungeni kushindwa kumuunga Mkono Spika huyo wa Bunge?

 

Proved

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
11,101
2,000
Tshekedi ameamua kuvunja ushawishi wa Kabila kwenye serikali yake, ni jambo jema maana Kabila alikua kama Rais kivuli.
 

Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
23,522
2,000
Hapo ndio utaona tofauti ya Tanzania na mataifa mengine ya Ki Africa

Taratibu wanaanza kuvuruga amani yao
 

Consultant

JF-Expert Member
Jun 15, 2008
10,127
2,000
Hapo ndio utaona tofauti ya Tanzania na mataifa mengine ya Ki Africa

Taratibu wanaanza kuvuruga amani yao
Utofauti wao na Tanzania ni kwamba wabunge hata wa upande wa chama kinachotawala wakiona mambo yanakwenda ndivyo sivyo hawaoni hatari au woga kupiga kura kinyume na matakwa ya viongozi wao.

Tanzania bado sana. Vyama vyetu vyote ukienda kinyume na msimamo au matakwa ya mwenyekiti, unafukuzwa kundini mapema asubuhi
 

Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
23,522
2,000
Hiyo unayoita 'bado sana' ndio salama yetu na tunamshukuru Mungu kwa hilo
Utofauti wao na Tanzania ni kwamba wabunge hata wa upande wa chama kinachotawala wakiona mambo yanakwenda ndivyo sivyo hawaoni hatari au woga kupiga kura kinyume na matakwa ya viongozi wao.

Tanzania bado sana. Vyama vyetu vyote ukienda kinyume na msimamo au matakwa ya mwenyekiti, unafukuzwa kundini mapema asubuhi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom