Spika Sitta Apotoka Tena Bungeni !- " Wapinzani wana Hila!"!. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Spika Sitta Apotoka Tena Bungeni !- " Wapinzani wana Hila!"!.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, Jun 10, 2010.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Jun 10, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,238
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,
  Nimekuwa nikifuatilia kipindi cha maswali na majibu ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu Pinda Bungeni leo asubuhi.

  Kumeulizwa jumla ya maswali 5 tuu badala ya 10, na yote ni kutoka wabunge wa kambi ya upinzani, hivyo baada ya dakika 15 tuu, kipindi hicho cha maswali ya papo kwa papo kilimalizika kwa spika Sitta kutangaza maswali yamekwisha!.

  Hivyo kikao cha bunge kiliendelea kwa kipindi cha maswali na majibu ya kawaida.

  Baada ya maswali mawili matatu, Spika Sitta aliintervene na kutoa ufafanuzi ufuatao, nimeparaphrase, " Najua wengi mtashangazwa na maswali kwa Waziri Mkuu leo kuwa yote yametoka upinzani!, hili sio bunge la wapinzani ni bunge la vyama vyote. Hali kama hii haiwezi kuachwa iendelee, lazima tutafanya uchunguzi nini kilitokea maana najua Wapinzani wana hila, wanaweza kuwa wamefanya manuva fulani"!

  Mhe. Sitta aliyazungumza hayo in a jocking manner, lakini ni maneno serious, kama kina Zitto, Dr. Slaa na wapinzani wengine wataiacha joke hiyo ipite tuu bila kuikemea,
  huko kutakuwa ni kumdekeza spika kuendelea kuliendesha Bunge kwa manufaa ya CCM.

  Kwa maoni yangu Spika amepotoka kwa kusema Wapinzani wana hila.

  Kitendo pekee cha kuwepo waulizaji 5 tuu tuka upinzani, ni uthibitisho toka, waliojitokeza ndio hao tuu, ndio maana maswali yaliisha baada ya dakika 15 tuu!.

  Kama kulikuwa hakuna swali toka CCM kuna ubaya gani?. Kama bunge wa CCM hawakuwa na swali, hiyo ni walakin?.

  Mhe Spika anasema hili sio bunge la wapinzani, nadhani status ya wabunge ndani ya bunge ni equal regardles parties affiliation, itakuja tokea siku pia kipindi hicho hicho cha maswali na majibu, kutakuwa hakuna swali toka upinzani, its ok.

  Kulikuwa na maswali mawili kutoka CUF na Matatu kutoka Chadema, eti kwa vile hakukuwa na swali toka CCM, basi ndio kuna hila, hivyo atafanya uchunguzi!
  Huu ni upotokaji!.

  "
   
 2. R

  Rwechu Member

  #2
  Jun 10, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mkuu kama ulivyobainisha kuwa ilikuwa joks nadhani tuichukulie joks, maana kama angekuwa serious hila angekuwa nayo yeye na wasaidizi wake maana wao ndo wanapokea majina na yeye ndo anaruhusu watu kuuliza maswali. Hope alikuwa analichangamsha bunge mkuu Pasco
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  Jun 10, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,238
  Trophy Points: 280
  Ok Rwechu, na tukubali it was a joke na kina Zito na Kina Slaa can stand such jokes kuelekea uchaguzi, ila kama ni kweli atafanya uchunguzi kwa nini CCM hawakuuliza swali, itakuwa sio jokes tena.
   
 4. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #4
  Jun 10, 2010
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Wapinzani hawaridhishwi na utendaji mbovu wa serikali ndiyo maana maswali mengi bungeni hutoka kwao. Nilikuwa nafuatilia pia kipindi cha maswali ya kawaida ambayo karibu yote pia yalitoka kwa wabunge wa upinzani kiasi kwamba Spika akaingiza utani tena kuwa leo ni siku wa wapinzani. CCM waseme au waulize nini wakati ilani waliyoitunga ndiyo hiyo inawatia kitanzi linapokuja swala la utekelezaji?
   
 5. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #5
  Jun 10, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,158
  Likes Received: 1,246
  Trophy Points: 280
  Kauli ya 6 ina maana kubwa sana, sio kwa wapinzani tu hata kwa CCM pia. Wabunge wa CCM wameenda kufanya nini sasa pale ikiwa wote zaid ya 200 wanashindwa kuuliza hata swali moja?
   
 6. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #6
  Jun 10, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  jamani tusimuunee huyu mzee wa watu hapa kuna tatizo la msingi kwanza ni kuwakumbusha wabunge wa ccm wawahi mapema alhamisi kujiandikisha ili wamuulize waziri mkuu maswali lakini pia kwa yale maswali ya kawaida kutakuwa na tatizo limetokea wakati wa kuandaa list, kumbukeni ni huhuyu sita analaumiwa kuiumiza ccm so as speaker of the national assembly needs to be neutral na kuweka platform sawa kwa wabunge wote, good mr. speaker sir
   
 7. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #7
  Jun 10, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Wabunge wa CCM wanawaza tu ni jinsi gani watarudi tena bungeni baada ya kupiga kambi DAR kwa miaka 5! walikuwa mjengoni kwa ajili ya posho tu, mawazo yao sasa hivi ni 31-10-2010, maana wanajua ile njia yao ya muongo sasa imefika mwisho!
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Jun 10, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,238
  Trophy Points: 280
  Bill, kwa vile huu ni mwaka wa uchaguzi, concetration yote ni majimboni, hivyo wabunge wa CCM kama wameamua kutouliza maswali kwa serikali ya chama chao ili kukinusuru kuna ubaya gani?.

  Tena mimi ndio ningekuwa mbunge wa CCM, huu ndio wakati wa kuuliza leading questions ili kuipaisha resikali mbele ya macho ya jamii kwa mfano
  Tangu serikali ya awamu ya nne imeingia madarani, kumekuwepo hisia kuwa haiko serious kwenye kupambana na rushwa na ufisadi,
  Hapo Pinda angepitisha ufagio wa nguvu, tumewashitaki mawaziri, kesi za Epa ziko mahakamani, na kesi hii, na kesi hii na kesi hii, ila pia serikali hii ya awamu ya mne, ina heshimu inazingatia sana suala zima la utawala bora na kuheshimu uhuru wa mahakama, hivyo hata wote wataonekana hawana hatia, sisi tutakuwa tumetimiza wajibu wetu kwa asilimia 100% makofi... etc.

  Hoja yangu ni kuwa, hakuna kanuni ati maswali yatoke wapi, ila kwa vile Wapinzani wanaibana serikali, Spika 6 ananawa mikono, asijeonekana ni yeye ana wa line-up wapinzani tuu ili waisulubu serikali, baada ya Mpendazoe kulikoroga CCJ, kwa kutangulias, wakati mpango wa awali ulikuwa Bunge likashavunjwa, ndipo wajimege, sasa hawajimegi tena, hivyo Sitta ana kibarua kigumu cha kujikomba serikali kuwa yeye ni mtetezi wa serikali ndani ya bunge, ndio maana amechachamaa kwa nini wapinzani ndio wameachwa kuisulubu serikali.

  Tena bunge hili, ndilo litaongoza kwa misusuru ya wageni, haswa viongozi wa vyama wa vilaya wakija kuwazuru wabunge pendwa wao ili kuwadhibitishia uungwaji mkono wao, at the same time free pre campaign live on TBC na Star TV. Kila mbunge atatembelewa this time.
   
 9. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #9
  Jun 10, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,582
  Likes Received: 4,692
  Trophy Points: 280
  Wabunge wa CCM siku zote kazi yao ni kubeba serikali hivyo haishangazi. Na ni kuthibitisha ile nadharia ya kuwa mbunge mmoja wa upinzani na sawa na wabunge 50 wa CCM.
   
 10. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #10
  Jun 10, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Inawezekana alikuwa anawasema wenzie wa CCM indirectly kwamba ndio wamefanya 'hila' kwa kutokuuliza swali!
   
 11. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #11
  Jun 10, 2010
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kwani kumuuliza PM swali la papo kwa papo ni lazima? Pia maswali ya msingi huwezi kuuliza papo kwa papo kwa vile mhusika ana nafasi kubwa ya kulikwepa akisingizia anahitaji muda ili kuweza kutoa majibu ya kina!
   
 12. M

  Mkono JF-Expert Member

  #12
  Jun 10, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 569
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  6 alikuwa anajikweza ili wenzake wasije kuanza kumtuhumu na hatimaye kumpiga chini ktk nyakati hizi za lala salama.Kilichonifurahisha ni swali la MH Halima Mdee kidogo majibu ya PM kama yatafanyiwa kazi na tume haki inaweza kutendekeka em tusubiri tuone maana unaweza kusikia Tendwa anakwambia hana bajeti hiyo.
   
 13. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #13
  Jun 10, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Ah hii nchi kwa jokes imezidi sasa.
  nasikia hata majambazi wanajoks wanapofyatua risasi hewani kuwatisha watu ili wawaibie
   
 14. P

  Paul S.S Verified User

  #14
  Jun 10, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  minadhani ni jokes kama ulivyosema hayo ni maneno ya kawaida kabisa katika siasa, usipaniki ndugu
   
 15. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #15
  Jun 10, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  ...hasa katika ishu siriaz.... eeeh?!!!!!
  tuamini ni jokes na tuendeleze jokes ili tujenge taifa letu
   
 16. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #16
  Jun 10, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Sioni ubaya wa 'joke' hii Pasco. Mara nyingi Six amekuwa akitoa jokes za aina hii bila kumaanisha kitu chochote kibaya.
   
 17. M

  Mugerezi JF-Expert Member

  #17
  Jun 10, 2010
  Joined: Mar 28, 2007
  Messages: 454
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Maswali kutoka kwa upinzani inaonyesha wabunge hao wako kazini muda wote. Lakini pia inaleta picha nyingine kuwa wabunge wa ccm licha ya kuwa wengi bado ni wavivu na wanaenda pale kupokea vijisenti vya walipa kodi bure tu.

  Maneno ya spika hata kama ni joke lazima hansard za bunge ziwekwe sawa kwa wakina Zitto na group lote kulisemea hili. Lakini pia huyu Spika wetu alikuwa anajikosha kwa CCM maana wote tunajua wanavyosema kuwa yeye mchonganishi kati yao na serikali.
   
 18. m

  mtemi Member

  #18
  Jun 11, 2010
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  vp swali la Mwerra wa tarime kuhusu wanawake kuwanyonya shemeji zao sehemu za siri kwa kurazimishwa na wale polisi wa kanda maalum??????......
   
 19. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #19
  Jun 11, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,238
  Trophy Points: 280
  .
  Mzee Punch, nimekubali, if it was a joke, then its fine let it be a joke, ila hata siku ile alipoomba ulinzi baada ya kushutumiwa sana kwenye forums, to me it was like a joke, jamaa alipewa ulinzi wa ziada.
  Enzi za Julius, alitembea na magari 3 tuu, Mwinyi akaongeza, Che akaongeza Mkulu kila apitapo, more than 10 any time T.

  Mama Maria na Mama Sitti wao walikuwa gari moja moja tuu, Mama Anna akapewa na Pikipiki , sasa Mama Salma naye anachokajimsafara chake na mpiga picha pia.

  Wakuu wa polisi, na Tiss eti nao wana magari matatu matatu, kwa vile mimi sio mwelewa issue za kuisalama, labda kweli kuna kitisho cha kiusalama kihivyo, ndio maana sometime nashindwa kudistinguish true joke na reality jokes.
   
 20. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #20
  Jun 11, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Mkuu wabunge wa CCM wana kihoro sasa hivi, nani ana muda wa kubuni haya mambo? More than 70% hawana uhakika wa kurudi, kinachowaweka kule ni kusubiri retirement benefit kujazia strategy za kampeni...
   
Loading...