Spika Tulia, huu si ufisadi kweli Bunge kukodi mabasi ya Shabiby?

Wabunge wa Kamati mbalimbali wako ziarani kukagua miradi.

Kampuni ya Shabiby (inayomilikiwa na Mbunge Shabiby) ikalikodisha Bunge mabasi makubwa 10 kwa ajili ya kuwatembeza Wabunge kwa siku 10.

Ni katika mikoa ya Iringa, Njombe na kadhalika.

Kila siku (bila ya kujali basi husika limetembea au la) kila basi linalipiwa shilingi milioni 3. Kwa siku 10 na kwa mabasi 10, ni jumla ya shilingi milioni 300.

Milioni 300 kwa siku 10 kweli? Mbunge Shabiby alipataje 'tender' hiyo ikiwa ana mgongano wa kimaslahi? Huu si ufisadi kweli?

Katiba mpya si takwa la Rais wala Kikosi Kazi....wananchi wanataka Katiba Mpya!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Bettina kahongwa
 
So zile basi mpyaaah zilikuja special kwa kazi za kibunge!?
300M Kwa siku 10 siyo haba!
Maisha Bora Kwa kila Mtanzania, kazi na BATA iendelee!
 
Wabunge wa Kamati mbalimbali wako ziarani kukagua miradi.

Kampuni ya Shabiby (inayomilikiwa na Mbunge Shabiby) ikalikodisha Bunge mabasi makubwa 10 kwa ajili ya kuwatembeza Wabunge kwa siku 10.

Ni katika mikoa ya Iringa, Njombe na kadhalika.

Kila siku (bila ya kujali basi husika limetembea au la) kila basi linalipiwa shilingi milioni 3. Kwa siku 10 na kwa mabasi 10, ni jumla ya shilingi milioni 300.

Milioni 300 kwa siku 10 kweli? Mbunge Shabiby alipataje 'tender' hiyo ikiwa ana mgongano wa kimaslahi? Huu si ufisadi kweli?

Katiba mpya si takwa la Rais wala Kikosi Kazi....wananchi wanataka Katiba Mpya!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Tulia hapo ana zake 5 milioni
 
Ndg hapa simtetei mfanyabiashara, ila ebu tuliweke upande wako, gari linafanya kazi na ni gari la biashara ambapo kila siku kama ni zima likiwa halina ubovu linaingiza fedha, Swali ni Je!

Ni sawa siku ambayo wabunge hawana ratiba gari lisiingize fedha kisa limekodiwa na wabunge huku likiwa limeondolewa kwenye mfumo wa kuingiza fedha?

Ameuliza pia kama mchakato wa kumpa zabuni ulifuatwa, lakini pia ameuliza kama huo siyo mgongano wa kimaslahi? Yaani Mbunge kupewa zabuni ya kuwatembeza wabunge wenzake kwa kutumia mabasi yake!

Tolea ufafanuzi kwenye hili pia.
 
Dawa ni kuiondoa tu CCM, haya mengine yataji set yenyewe.
Hawa watu wamegawana maeneo ya kula hela zetu, wamekuwa wamoja sanakatika kutafuna hela zetu, usitegemee wtatofautiana katika hill, wanaungana mkono sana kwa sababu ya kula hela namna hii
 
Acha wale tulimpata Magufuli mzalendo na yeye mlilalamika wamekuja wapigaji na wenyewe mnalalamika.

Shida ya watanzania hawajui wanachokitaka.
Wabunge wa Kamati mbalimbali wako ziarani kukagua miradi.

Kampuni ya Shabiby (inayomilikiwa na Mbunge Shabiby) ikalikodisha Bunge mabasi makubwa 10 kwa ajili ya kuwatembeza Wabunge kwa siku 10.

Ni katika mikoa ya Iringa, Njombe na kadhalika.

Kila siku (bila ya kujali basi husika limetembea au la) kila basi linalipiwa shilingi milioni 3. Kwa siku 10 na kwa mabasi 10, ni jumla ya shilingi milioni 300.

Milioni 300 kwa siku 10 kweli? Mbunge Shabiby alipataje 'tender' hiyo ikiwa ana mgongano wa kimaslahi? Huu si ufisadi kweli?

Katiba mpya si takwa la Rais wala Kikosi Kazi....wananchi wanataka Katiba Mpya!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Jamaa unaakili sana
Hahahahaha Hapana sema hutakiwi Kushangaa Sana Maana Wameshakuwekea Mziki Wao wanaocheza sasa Wao wanacheza AMIPIANO wewe unataka Zilipendwa. na Wewe Cheza AMAPIANO utakayempata Kucheza Naye hakikisha Umemshika Kiuno Unakiendesha Kweli kweli
 
Ndg hapa simtetei mfanyabiashara, ila ebu tuliweke upande wako, gari linafanya kazi na ni gari la biashara ambapo kila siku kama ni zima likiwa halina ubovu linaingiza fedha, Swali ni Je!

Ni sawa siku ambayo wabunge hawana ratiba gari lisiingize fedha kisa limekodiwa na wabunge huku likiwa limeondolewa kwenye mfumo wa kuingiza fedha?
Nadhani hiyo ni pesa kidogo sn yangekuwa ya serikali service tu ya gari moja kabla ya safari sijui na vipuri milioni 20 kila moja bado mafuta na dereva na ufisadi, bora serikali iwe inakodi magari isipokuwa gari ya Rais, Makamu wake, PM, Jaji Mkuu na Spika
 
Back
Top Bottom