Spika Sitta amtimua nje Cheyo (UDP) Bungeni kwa kubishana naye!

Selous

JF-Expert Member
Jan 13, 2008
1,325
144
Jamani ilikuwa hivi;

Cheyo ameuliza swali kwenye kamati za kupitia mahesabu ya wizara ya mazingira. Alipouliza Sita hakuelewa ikabidi amuulize tena. wakati anauliza Sita akaingilia kuwa je wewe ni chemisty? jamaa akamwambia. baada ya kuuliza sita akamwambia hayo yalishasemwa na waziri.

cheyo akasema ndo umejibu? sita akasema ameshatolea maelezo sio majibu. cheyo akasema hajaridhika.

Sitta kamwaga radhi eti wapinzani wanapenda sana kila kitu wadikteti tu maana waklishasema lazima wasikilizwe tuu. akasema eti cheyo akishakalia kiti basi huku UDP hakuna mtu kuzungumza. Sita akasema eti cheyo anasema chemical haiunguzi mara moja. cheyo uvumilivu ukamshinda. basi akasimama, sita akamwambia kaa chini yaani kama polisi. nakwambia kaa chini. cheyo akaamua kuondoka na sita akasema sajini mtoeni nje. akatoka nje.

i474_CheyoJune09.jpg

Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo akitoka nje ya ukumbi wa Bunjge Mjini Dodoma Juni 29, 2009 baada ya kuamriwa kufanya hivyo na Spika wa Bunge Samwel Sitta kwenye kikao cha jioni. (Picha kwa hisani ya Ofisi ya Waziri Mkuu)
 
Last edited by a moderator:
Spika wa Bunge la Jamhuri amemfukuza nje ya ukumbi wa bunge mheshimiwa John Cheyo, baada ya koungea wakati yeye spika akiongea...kabla ya hapo mheshimiwa Cheyo alikuwa anamuuliza waziri kuhusiana na suala la North Mara na madhara yake kwa wananchi wanaozunguka....je, Spika anailinda serikali au udikteta umeanza kumzidia na sasa unatoka?? Kwa ntu makini aliyekua anafuatilia mjadala, Sitta alimprovoke Cheyo,haipingiki!!
 
nafungulia TBC dakika chache zilizopita nikakuta Sitta akiamuru Mh. John Cheyo Mbunge wa UDP atolewe nje ya ukumbi wa Bunge. kisa eti Cheyo hamsikii. cheyo kasema Mgodi wa North Mara unatoa chemicals ambazo zinaathiri wananchi taratibu. yeye kasimama kwa jeuri na kusema kama ni kemikali italeta madhara mara moja. cheyo naye kamtolea uvivu na kusema amesomea Textile Chemistry na anajua anachosema. Sita kawa mboyo na kuamuru askari wake wamtoe nje mara moja.
na mara nikasikia Sitta akiongeza "naona wabunge wa upinzani wanataka kuendesha bunge kwa udikiteta"
kwa kweli nimeshangaa na kusikitika.
habari zaidi zitakuja na bila shaka hansard za bunge zitaonyesha kwa uzaidi.
nawasilisha
 
Spika sitta anadai Cheyo alikaidi amri yake na kutaka kubishana nae ndio maana akamtoa nje
 
Sisi tunasema kuwa Sita ni mbabe sana sana hivyo kuwa na Wabunge wengi wa CCM ni Tatizo kubwa sana
 
Spika sitta anadai Cheyo alikaidi amri yake na kutaka kubishana nae ndio maana akamtoa nje

Lakini si walikuwa live? wacha tusubili maoni ya walio ona kilicho endelea, haya ni makubwa sasa, lakini kwanini amalizie kwa kusema anaona wapinzani..... hapo lazima kuna kitu.
 
Kumbe bado ana donge moyoni la Mh Zitto, sasa hapa ngoja tusubiri details zaidi, but hii ni too low kwa Spika!
 
Lakini si walikuwa live? wacha tusubili maoni ya walio ona kilicho endelea, haya ni makubwa sasa, lakini kwanini amalizie kwa kusema anaona wapinzani..... hapo lazima kuna kitu.

Kwa kweli bunge hili ni upuuzi mtupu! Sitta anadai chemicals zinadhuru papo hapo, hajui kuna nyingine na Carcinogic kama heavy metals. Akasome kilichotokea Minamata, Japan! Dawa ni kuhakikisha dominance ya CCM 2010 ndani ya Bunge inapungua by at least 40%
 
Selous,
Asante kwa ujumbe. Naona umeuandika kwa haraka sana ili kutupa habari LIVE. Tafadhali kama wakimaliza, basi upitie ujumbe wako na u-edit na kuongezea maelezo ili usomeke kwa ufasaha zaidi. Ukisoma kuna vitu nashindwa kuviunganisha. Ila niseme tena, asante kwa ujumbe .....
 
Lakini umeelewa au vipi maana hoja uweze kusoma na kuelewa na pia kuna haja ya Kuchagua Spika asiye kuwa toka Chama Tawala
 
Selous,
Asante kwa ujumbe. Naona umeuandika kwa haraka sana ili kutupa habari LIVE. Tafadhali kama wakimaliza, basi upitie ujumbe wako na u-edit na kuongezea maelezo ili usomeke kwa ufasaha zaidi. Ukisoma kuna vitu nashindwa kuviunganisha. Ila niseme tena, asante kwa ujumbe .....


Naomba nisaidie hapo.

Nimeshuhudia spika Sita akimfukuza mbg. Cheyo. Sababu kubwa ni kwamba eti amedharau kiti cha spika. Niliona live na yaliyotoke ni haya;

Kwanza Cheyo aliuliza swali kwa Waziri Batilda akitaka kueleza kwamba hayo matatizo ya North mara ni ya siku nyingi na si ghafla kama ilivyoelezwa na Waziri. Spika kwanza kasema sikuelewi au rudia maana naamini hata waziri hakuelewa (sijui alijuaje). Cheyo karudia tena na kabla hajamaliza Spika kaingilia kati akitaka Cheyo aeleze kama kweli maelezo yake ni ya kisayansi. ‘Acid haiunguzi mara moja?” Cheyo akajibu anayo sayansi ya kemia, hivyo ana hakika. Spika akadai Cheyo kisha sahau Chemistry (kumbuka spika kasoma sheria). Cheyo akaonyesha kuridhika na mamlaka ya kiti cha spika lakini akasema hakuridhika na jibu la swali lake. Spika kaendelea na maelezo mareeefu ya kuonyesha kwamba Cheyo ni dikteta na akasema hajui huko UDP mambo yakoje.

Haya! Cheyo kasimama akitaka kusema kitu, mara kaambiwa kaa chini! Go out! Sajenti mtoe nje!

Maoni yangu ni kwamba, this was too much with this human so called ‘spika’ Nadhani sasa tuko hatua ngumu ya uongozi. Hata kama anayo madaraka ya kumfukuza mbunge bungeni, kuna lugha ya kutumia. Mara moja nilikubali kwamba huyo ndo Sitta. Hizi lugha za ‘go out!’

Kuna tabia ambayo naiona kwa spika Sita. Mara nyingi anakuwa activated akiona akina mama. Labda hapo hakutaka bi Batilda aulizwe swali. Nimemuona hata akitambulisha wageni wa wabunge wenzake pale Bungeni, akiwepo mwanamke, lazima atatoa comments za ziada ambazo mara nyingi huwa ni zile za kubembeleza. Nadani tuna tatizo
 
.....kwanza ilikuwa Mh.Zitto, sasa ni Mh.Momose......there is surely a big storm ahead, Spika ajiandaye tu....this is just the calm.
 
Hii ni Kusema kuwa Wabunge wa CCM mbona hawatolewi nje wa Kuambiwa kama hivyo, Sitta ni Mbabe bwana
 
Mimi nakwambia kuwa Ubabe huu utaisha mwaka 2010 kama Watzania wakiamua kufuata mafiga watatu
 
It is all about election na kuutaka u spika tena .Uchaguzi umefika na kuna mengi yatakuja .Wananchi wanaona na sijui itakuwaje .Hiki ni kiburi cha ajabu watu kudhani TZ inamilikiwa na wachache .CCM wamejawa na uoga na kukimbilia mambo mengi kama kutunga sheria nk.Wanaweza kujikuta wametunga sheria za kubana wakawa wapinzani ikawa kazi kwao .Huu ni uchaguzi Sitta anataka kuonyesha kwamba anaweza na hata kuibeba CCM.Lazima watete kemikali zile maana ni barrick huyo ambaye pesa yake huwapa nafasi ya kubakia madarakani .
 
Wakati na saa inakuja sio Mbali sana utaona mwakani itakuwa vipi, maana na huyu jamaa anakuwa mbabe sana sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom