Spika Tulia endelea kuonesha ukomavu katika kuliendesha bunge

Michael Uledi

Senior Member
Mar 29, 2023
132
322
Tangu kuanza kwa Bunge hili April, 2023 nimekuwa nikifuatilia sana Spika Dkt. Tulia Ackson katika kunyosha hoja na kutoa ufafanuzi wa kimantiki kwa Wabunge na Watanzania!

Hoja ya Over Invoice ya ununuzi wa ndege ya mizigo, Watanzania wengi walijua inatokana na repoti ya juzi ya CAG ya mwaka 2021/22 kumbe sio kweli! Kwahiyo hoja hiyo imekosa nguvu kidogo ndani ya mjadala wa Bunge!

Hoja ya pili ni ya kujichanganya kwa Waziri wa fedha kuhusu nani ndiye mlipaji Mkuu? Je, ni Rais au Katibu Mkuu Hazina? Ni wazi Waziri alitaka kujificha kwenye kichaka cha Rais lakini Mzee Sendeka akamrudisha lakini Spika ndio kampuni zaidi kwa vifungu vya Katiba ya nchi! Mwisho Brother Mwigulu ikabidi atulie!

Inaonekana tuna Spika ambaye yupo fame sana kwenye ishu za msingi!

Hongera Spika kwa kuleta uelewa wa pamoja kuhusu ishu zenye maslahi kwa Taifa la Tanzania!

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom