Spika Tulia Ackson: Mdee na wenzake 18 wako bungeni kihalali, aeleza kuhusu kurejea kwa Bunge LIVE!

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari. leo Februari 14, 2022 ameeleza kuwa Mdee na wenzake 18 wako bungeni kihalali:

“Uharamu haupo kwasababu hawezi kuwa haramu halafu akawepo mule ndani. Nchi yetu inaendeshwa Kidemokrasia na Kisheria. Jambo moja tu linalosubiriwa ni watu kumaliza michakato yao inayohusika.

“Jambo moja linalosubiliwa ni kumaliza michakato yao inayohusika ndani ya chama. Katiba yetu inasema mbunge lazima awe mwanachama, kwa hiyo wakimaliza wakaleta taarifa tutachukua hatua.”

Kuhusu mpango wa kurejesha Bunge live, Tulia amejibu: “Hili ni jambo ambalo linazungumzika, wacha tuone sababu zilizolifanya kuondolewa. Tutazungumza na Waziri wa habari kuona nini cha kufanya.”
 
wale walishafukuza uanachama (kwa mujibu wa katiba hawastaili kuwa bungeni ili hata spika mstaafu Mzee Msekwa alishaliongelea) suala la wao kukata rufaa ni maana yake wanataka warudishwe uanachama wao.

Hivi Sabaya alivyofunga miaka 30 ameamua kukata rufaa kwa hiyo maana yake sio mfungwa.

Jurisprudence inaelekeza kwamba unapokata rufaa ni kwamba hukumu iliyotolewa inaendelea kusimama hadi hapo rufaa yako itakaposikilizwa
 
Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson amesema, Mdee na wenzake 18 wako bungeni kihalali: “jambo moja linalosubiliwa ni kumaliza michakato yao inayohusika ndani ya chama. Katiba yetu inasema mbunge lazima awe mwanachama, kwa hiyo wakimaliza wakaleta taarifa tutachukua hatua....
CHADEMA haiwatambui sijui anataka mchakato wa chama gani?
 
Spika Dkt. Tulia Ackson amesema kuwa Wabunge 19 wa Viti Maalum wa CHADEMA ni halali, kwani wangekuwa haramu wasingekuwepo bungeni. Amesema bunge likipewa taarifa rasmi kuwa wamefukuzwa uanachama, watakoma kuwa wabunge, kwani mbunge sharti awe mwanachama wa chama cha siasa. https://t.co/jPMx7uj9UW
20220214_125707.jpg
 
Back
Top Bottom