Elections 2010 Spika Sitta Ukifanyiwa Zengwe CCM fanya haya

1. Weka hadharani ripoti ya Richmond hasa ule upande uliouzuia kuiokoa Serikali.
2. Tujuze Watanzania kuhusu ule unga wa Bungeni.
3. Waeleze wazi kuwa huzitaki siasa za majitaka.
4. Pambana na mafisadi popote pale hasa wanaotaka kuiuza nchi yetu.
5. Weka wazi zile kashfa za meremeta,kagoda na tangold ulizozizuia Bungeni.
6............

Sita hana ubavu wa kufanya hata jambo moja hapo juu.
 
Hivi kwani lazima Spika awe Sitta??no way he has to go ni MNAFIKI sana huyu mzee..i Hate him..ni mara 100 chenge awe spika kuliko sitta..huyu si ndo kajenga ofisi ya spika kwa 500m

Sasa kama ameshajenga ofisi ndogo ya Spika mjini Urambo, mkinyima uspika si itakuwa ile ofisi haina maana yeyote? au itakuwa ya mbunge wa Urambo?
 
Sitta ni Vugu vugu na anastahili kabisa kutapikwa! Kwangu mimi ni heri anngie chenge ili wananchi twende msituni kudai nchi yetu kuliko watu kama wakina sitta ambao wanataka kuendeleza mambo yale yale!
 
Kwanini mzee YUSUPH makamba asigombee hiyo nafasi? kama yupo bize hata mzee kingunge agetufaa sana, wanasifa zilizopitiliza. Ila hata huyo chenge naona hana shida, ni mtu wa watu, anauchungu na taifa hili, hana dharau na ni mahili katika taaluma ya sheria, nafikiri kiti kinamfaa.
 
sitta ni vugu vugu na anastahili kabisa kutapikwa! Kwangu mimi ni heri anngie chenge ili wananchi twende msituni kudai nchi yetu kuliko watu kama wakina sitta ambao wanataka kuendeleza mambo yale yale!

uchaguzi huu uliopita unaendelea kuthibitisha hofu ya wengi kuwa njia ya kura haiwezi kuleta mabadiliko tanzania.
 
Uzuri wa Sitta ni upi?

Naona ana unafiki vile, EPA aliitupilia mbali. Richmond issue imeisha hivi hivi.

Spika si lazima awe Sitta anaweza kuwa mtu mwingine ambaye ni jasiri zaidi ya Samwel Sitta aliyetishwa na chama chake, na akanywea.
Jasiri kati ya hao waliochukua fomu sioni!bora abakie sitta kuliko huyo chenge
 
Jamani msiwape pointi CCM acheni wafanye viroja kwa kuwalinda mafisadi na tutajua kama wana fore sight au hawana. Ili sisi tunona zaidi ya 2010 na wao wanaona tu 2010. Tunajua viongozi wasiokuwa na maono huangamiza taifa. Na hapa dalili tayari zimeshaanza kuonyesha kwani kuna matukio mawili ya hatari yamejitokeza;
La kwanza ni chenge kuchukua fomu na kugombe a uspika na kumponda Samweli 6 hadharani bila woga
La pili ni TAKUKURU kumsafisha Chenge kuwa kashfa ya RADA alihusishwa kimakosa.

Mambo haya yanapokuja pamoja wenye akili tunajua siyo bahati mbaya kwani hiyo ni trella na sinema yenyewe imeshapikwa.
Tusishangae kuona Chenge ndiye atakaye chaguliwa Spika. Lakini nasema itakuwa ni BLOW KUBWA kwa CCM anguko ambalo hawatakaa walisahau
 
Sitta ni Vugu vugu na anastahili kabisa kutapikwa! Kwangu mimi ni heri anngie chenge ili wananchi twende msituni kudai nchi yetu kuliko watu kama wakina sitta ambao wanataka kuendeleza mambo yale yale!

unaona n heri aingie chenge ili mwende msituni, are you serious? Nchi imeporwa imebaki na mashimo tupu, wahindi wanagawana urithi wetu mchana kweupe, still unangoja chenge awe spika ndipo uende mstuni, i could almost call it a nonsense!
 
it is a nonsense .......... Not almost...............
 
By the way who is clean ndani ya CCM, pengine huyo Sitta ana unafuu but all are the same fish
 
Ni nani aliyemsafi katika CCM?

To me either SITTA or Chenge or Makinda or any CCM party member - they all stink! Wananuka RUSHWA.. NUKTA

Mabadiliko hayataletwa na nani ni SPIKA bali sisi Watanzania wenyewe - attempt yetu on 31/10 was marred by all sorts of shit*, but always there in next time, and the REGIME change is well underway!
 
Hivi kwani lazima Spika awe Sitta??no way he has to go ni MNAFIKI sana huyu mzee..i Hate him..ni mara 100 chenge awe spika kuliko sitta..huyu si ndo kajenga ofisi ya spika kwa 500m
Kwa hilo Sitta bado ni afadhali, Mbona ofisi ya spika ni bei kidogo ssana! na zile za Gavana wa BOT ilikuwa ngapi vile? Billion na watu walitetea.

Na ukusema Chenge ni bora kuliko Sitta lazima ulale usingizi tu basi, nasi tusiwe na huyo anayeitwa spika.
Huyu kaja na yake, tena hana hata aibu
 
Bora Sitta mara mia... huyu chenge kwa jinsi alivyoongea nia yake ya kutaka uspika inatia kichefuchefu... Hata kama ccm watachukiwa na wananchi kumbukeni bunge litaendeshwa kikandamizi kwa miaka 5!!

Sitta arudi halafu asiogope vitisho vya ccm... kwanza nimesikia tetesi ataachana na siasa baada ya miaka 5 so ni muda muafaka wa kurudisha yale aliyozima (iam sure kwa shinikizo la mafisadi). Watampata wapi tena akishaachana na siasa? Mafisadi na vibaraka vyao watamchukia lakini wananchi wa Tanzania watampenda na kumheshi na atastaaf kwa heshima kubwa... Popote alipo ujumbe huu aupate
 
jama jama chenge nanchukia sana huyu mtu Jamani hakuna aliyekamilika ila ni bora ya sita thithim ikimuweka tu chenge itakuwa imejitafuna
 
1. Weka hadharani ripoti ya Richmond hasa ule upande uliouzuia kuiokoa Serikali.
2. Tujuze Watanzania kuhusu ule unga wa Bungeni.
3. Waeleze wazi kuwa huzitaki siasa za majitaka.
4. Pambana na mafisadi popote pale hasa wanaotaka kuiuza nchi yetu.
5. Weka wazi zile kashfa za meremeta,kagoda na tangold ulizozizuia Bungeni.
6............

6. hamia kwa wapiganaji wenzako CHADEMA
7.mshauri mwakyembe, mwandosya, anne kilango malecela na ole sendeka nao wahamie ccm.
8.mwache rostam, abood, habib, dewji, kikwete, chenge na lowasa wao wabaki hukohuko ccm
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom