Spika Sitta, iachie serikali isambaratike | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Spika Sitta, iachie serikali isambaratike

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JoJiPoJi, Aug 16, 2009.

 1. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #1
  Aug 16, 2009
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,458
  Likes Received: 1,331
  Trophy Points: 280
  KILA jambo lina wakati wake na ukifika halizuiliki. Serikali inaelekea kuanguka. Dalili zinaonekana wazi kadri siku zinavyosonga.

  Ni vigumu watu kusahau kwa haraka, suala la kampuni ya kufufua umeme wa dharura ya Richmond Development LLC ya nchini Marekani, iliyopatiwa zabuni ya kuzalisha umeme mwaka 2006 hapa nchini.

  Hata kama kampeni kubwa zitapigwa kwa kuibua mambo mapya mengi na mengine yasiyo ya kawaida ili vyombo vya habari na makundi ya watu wanaopiga kelele, wasahau au waelekeze nguvu huko, ni vigumu kwa kwa Richmond kusahaulika kirahisi.

  Kusahau au kukubali kusahaulishwa ni dhambi na haitakiwi, kwani leo hii suala hili limefika patamu na linavyokwenda jamii inatakiwa kuwa macho na kusimama imara bila kukata tamaa hadi ukweli uwekwe bayana na wahusika wawajibishwe.

  Hivi ni vita inayohitaji Watanzania wawe kitu kimoja na kutokukubali kurudi nyuma, mwanajeshi mzuri anapokuwa vitani daima harudi nyuma, ni lazima vita isonge mbele mpaka ushindi upatikane.

  Wimbo wa Richmond, bado unaendelea kuimbwa hata kama baadhi ya watu hawaupendi au wanaziba masikio yao, ili wasiusikie lakini ukweli unabaki kuwa ni lazima ukweli na uwazi utawale katika sakata hilo.

  Tulipofikia sasa ni dhahiri kuwa ni vigumu kuzitenganisha siasa za nchi hii na suala la Richmond, ni vigumu kama ilivyo kwa ngamia kupenya katika tundu la sindano. Ni vigumu kukitenganisha Chama cha Mapinduzi (CCM), na ufisadi uliotendeka.

  Katika mjadala wangu hapa sitaki kugusia ufisadi wa aina nyingine, nitaeleza jinsi ambavyo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samuel Sitta, alivyo na jukumu zito la kuiacha serikali iwajibike kwa kushindwa kuwaadhibu watuhumiwa wa Richmond.

  Pia tunapaswa kuangalia jinsi ambavyo kama Spika Sitta, atakuwa makini, na kutumia vizuri madaraka aliyopewa na katiba ya nchi na kanuni za Bunge, anaweza kuiacha Richmond na wamiliki wake sambamba na kuwajibishwa kwa waliohusika kuipatia kampuni hiyo zabuni.

  Richmond bado inabakia kuwa mikononi mwa wana-CCM, wenyewe siku watakapoamua kuikataa na kuwakana waliohusika basi wananchi watawaelewa.

  Sote tunakumbuka Jumamosi ya Agosti 1, mwaka huu, ambayo binafsi ilinigusa, na ninajua kama ingekuwa kama ilivyokuwa imeanza kuonekana siku hiyo, katika mkutano wa Bunge wa 16, mijini Dodoma, Spika akaruhusu mjadala kuendelea, leo hii tungekuwa tumejenga historia mpya katika taifa.

  Sishabikii kuvunjika kwa serikali kama ninavyomtaka Spika Sitta aiache ivunjike, pia sishabikii kwa watu kujiuzulu katika nyadhifa zao, hapana!, ninachoka ni matokeo ya dhambi ya ufisadi iliyofanyika ya wahukumu wahusika. Watahukumiwa tu endapo tutaacha kuwalinda, au kuilinda serikali ambayo inawalinda mafisadi hao.

  Katika mkutano wa Bunge, serikali ‘ilichemsha' bila kujua kuwa wabunge hawatakubali kuburuzwa kama ilivyofikiri, ilitoa taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge, kinyume cha matarajio ya wengi.

  Serikali inajua wazi kuwa wananchi, na wabunge walishatoa mapendekezo baada ya kudhibitisha kuwa wahusika ni kina nani, na kwa sababu Bunge halina mamlaka ya kumshitaki mtu mahakamani, liliiambia serikali itafute adhabu iwape wahusika hao.

