Spika Sitta na Usiri wa Mikataba na majibu ya serikali

Mazuzu maheshimiwa yote yatajikamatisha mwaka huu, kila moja kwa nafasi yake atanena kwa kinywa chake ujinga wake. Malima wewe tulia kijana, mapafu huna Watanzania wamejanjaruka. Unajitega mwenyewe, ushindani upi? kwa biashara ipi?
 
Hawa nilishwaasa tangu mwanzo waache kukimbilia wake za watu

matokeo yao ndio haya!!!wanamtia aibu bwana wao (kikwete)

na kuonekana kumbe lile baraza hata punda anaweza kaa!!!!1
 
Wadanganyika bado tuna safari ndefu saaanaa! Yaani mkataba umeshasainiwa then atokee mtu mwingine mfanyibiashara kumzunguka mwenzie hiyo haipo popote pale. Ila kama anaongelea ushindani wa tenda au wakati wa mchakato wa kuendesha hiyo project hapo ya kuwa siri. Lakini mwekezaji keshapatikana, mchakato umeisha halafu mheshimiwa anasema wananchi hawana stahili ya kujua nini kimekubaliwa. Sasa hapo Mafisadi wanataka kuleta biashara ya kuuziana mbuzi kwenye gunia. Au kuna "ten percent" zao humo hawataki watu wajue??

Kama tunataka uwazi basi kila kitu kiwekwe peupe mara baada ya mkataba kusainiwa ili sote tujue nani anafaidika na kipi na nani kaingizwa mkenge!! Nampongeze spika SITTA kwa kuweka peupe jambo hili na sasa mafisadi wanajianika tu!
 
Mpumbavu utamjua kwa mawazo yake. Uwaziri wa kupewa kwa kujuana imekuwa matatizo.
 
(1) Katiba yetu inataka mikataba yote mikubwa kati ya serikali na wengine ipate ridhaa ya Bunge kwanza (nimeweka vipengele husika hapa zaidi ya mara moja). Waziri anayesema mikataba mikubwa ya uwekezaji ni siri, aidha hajui katiba au ni mhujumu wa katiba.

(2) Kuna kudanganya sana kwenye unyonyaji. Na kwa kweli ni mtu mjinga tu ndiye anayenyonyeka kirahisi. Naona Barrick Gold wamesema huenda wakajitoa Tanzania, eti kwa vile ubaya wa miundombinu unafanya faida yao kuwa ndogo. Hatuna barabara nzuri, lakini Barrick hao hao wanachimba dhahabu sehemu za Papua New Guinea ambazo hazina hata njia ya wapita miguu! Ni sehemu ambazo usafiri pekee ni wa helikopta. Na nchi hiyo, pamoja na ukweli kwamba haina Elimu kama sisi, haikubali rasilimali zake zichukuliwe bila malipo. Kwa mfano, wana mradi mkubwa wa gesi (LNG) na BUNGE lao limepitisha sheria kwamba angalau 19% lazima iwe mali ya nchi.

(3) Mkuu wa Madini Tanzania, Dr. Kafumu, kasema juzi kwamba tunapata 3% ya gross profit. Yeye anaelekea kuridhika nayo. Sisi tunajua hata hiyo 3% hatupati (inachukuliwa na wathibiti). Tumesoma juzi kwamba wahasibu wa Barrick na wengine huweka mahesabu kwa namna ambayo kunaonekana hakuna faida!

(3) Barrick Gold wanatingisha kiberiti. Wamegundulika kwamba wanadanganya kwenye mahesabu yao, na njia yao ya kujitetea ni kusema "msipoangalia tutaondoka"! Tuwabane walipe kodi inavyotakiwa. Kwani hatujui bei ya dhahabu? Ni uongo wanaposema wanapata hasara.

(3) Bunge lipitishe sheria inayoweka wazi maslahi ya taifa katika uwekezaji kwenye madini, mafuta na gesi. Sheria iliyopo hairidhishi. Hata wawekezaji wanakubali hairidhishi.
 
(1) Katiba yetu inataka mikataba yote mikubwa kati ya serikali na wengine ipate ridhaa ya Bunge kwanza (nimeweka vipengele husika hapa zaidi ya mara moja). Waziri anayesema mikataba mikubwa ya uwekezaji ni siri, aidha hajui katiba au ni mhujumu wa katiba.
.

kwa hiyo hata mheshimiwa Waziri wetu hajui hilo? ina maana hasomi katiba? hawa mawaziri wetu inabidi wajue kwamba haya majibu wanayoyatoa yanahitaji umakini!!
 
Nilishasema huko mwanzo "MTOTO WA NYOKA NI NYOKA" kwa hiyo msishangae huyu Adam Malima akionyesha ujinga na ufisadi wake kwani hata baba yake Kighoma alikuwa hivyo hivyo akawaruhusu wahindi misamaha ya kodi alipokuwa waziri wa fedha ; wahindi wakamdanganya watamuwekea 10% ughaibuni, LO alipokwenda kuzifuata ngawiwra zake huko akakuta hakuna kitu hatima yake jamaa akacollapse na kufa!! Mafisadi mwisho wao sio mzuri na huyu mtoto nadhani atakuwa kama baba yake, history repeats itself; kwani hata baada ya baba yake kufa alirithi chama alichokianzisha cha NRA na sijui CCM ilimuokota wapi? Pengine Kingunge na Makamba wanajua. Haya ndio matunda ya kuleta watu kutoka upinzani kuja CCM; wanajaza wachumia matumbo tu!! SITTA was discussing about "CONTRACTS" and not "TENDERS" sasa mambo ya commercial secrets yanatoka wapi?? Kijana anaonesha how uneducated he is. Kazi kwako Jakaya hiyo ndio team yako ndio maana bondeni kwenye world cup huwezi kufika.
 
This 4th phase government gives me headache really. Tumuamini waziri gani sasa? Nadhani kuna haja wana JF tuanzishe thread maalumu ya kujadili utendaji wa kazi na uwezo binafsi wa kila waziri.
 
Malima amjibu Spika Sitta
• Usiri wa Mikataba

na Esther Mbussi

NAIBU Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima, amesema mikataba ya uchumi na kibiashara inayosainiwa nchini, haiwezi kuwekwa wazi kutokana na ushindani wa kibiashara.

Kauli hiyo aliitoa jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari kuhusu usiri uliopo katika utiaji saini wa mikataba ya madini ambayo katika siku za hivi karibuni imekuwa ikipigiwa kelele za kutoifaidisha nchi.

Malima ametoa kauli hiyo siku moja tu baada ya Spika wa Bunge, Samuel Sitta, kuhoji kuwepo kwa usiri katika kusaini mikataba ambayo haitoi fursa ya kutekelezwa kwa masilahi ya umma na badala yake wawekezaji wa kigeni ndiyo wanaofaidika.

Alisema kamwe mikataba hiyo haiwezi kuwa wazi wakati wa mchakato na utiaji saini lakini itawekwa wazi katika utekelezaji tu baada ya makubaliano hayo kuafikiwa.


"Kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa wananchi na hata baadhi ya viongozi wakihoji usiri wa nini na kwa faida ya nani? Ukweli ni kwamba huwezi kuweka wazi mkataba na mwekezaji katika hatua za awali kwani huwezi kujua nani atakuja na wazo kama la yule wa awali, kwa hiyo ni ushindani wa kibiashara na si vinginevyo, kitakachowekwa wazi ni utekelezaji, kwa wabunge na wananchi kwa ujumla," alisema Malima.

Alisema katika biashara kuna watu husikiliza nani anataka kufanya nini, kwa hiyo kuwekwa wazi kwa mikataba hiyo kunaweza kuathiri nchi kukosa wawekezaji kutokana na mwekezaji mwingine kuchukua siri au wazo la mwenzake na kumzunguka.

