Spika Sitta Kupewa Tuzo na Maaskofu

UramboTabora

Member
Sep 11, 2008
49
2
na Prisca Nsemwa

MAASKOFU na wachungaji wa makanisa ya Pentekoste hapa nchini, wameandaa tuzo ya uongozi bora kwa ajili ya kumtunuku Spika wa Bunge, Samuel Sitta kwa kuuongoza vema mhimili huo tofauti na wakati mwingine wowote.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mchungaji William Mwamalanga, alisema wanatarajia kumpa Spika tuzo hiyo baada ya kuridhishwa na utendaji kazi wake, hasa kwa namna anavyoliongoza Bunge.
Alisema, Spika Sitta amejitahidi kuliweka Bunge karibu na wananchi tofauti na miaka mingine ambapo chombo hicho kiliendeshwa kama kiini macho kwa wananchi, kwa vile mambo mengi yalifichwa.

“Spika Sitta tuna kila sababu ya kumpa tuzo kwa kuwa ameweza kuliongoza Bunge ipasavyo, tofauti na miaka mingine yoyote, ndiyo maana baadhi ya viongozi mafisadi wanamchukia…Sitta ni Spika bora,” alisema Mwamalanga.

Mbali na hilo, maaskofu na wachungaji hao wamelaani kitendo cha Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kumlazimisha Spika huyo kujiuzulu na kutishia kumpora kadi ya uanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuwataka wajumbe wa NEC kumuomba radhi Sitta.

Mwamalanga, alisema kitendo walichofanya ni kuifahamisha jamii kuwa wanaendelea kuwakumbatia mafisadi kwa kuwa sababu zao za kumlazimisha ajiuzulu hazina msingi.

“NEC ni kipofu na inataka kutuingiza shimoni, lakini kwa kuwa tuna macho, tutaendelea kusema, na chama hakiwezi kutupeleka mahala pabaya kwa sababu zao ambazo hazina msingi,” alisema Mwamalanga.

Alisema, chama hicho kinamdhalilisha Rais Jakaya Kikwete kwa kuwa baadhi ya wanachama wake wanakumbatia ufisadi. “Chama legelege kinazaa vitu legelege, hatuwezi kunyamaza endapo anatokea mmoja wa kukiweka chama mahala pa kuridhisha na wengine wakamkataa na kumtaka ajiuzulu, NEC imetushangaza.

“Rais awe mkali kwa viongozi wasio waadilifu, na ikiwezekana awapunguzie mishahara wasiofanya kazi ipasavyo kwakuwa viongozi wanaofanya kazi wanahesabika, mfano Spika Sitta na Magufuli,” alisema. Naye Askofu Thomas Faida, alisema kuwa ujasiri wa Kikwete umepotea kwa kulea watu wachache ambao wapo kwa ajili ya manufaa yao, hivyo ni wakati wake wa kurudi kwa wananchi kulijenga taifa.

Source: Tanzania Daima
 
yeah naamini kwa kiasi fulani hiyo nec ya ccm imeanza kuchimba kaburi la chama cha mafisadi hongereni maaskofu wa pentekoste.
 
That's a controversial timing! Let's hear the response from him and his foes!
 
CCM naichukia kwa moyo wangu wote,Tanzania ilistahili kuwa taifa tajiri sana Afrika lakini kwa sababu ya Upuuzi wa hili Genge haramu...tunaburuzwa kiuchumi na majirani zetu
 
Hii ina maana zaidi nafikiriri kuliko hata waraka.... Its very clear and objective confrontation!!

Ni Vitendo hadharani.

CCM na Kinguge waje na hoje nyigine sasa...But slowly wanajichimbia kifo na finaly watafanya a very clear blind mistake ... ya kujimaliza wenyewe!!
 
Kabisa si makanisa ya Pentekoste tu bali makanisa yote ya Kikristo na wale wa dini nyingine ambao wanapenda wazalendo wa Tanzania na wako against Mafisadi basi na wampe TUZO. He deserves this. Congrats our hero Mr. Six.

Pia nimefurahishwa kuwa hakuomba msamaha. Msamama wa nini wakati he is right beyond doubt. Again thanks for this.
 
Tatizo la wana JF ni hilo hupenda kuunga mkono ili mradi SISIM imelaumiwa bila kutazama mantiki ya jambo lenyewe.Sijui kama mnamfahamu Huyo anayejiita mchungaji mwamalanga?Watanzania tusijitie kuruka majicu tukakanyaga moto.Lets be careful with those people who claims kupambana na ufusadi.
 
Masikini TANZANIA..

Natumai SITTA atakuwa makini kuepuka tuzo hii. Kwa hali ilivyo kisiasa, kupokea TUZO hii kutoka kwa kundi fulani la kijamii haswa kidini na kutokana na hali ya kutokuaminiana inayoelekea katika chuki miongoni mwa watanzania wa imani tofauti, ni wazi tuzo hii itawagawanya zaidi watanzania na kumuingiza mtegoni Samwel Sitta.

Lakini pia tukumbuke kuwa mgawanyiko uliokuwepo sio kati ya dini kuu mbili tu bali hata miongoni mwa makundi ndani ya dini kuu mbili hizo....WALOKOLE factor ni sumu kali katika mahusiano yetu kijamii kuliko hata UKATOLIKI.

Politics is about perceptions, I can foreseen how this will be received by "others"...

omarilyas
 
MOD hivi JF hatuwezi toa nasisi tuzo kwa mzalendo wa kweli?

Masanilo na wengineo,

Kwanza niseme nakuunga mkono kwa 100%

Ebu tuachane na dhana ya siku zile eti kuwa member JF ni siri. Hii dhana si hai tena watu tunajuana kwa majina halisi, na bado tunao uhusiano mzuri tu na jamii, Chama/vyama pamoja na serikali tunayoikosoa

Nilifurahi jinsi Mode1 wa hapa JF alivyojitambulisha kwenye Mkutano wa Internet Governance hivi karibuni. Alisema mimi ni fulani bin fulani kutoka JamiiForums. Muulizeni nani kamugasi mpaka sasa?!

Shime, ebu walio serious tujadili JF Leadership Awards 2009
 
Waangalie pia na vigezo vingine kama OFISI ya BUNGE inaendeshwa kwa uadilifu kiasi gani. Vinginevyo kumzawadia MBADHIRIFU na MZINZI kwa sababu ya kujua kulitawala jukwaa la Bunge pekee hakutoshi.
 
Waangalie pia na vigezo vingine kama OFISI ya BUNGE inaendeshwa kwa uadilifu kiasi gani. Vinginevyo kumzawadia MBADHIRIFU na MZINZI kwa sababu ya kujua kulitawala jukwaa la Bunge pekee hakutoshi.

Naunga mkona kaka, tusije tukatumika kuhalalisha MANYANG'AU MBADALA. Nidhamu binafsi, historia ya uaminifu na uadilifu kwa watanzania, rekodi iliyotukuka katika kuwezesha demokrasia ya kweli na sio pale tu maslahi ya chama na binafsi yanapokuwepo ni muhimu kuwa miongoni mwa vigezo vikuu...

omarilyas
 
Masikini TANZANIA..

Natumai SITTA atakuwa makini kuepuka tuzo hii. Kwa hali ilivyo kisiasa, kupokea TUZO hii kutoka kwa kundi fulani la kijamii haswa kidini na kutokana na hali ya kutokuaminiana inayoelekea katika chuki miongoni mwa watanzania wa imani tofauti, ni wazi tuzo hii itawagawanya zaidi watanzania na kumuingiza mtegoni Samwel Sitta.

Lakini pia tukumbuke kuwa mgawanyiko uliokuwepo sio kati ya dini kuu mbili tu bali hata miongoni mwa makundi ndani ya dini kuu mbili hizo....WALOKOLE factor ni sumu kali katika mahusiano yetu kijamii kuliko hata UKATOLIKI.

Politics is about perceptions, I can foreseen how this will be received by "others"...

omarilyas
All the problems are caused by people with desire to exult their evil whims within the ruling part. This award might be perceived as something to do with christians, but as a human being Sitta wants to see he is supported.As it is now, he has been cornered and if CCM wants to avoid the religious problems then all those accussed with plundering national resources should be held accountable and not supported. I don't think CCM cares about Tanzania if they continue to support day time thieves, pretending to be part supporters and members.
 
Back
Top Bottom