  Kazi ya serikali katika suala hilo haikuwa kuchunguza, uchunguzi ulishamazika kupitia kamati ya Bunge ya Dk. Harisson Mwakyembe.

  Kilichotokea siku hiyo Bungeni, kwa walioshuhudia wataniunga mkono kuwa ilikuwa ni serikali kuvunjika ndani ya dakika chache, kuanzia saa 3:30 hadi saa 6:00 mchana ilitosha serikali kusambaratika na taifa kuingia katika uchaguzi mkuu upya.

  Spika Sitta ni miongoni mwa watu muhimu sana kwa chama hicho, ambaye ana jukumu kubwa la kukilinda chama hicho na serikali yake, na siku hiyo alifanya anachotakiwa kukifanya.

  Pamoja na hali ya kupingwa ndani ya chama chake, na kuandamwa na mahasimu wake kisiasa, ambao ni wana-CCM na wana-NEC wenzake, aliamua kuilinda serikali.

  Spika Sitta ana jukumu moja kubwa na gumu ambalo lipo mbele yake, lakini anaweza kulitekeleza kwa manufaa ya taifa, serikali ya CCM inayoongozwa na Rais Jakaya Kikwete, ilipofikia sasa ipo mikononi mwa Spika Sitta. Ndivyo ninavyoamini!

  Ina maana serikali ipo mikononi mwa Spika kutokana na nguvu ambayo Bunge linalo leo, na Spika kama kiongozi mkuu wa Bunge, analo jukumu la kulipa Bunge muda na nafasi ya kutosha kujadili suala hilo, na hata kama wabunge watataka kujiuzulu yeye akubali.

  Anapaswa kujua kuwa anapiga vita ufisadi, hapaswi kuwa katika chungu kimoja na mafisadi, anapaswa kuelewa kuwa alivyokubali kujitosa na kuliruhusu Bunge liunde kamati ya kuchunguza Richmond, anapaswa kuiachia serikali iwajibike mbele ya wananchi ambao wanawakilishwa na Wabunge.

  Tumeona jinsi alivyotumia madaraka yake kuiokoa serikali, katika mkutano huo wa 16, aliiambia ijipange na kutoa taarifa Bungeni Mwezi Oktoba wakati wa Mkutano wa 17. Kazi ipo hapo.

  Kinachotokea sasa ni kwamba Spika Sitta anaweza kuamua kuitetea serikali lakini akawapa wabaya wake nguvu ndani ya CCM, wakatumia nguvu hiyo hiyo atakayokuwa amewapa yeye wakamuangusha kisiasa.

  Kupigana vita na rushwa au ufisadi unabidi uwe mwendawazimu, au uikane nafsi yako kabisa. Sioni kama kuna haja ya Spika kuendelea kuilinda serikali. Aiache ibanwe, inyongwe kama inanyongeka, na kama inaanguka kutokana na uzembe wa wachache, basi na iwe hivyo.
  Huwezi kuvaa kanzu moja na mtu anayenuka kikwapa, itafika mahali harufu mbaya itakufanya umwachie hiyo kanzu aivae yeye na wewe unakimbia kununua mpya.
   
 2. ThinkPad

  ThinkPad JF-Expert Member

  #2
  Aug 16, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,851
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mh. Sitta, nikiongozi mmoja wapo ktk viongozi wenye upeo wajuu ktk kushughulikia mambo naamini hii hoja yako ni ya msingi sana na umetulia mno ktk kuipangilia ninachosema Mh atazingatia hii hoja yako imetulia kwakweli alafu huyo mshua huwa yupo makini sana.
   
 3. M

  Magezi JF-Expert Member

  #3
  Aug 16, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145

  source???
   
 4. Domenia

  Domenia JF-Expert Member

  #4
  Aug 16, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Duh!!.....
   
 5. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #5
  Aug 16, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Sam Sitta spika wa bunge letu hana budi kuachana na tabia ya POPO; ni wakati muafaka kwake kujitambulisha bila woga kuwa yeye hayukotayari kukiunga mkono chama ambacho kinawalinda mafisadi ambao wamekwishaamua kummaliza kisiasa. Sitta ni lazima atambue kuwa Serkali na viongozi wake wanawalinda mafisadi kwa uamuzi wa maksudi ili kulinda maslahi yao binafsi na ndio maana kuna umuhimu kwa bunge kusimamia kiamilifu maslahi ya Taifa ikibidi hata kuicha serikali inayowalinda wahalifu ianguke ili wananchi wapate nafasi ya kuchagua viongozi wapya!
   
Loading...