"Kinachofanyika kabla ya kusaini mkataba wewe kama mwekezaji ni kupata maelezo yako, kwamba utafanya hili na lile, utalipaje kodi, na vitu kama hivyo, kwa hiyo kujianika kwako hadharani (mwekezaji), ni kumuwezesha mwenzako kutaka kufanya ulichokusudia, hakuna mazingira ya rushwa wala kuuza nchi katika suala la kusaini mikataba," alisema Malima.

Moja ya mikataba ya siri iliyowahi kufanywa ni ule wa mgodi wa Buzwagi unaomilikiwa na Kampuni ya Barrick ya Uingereza, uliosainiwa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, aliyejiuzulu Februari mwaka huu, Nazir Karamagi.

Juzi, Sitta alisema kuna makubaliano baina ya serikali na ofisi ya Bunge yaliyofikiwa kuwa mikataba yote ya maendeleo waziri husika anapaswa kumpatia Katibu wa Bunge ambaye ametengewa masijala mahususi ya wabunge kuona mikataba hiyo.


"Kuna mantiki gani kwa waziri kwenda ughaibuni na kutuambia kuwa anakwenda kusaini mkataba wenye masilahi yetu wananchi na baadaye akirejea atuambie walichokubaliana ni siri, hata kwa wawakilishi wetu, yaani wabunge? "Tutapimaje kama masilahi ya nchi yamezingatiwa au mhusika amekwenda kuiuza nchi?" alisema Spika.

Alisema wanaoendeleza dhana ya usiri dhidi ya mwenye mali ambaye ni mwananchi, wanalo jambo na wasakamwe ili waache mizengwe, usiri wa namna hiyo ndiyo unasababisha wanahabari kuandika habari za kuhisi au kile wanachokiamini kuwa ni sahihi.

Sitta aliishauri serikali kuweka utaratibu ulio wazi kwa kila wizara kuwa na dawati la taarifa, ambapo wanahabari na wananchi wataweza kupata habari za uhakika kuhusu utekelezaji wa majukumu yaliyo chini ya wizara hizo.



My take -Mikataba na ushindani, wapi na wapi ama anamaanisha tenda ? Kwa tamko hili Malima amechemsha na ama aombe radhi au ajiuzulu.


Kweli kabisa Mag3. Kauli yake imevuruga zaidi.
Yaani huo ndio anauita ushindani? Mbona kinachofanyika hapo ni kuzuia ushindani?
Aggrrrrrrrr!
 
Hii ni taabu ya kumpa mtu cheo kwa kuangalia urafiki zaidi ya uwezo.Michango ya Adam Malima katika vikao vya bunge kabla ajazawadiwa unaibu waziri ilikuwa ya hovyo kupitiliza.Nakumbuka jinsi alivyomshambulia Zito katika hoja ya Buzwagi,alimpongeza Karamagi kwa kusaini mkataba haraka nje ya nchi.Haishangazi hata kidogo kwa bwana Malima kutuambia mikataba ya uchumi na kibiashara inayosainiwa nchini, haiwezi kuwekwa wazi kutokana na ushindani wa kibiashara kwasababu ndiyo kikomo cha uwezo yake.
 
Augustine Moshi,

You are a scholar, a gentleman and a class act.

Thanks for that illuminating piece.
 
Kama waliyochanganua wajumbe hapo juu, usiri unaweza kuwepo kwenye hatua za awali za makubaliano baina ya serikali na mwekezaji. Naomba hapa hoja isiwe kwa wachimba madini peke yake, bali kwa mikataba yote mikubwa yenye maslahi kwa taifa. Serikali inapaswa kudisclose kile walichoafikiana na mwekezaji baada ya kuwa wamekubaliana. Kama wananchi (kupitia wabunge) wataona kuna mapungufu, basi mkataba huo urekebishwe kabla mwekezaji hajaja kuwekeza hapa nchini. Yaani kwenye hiyo contract kuwe na clause inayosema kwamba this contract will be executed subject to agreement by majority of members of parliament. Hapa bunge litapata nafasi ya kuchambua mikataba yote mikubwa na ikiwezekana kupiga kura na kuuipitisha au kuikataa ile isiyo na maslahi kwa taifa. Pia ni nafasi kwa bunge kujua nini hasa kilichoko kwenye mkataba ili leo na kesho wawe na majibu kwa wananchi.
 
Mkuu Augustine Moshi,
Hilo somo zito sana shukran... Na huyo Malima anatakiwa kuomba samahani huu mchezo wa kubadilisha maneno pizani ya katiba ya nchi ni utovu wa adabu na heshima mbovu kwa wananchi...

Kwa afikirie hili, ikiwa yeye kama waziri na wengine wote walioshirikishwa kutazama na kupitisha mwekeshaji mmoja iwe Barricks hiyo siri iko wapi?..Hao walioutazama mkataba sio Watanzania na wakitaka kuvujisha hiyo siri kwa mwekeshaji mwingine watashindwa kitu gani...Hakuna siri ndani ya mapendekezo ya mwekeshaji kwa wananchi, wala hakuna miiko, sheria ama utaratibu wowote wa KIBIASHARA acha hizo SIASA, unapinga mkataba wowote kati ya nchi na shirika kupitiwa na Bunge, unless uwe unahusiana na Usalama wa Taifa ktk swala la muda mfupi.
Ndugu zangu hakuna usiri wa awali ama wakati gani kwani kinachozungumziwa hapa ni kodi na pato la Taifa sio sehemu ya mwekezaji, na sidhani kama Malima ana maana hana imani na Bunge letu inapofikia maswala ya siri..Bunge letu linaweza kuitunza hiyo siri..
Katika kuvutia hao wawekeshaji masharti yetu yote huwa wazi ili wawekeshaji wote wafahamu tunacho (nchi) offer, iwe kodi ya mapato, ushuru na kadhalika bila usiri hivyo ndivyo tunavyowavuta wawekeshaji nchini sasa iweje wao waingie kwa usiri usiri wakati sisi wenyewe kama nchi tupo ktk mashindano vile vile ya kibiashara.
sasa iweje kuwepo na siri kati ya serikali na mwekeshaji inapofikia wananchi kutaka kujua kama kuna uwezekano wa mwekeshaji amepewa tender fulani... hii ikiwa ni pamoja na kuandaa mipango ya kuwahamisha wananchi, wananchi kufahamu ni vipi watanufaika na uwekeshaji huo. Hii mbona inanukia kama ndoa ya kul;azimishwa kwa wananchi wakazi wa sehemu zinazohusika. ndio maana tunapata matatizo kila siku kuhamisha watu kwa sababu ya Usiri uliojengwa na hawa viongozi wetu.

Huu ni Upuuzi mtupu, hii miwaziri ipo tu kutazama matumbo yao utadhani nchi hii ni ya kwao...On the record, huyo Malima alimpongeza Karamagi kwa mkataba wa Buswagi na hata kudhihaki bunge kwa kejeri akisema kuwa - Kama Karamagi anawajua wawekeshaji wa madini awapeleke jimbo lake, Utafikiria yeye ndio mmiliki wa jimbo hilo..
 
Huyu bwana mdogo Adam Malima aliyemtetea Karamagi kwa kusaini mkataba wa kuchimba madini Buzwagi, hatimaye akapewa unaibu waziri na bwana Kikwete.

Bado kuna watanzania wenzetu wanataka tuamini JK ni kiongozi anayeweza(competent leader). Maajabu hayataisha Tanzania hii.
 
Big up Mkandara!

Umechambua vizuri hoja nzima ya usiri katika karne hii ya utandawazi. Hakuna siri ya watu wawili duniani.
 
Back
Top Bottom