Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,480
- 30,152
Kwanza nieleze masikitiko yangu makubwa Sana kwa jinsi nilivyomsikia Spika Tulia Ackson akihamasisha machafuko, wakati akihutubia Umoja wa vijana wa CCM huko jijini Mbeya.
Kwa nchi inayoendeshwa kwa Demokrasia na yenye mfumo wa vyama vingi, ni jambo la kuskitisha Sana kwa matamko aliyoyatoa Spika wa Bunge letu Katika kikao cha UVCCM, kwa kuwataka vijana hao kuwa wasimvumilie mtu yoyote, aidha kutoka CCM au vyama vya upinzani, kuwa washughulike naye, atakayemsema vibaya Rais wetu Samia Suluhu Hassan!
Hayo maneno ni ya hatari Sana Katika nchi inayohubiri kudumisha amani kila siku.
Hivi kutoa "critical criticism" kwa kiongozi wa nchi, au kwa Spika wa Bunge, au hata kwa Mbunge yeyote, lengo likiwa kurekebisha mfumo ambao utauona siyo wa Haki, hivi kuna ubaya gani, Hadi Spika wetu atoe maneno ya vitisho vya kiasi hicho?
Katiba ya nchi yetu, ambayo ni sheria mama, Katika ibara ya 18(1) inatoa uhuru kwa kila mtanzania kutoa maoni yake.
Hivi Spika Tulia Ackson, anajaribu hata kupingana na Katiba ya nchi yetu, iliyotoa uhuru wa wananchi, kutoa maoni yao?
Hivi Spika Tulia Ackson, anajua kuwa kutokana na hayo matamko yake aliyoyatoa kwa huo Umoja wa vijana wa CCM, unaweza kuleta machafuko makubwa ya umwagaji damu nchini?🥺
Kutokana na maelezo hayo ningependa kumwomba Spika Tulia Ackson, ajiuzulu nafasi yake ya u-Spika wa Bunge Ili kuliepusha Taifa hili na machafuko ya umwagikaji damu
Mungu ibariki Tanzania