Spika wa Bunge, Job Ndugai athibitisha kupokea barua ya kuvuliwa uanachama Wabunge 8 wa CUF

Hakika kabisa. Ila, hivi alifahaamu mwishilizo wa maamuzi yake? Seif ni mwerevu sana na ni mtu aijuaye kesho yake hasa linapokuja suala la mikanganyiko kama hii, mimi najiuliza je ilikuwa ni bahati mbaya au alikusudia?
Hakutumia akili yake au hakuiamini akili yake akachukua ushauri wa chadema huo ndio ukweli japo watu watatukana

the great
 
Maalim alishinda uchaguzi wa tarehe 25
Alafu akaporwa baada ya kuporwa akapewa nani? Maana kama angepewa shen angetangazwa kuwa ndie mshindi ila kwasababu hakujulikana aliyeporwa ndio maana uchaguzi ulirudiwa

the great
 
SAFI SANA PROF LIPUMBA PAMBANA MNYAMWEZI MPAKA MPEMBA AKUJUE WEWE NI NANI HIZI SIO ENZI ZA KULIMA KARAFUU KULE PEMBA TUPO NYUMA YAKO PROF UNAPAMBANA NA CHADEMA NA WASALITI WA CHAMA INSHAALLAAH ANAYETEGEMEA KUWA RAIS WA ZANZIBAR ATAKUJUA WEWE NANI
 
Ila bora ya Dr slaa aliamua kuchagua kukaa kimya , huyu lipumba ajiangalie Sana asije kulewa sifa mwisho wa siku akaja kuumia na kubaki jina jina hizi fitna za kibwege zinaweza kuja kugharimu maisha yake
 
Sio

Hiyo sio issue kesi yaweza endelea wakiwa wamepigwa chini ubunge.Kesi haijatolewa hukumu huwezi zuia shughuli zingine za chama zisiendelee zikiwemo za kuwapiga chini wakorofi ndani ya.chama.Spika usiogope wapige chini
Lipumba alishafukuzwa ndani ya chama
 
Shida ni upinzani kukubali kugawanywa na ccm, yaani wakisikia wimbo wanakomalia kibwagizo wanaitikia wee mpaka wanaamini uongo, bila aibu mnaitana wasaliti, ndumila kuwili, zwazwa, ccm b, wenzenu ccm kazi yao moja _kuwatibulia kisima chenu hadi mhame kijiji ama muwaombe poo
 
CUF ya Maalum Seif ndiyo CUF halali kabisa kisheria lakini imezidiwa maarifa na akili na ile CUF ya bwana yule.

Kuna wakati Bwana Yesu aliwaambia wafuasi wake ambao wakati huo hawakuwa wakiitwa wakristo kuwa Wanaangamizwa kwa kukosa maarifa. Hakusema kuwa wamekosa imani au matendo mema bali wamekosa "Maarifa".

Wakati mwingine Bwana Yesu akawaambia tena kuwa wana wa giza katika ulimwengu wao wamewazidi busara na hekima kuliko wana wa nuru.


Ni hivi :
Niliwahi kusema kipindi cha uchaguzi wa kule Zanzibar kuwa uchaguzi ule ulikua ni halali kwa Wawakilishi wote waliopewa vyeti vya ushindi na hapakuwa na haja ya kufuta matokeo ya wawakilishi.
Sheria ilikua wazi kabisa. Upande wa urais wa Zanzibar ndio ulikua na shida kwani hakuna mshindi aliyekuwa ametangazwa na ZEC hivyo hapakuwa na sababu yoyote kwa wawakilishi waliokuwa wameshinda kihalali na kupewa shahada za ushindi ya kuacha kwenda mahakamani wakati ule au kwenda kwenye baraza la wawakilishi na shahada zao halali ili wakaapishwe.

Mahakama zilikua badao zina uwezo na nafasi ya kutoa hukumu iliyokuwa ya haki kwa wakati ule kutokana na ukweli kuwa hata majaji walikuwa wapo watiifu kwa Makamu wa Rais ambaye alikua ni maalum Seif.

Maalim na kundi lake hawakuweza kuona haki yao iliyokuwa wazi kule Zanzibar kwa upande wa wawakilishi waliokuwa tayari wametangazwa na kupewa vyeti vya ushindi. Wao walibaki kungangania upande wa ushindi wa urais ambao haukuwa na ground yoyote ya kisheria zaidi ya maneno ya kisiasa ya Maalim Seif.
Tume ilikua bado haijatangaza matokeo ya urais hivyo hapo pangeweza kuwa na changamoto ya kisheria kuzuia tume isiyafute.

Suala la Buguruni nalo pia ni kati ya mambo ambayo yalikua yako wazi kabisa kwa CUF ya maalim Seif kisheria lakini hawakutumia vyombo vya sheria badala yake wakaja na matamko ya kisiasa.
Mfano Lipumba alipokuja kuvunja viti na kuvamia mkutano . Ile ilikua ni jinai wala sio siasa hivyo walipaswa wafungue kesi ya kijinai na waisimamie pia kesi ya kudai fidia iliyotokana na Lipumba kuharibu mkutano halali wa chama ambacho yeye alijipambanua kama mwanachama wa kawaida . Pia kundi la Maalim Seif lingeweka zuio la kimahakama la kumzuia Lipumba asifanye siasa ndani ya chama hicho kutokana na kuwa na shauri liliopo mahakamani.
Wakati ule mahakama bado zilikua na nafasi nzuri ya kupokea malalamiko hayo.
Badala yake Maalim Seif alibaki na matamko ya kisiasa tu.
Makosa hayo nayaona pia yanafanywa na Chadema kushindwa kuzitumia mahakama kupeleka malalamiko yao badala yake wanachukua sheria mikononi na kudanganya watu kuwa wanagandamizwa na serikali. Lakini wakizidiwa wanalalamika wapelekwa mahakamani.
Badala ya wao kuwahi na kuwapeleka wale wanao walalamikia mahakamani wao ndio wanawahiwa na kupelekwa mahabusu na baadae mahakamani.

Ninachokiona kwa Maalim Seif ni kuwa anaona aibu kujiuzulu baada ya kushindwa kufikia malengo yake kisiasa kwa kukosa mbinu za kisheria badala yale anataka kuenguliwa na mahakama kupitia kundi la Lipumba ambalo linatumiwa na chama tawala kwa kuwa halina madhara ya kisiasa kwao. Kwa ujanja wa Lipumba yeye anadili na udhaifu wa sheria huku akiungwa mkono na msajili.

Kiukweli mahakama zetu zipo huru kwa kiasi kikubwa pale penye uhalali wa kisheria.
Ni bora wapinzani wakazitumia mahakama zetu kuliko kutumia nguvu ambazo zitawaumiza wao wenyewe.

Kwa hili la wabunge ni vyema mwanasheria wa CUF akaenda mahakamani kupinga kufukuzwa uanachama kwa hao wabunge.
Na ingekuwa vizuri pia wakafungua kesi ya kupinga uenyekiti wa Prof. Lipumba kwa ushahidi wa kimaandishi wa barua yake mwenyewe ya kujiuzulu na kuwa mwanachama wa kawaida.

Lipumba hakuawa na uhalali wowote wa kujirudisha mwenyewe madarakani kutokana na ukweli kuwa maamuzi ya kujiuzulu kwake yalikuwa hayajajibiwa ili ajue kama haki imetendwa na chama chake au la. Kama angeonewa alipaswa akate rufaa na sio kutumia nguvu na uvunjifu wa amani na kujirudisha madarakani.

Vinginevyo ni vyema CUF ya maalim Seif ikajitoa na kuunda chama kingine kama bado wanapenda kujiweka chini ya UKAWA au CUF ya maalim Seif iamue moja kujiunga na Chadema au NCCR Mageuzi na kuweka nguvu zaidi kwenye siasa za upinzani.
Kuungana na Lipumba itakuwa ni kuanzisha siasa za kuua upinzani nchini.
Lipumba sio salama kwa wapinzani na pia kwa amani ya nchi yetu kutokana na siasa zake za vurugu tangu kipindi cha mapanga shaa na ngangari na ngunguri. Lipumba Hafai kwa siasa za amani ya nchi yetu. Ana siasa za ugomvi na vurugu.





Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa maoni yangu, kwakuwa kuna mashauri Mahakamani yanayojikita katika uhalali wa viongozi wa CUF, suala hili linapaswa kusubiri kuisha kwa mashauri husika. Hii ni kwakuwa hata uanachama wa Prof. Lipumba pamoja na Mbunge Sakaya unahojiwa mahakamani.

Yatakapoisha mashauri hayo yaliyo mbele ya Mtukufu Jaji Ndyansobera, viongozi halali watajulikana. Na vitendo na maamuzi halali vitaonekana. Mambo ya CUF yatakwisha tu kisheria siku si nyingi.
Niliposoma habari hiyo na kuona Bunge limepokea nikajiuliza sana

Hivi Bunge linajua mihimili inavyofanya kazi?

Shauri lipo mahakamani, kulizungumzia achilia mbali kulipa uzito wa habari ni mapungufu makubwa sana. Yanaacha tasisi zote, Bunge, msajili wa vyama bila 'mavazi'
 
Prof Lipumba, haya yote unafanya kwa maslahi ya nani? Tambua kuna Mungu na anakuona!
 
Kisheria Lipumba hana mamlaka ya kuwafukuza hao wabunge kwa kuwa ameyafanya hayo wakati shauri la msingi ambalo ni mgogoro kati ya Lipumba na chama chake haujaisha.
Yaani hilo hajalifanya kwa bahati mbaya bali mgogoro alionao na wahusika. Spika ana uwezo wa kutengua barua ya Lipumba kwa hoja hizo.
Lipumba angekuwa sahihi endapo tu angekuwa pamoja nao tangu mwanzo. Wamekuwa wabunge nje ya uwepo wake hawana msaada naye hata chembe. Pili mshikamano wa cuf na chadema kwa sasa ni mkubwa ambapo yeye hawezi tena kuwagawa. Kitendo cha chadema kuwasaidia cuf kuwadhibiti wale wahuni waliotaka kuharibu mkutano wa cuf ni somo tosha.
Huyo Lipumba ni sikio la kufa. Nashauri watinge mahakamani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa maoni yangu, kwakuwa kuna mashauri Mahakamani yanayojikita katika uhalali wa viongozi wa CUF, suala hili linapaswa kusubiri kuisha kwa mashauri husika. Hii ni kwakuwa hata uanachama wa Prof. Lipumba pamoja na Mbunge Sakaya unahojiwa mahakamani.

Yatakapoisha mashauri hayo yaliyo mbele ya Mtukufu Jaji Ndyansobera, viongozi halali watajulikana. Na vitendo na maamuzi halali vitaonekana. Mambo ya CUF yatakwisha tu kisheria siku si nyingi.
Hujui kama Bunge ni mhimili unaojitegemea?
Prof.Ibrahim Haruna L. ndiye mwenyekiti halali anayetambulika na msajili wa vyama vya siasa.
UKAWA ndipo mtakapokubali kwamba mlipokea FISADI aliyelaaniwa na baba wa Taifa,sasa laana inawatafuna!
 
Kwani huu mgogoro ni faida ya nani kwa sababu chama kama chama hakifaidiki kuvunjika kwake Kwa nini msimaluze kwa kukaa ktk meza ya mazungumzo.

Kama Kesi iko mahakani inakuaje huo mihimili mwingine upokee hiyo Barua huku wakijua halijakaa vizuri hapa ni ni kupigana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu mgogoro utamalizwa endapo tu mmoja kati ya Lipumba ama maalim seif kuondoka duniani,,, Matarajio ya Lipumba kwakuwa anaungwa mkono na serikali na ccm maombi yake yatakubalika na kupelekea kuwaondoa hao wabunge na kuweka wabunge wake ili kuwea kurudisha control ya wabunge kwani hana uwezo huo kwa sasa..

matarajio yangu ni kuwa naona siku za usoni pale buguruni ofisi ndogo watu watakatana kisu na mapanga,,, mgogoro wa cuf unaelekea kuondoa baadhi ya maisha watu,,, tujiandae kuona umwajikaji wa damu,,,

Serikali ya ccm itakuwa imehusika. Na ndo maana kwa wazi kabisa tunaiona iko upande wa Lipumba
 
Back
Top Bottom