Spika Sitta amsafisha Zitto Kabwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Spika Sitta amsafisha Zitto Kabwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by AmaniKatoshi, Jul 14, 2009.

 1. A

  AmaniKatoshi Senior Member

  #1
  Jul 14, 2009
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 158
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Sitta amshukia Zitto na kukwepa kosa la mwaka juzi

  Na Beatrice Bandawe

  14th July 2009

  [​IMG]
  Spika wa Bunge, Samuel Sitta.  Spika wa Bunge, Samuel Sitta, jana ametoa ufafanuzi kuhusu madai ya kutumia lugha ya kuudhi bungeni na kusema kwamba Bunge ni uwanja wa siasa za ushindani ambapo katika kutetea maslahi ya kiuwakilishi, migongano na mitazamo na hata ya lugha haiwezi kuepukwa.  "Mwanasiasa hasa kiongozi anatakiwa awe na ngozi ngumu inayohimili mikwaruzo ya maneno makali ya siasa bila kuchubuka kwa urahisi," alisema.  Spika alitoa ufafanuzi huo baada ya mara kadhaa katika mkutano huu na iliyopita ya Bunge, wabunge kusimama na kuomba mwongozo wa Spika kwa kumtaka Mbunge anayechangia afute kauli yake kwa kuhisi kuwa ni ya kuudhi na haistahili kuwa lugha ya kibunge.  Alisema ni jambo la kawaida katika mazingira ya pekee pale ambapo mjadala unapamba moto mzungumzaji anaweza akajikuta akitumia maneno makali.  "Waheshimiwa wabunge pamoja na waheshimiwa mawaziri ni binadamu na wanaweza kuwa na hisia kali katika mambo wanayojadili. Kwa hiyo, kutafsiri kanuni hii inayozuia "maneno ya kuudhi" kwa wigo mfinyu kuna hatari ya kuminya ule uhuru wa majadiliano uliopo katika ibara ya 100 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania."  Alisema katika mabunge mengi duniani kanuni za mijadala zinazuia matumizi ya lugha za kuudhi au kwa maneno mengine, lugha isiyo ya kibunge.  "Katika kanuni za Bunge letu, Kanuni ya 64 inaanisha mambo yasiyoruhusiwa bungeni katika mijadala. Miongoni mwa mambo yaisyoruhusiwa ni kutumia lugha ya kukudhi au inayodhalilisha watu wengine – kanuni ya 64(1) (g)," alisema.  Sitta alisema ukiwataka wabunge wazungumze bungeni mithilli ya mashahidi mahakamani, "utakuwa umeiondoa ladha yote ya mijadala bungeni."  Alisema katika mifano kadhaa katika mabunge mbalimbali duniani ambapo katika mazingira hayo, wabunge wamenukuliwa wakitoa maneno makali ambayo kwa tasfiri finyu mtu anaweza kuyaita ni ya kuudhi au hata ya matusi.  Alitoa mfano wa Bunge la New Zealand ambapo baadhi ya wabunge wa huko katika nyakati mbalimbali wamenukuliwa katika Hansard mwaka 1949 baadhi ya mawaziri walitajiwa kuwa ni sungura walioduwazwa na wasio na maamuzi ya kujitegemea na mwaka 1963 waziri alimwita Mbunge mwingine kuwa ni mwanamke katili na mwaka huo huo Mbunge mmoja alimwelezea Mbunge mwingine kuwa ni kama konokono aliyechoka akirejea kutoka kwenye mazishi.  Aidha, alitoa mfano katika "House of Commons" ya Waingereza ambapo mijadala inapopamba moto maneno makali hutumika, na kutoa mfano wa Mei 15, 1846, Benjamin Disraeli alimshambulia Waziri Mkuu Sir Robert Peel kwa kumwambia "Najua kwamba kwa miaka kati ya 30 na 40 mheshimiiwa ameishi kwa kutumia mawazo na akili za wenzake.  Maisha yake yote yamekuwa ni ya ubinafsishaji wa maoni ya wenzie. Ni mporaji wa akili za wenzake…Hakuna mwanasiasa ambaye amekuwa hodari zaidi kuliko huyu katika uhalifu wa wizi mkubwa wa ajenda za kisiasa."  Hata hivyo, Sitta alisema kwa mifano hiyo si nia yake kuwashawishi wabunge watumie aina hiyo au maneno mengine makali na yanayoweza kuumiza wengine.  Alisema Wenyeviti wa Bunge ni wasaidizi wa Spika na Naibu Spika katika shughuli za Bunge. Wanapokalia Kiti cha Spika na kuendesha vikao vya bunge wanafanya hivyo kwa niaba ya Spika na kwa wakati huo wanakuwa wanatekeleza mamlaka ya Spika na wanastahili heshima ile ile wanayopewa Spika na Naibu Spika.  Kwa mujibu wa Kanuni ya 67(2) Spika anaposimama wakati Mbunge anachangia, Mbunge anatakiwa kuketi mahali pake na Bunge litabaki kimya ili Spika aweze kutoa maelekezo au taarifa anayokusudia kuitoa.  "Spika anawajibika kutilia nguvu kanuni za Bunge na anawezakumtaka Mbunge yeyote anayekiuka utaratibu ajirekebishe," alisema.  Alisema kanuni zimeweka wazi kuwa Mbunge yeyote ambaye hataridhika na uamuzi wa Spika anaweza kuwasilisha sababu za kutoridhika kwake kwa Katibu wa Bunge ambaye hataridhika na uamuzi wa Spika anaweza kuwasilisha sababu za kutoridhika kwake kwa Katibu wa Bunge ambaye atawasilisha malalamiko kwa Kamati ya Kanuni kupitia kwa Spika.  "Kwa kuzingatia misingi hiyo niliyoieleza, tarehe 24, Juni, 2009 Mheshimiwa Zitto hakuathiri kanuni yoyote kwa kutamka kwamba mheshimiiwa Fulani alijibu "ovyo ovyo".  Tatizo hapa ni kwamba Mheshimiwa Zitto aliendelea kuyakaidi mamlaka ya kiti kwa kauli. '"Kwa hilo, ninamwagiza amwombe radhi Mheshimiwa Mwenyekiti, Zubeir Ali Maulid humu bungeni," alisema.  Hata hivyo, wakati Spika akitoa ufafanuzi huo,Yahya Kassim Issa, alitaka mwongozo wa Spika na kusema Tanzania ina ustaarabu wake na kwamba Tanzania inaangaliwa na nchi nyingine "sasa kauli aliyoitoa Spika hatuoni tunavuka nje ya maadili yetu."  Spika alimjibu Mbunge huyo kuwa ameshatoa mwongozo na hafahamu mbunge huyo anataka mwongozo gani mwingine.

  CHANZO: NIPASHE ​
   
  Last edited: Jul 15, 2009
 2. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hii safi sana, ni kumkoma nyani giladi mchana kweupe!
   
 3. K

  Kalimanzira Senior Member

  #3
  Jul 14, 2009
  Joined: Aug 15, 2007
  Messages: 100
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kuwa spika kuna hitaji busara zaidi, na hili limedhihirishwa na uamzi wa jana. Bila kuangalia alama za nyakati angejikuta matatani kama mwaka juzi!
   
 4. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #4
  Jul 14, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Ni kweli, Spika kazisoma vizuri 'alama za nyakati'!
   
 5. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #5
  Jul 14, 2009
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  SHERIA NA KANUNI ZA JAMII FORUMS

  Tafadhali jiepushe na mambo yafuatayo:

  1. Kumvunjia heshima, kumkejeli, kumtukana, mjumbe yeyote.

  2. Kuleta katika JAMII FORUMS maelezo yenye maudhui mabaya, au kuweza kuleta maudhi yoyote kwa wajumbe ama kwa wingi wake, ukubwa wake, au mfumo wake.

  3. Kuleta makala au kuendeleza mijadala yenye kuleta ugomvi,uchochezi na yenye muelekeo wa kutengenishana badala ya kuungana miongoni mwa wajumbe wa JAMII FORUMS na Watanzania wote kwa ujumla.

  .......

  5. Kutoa maelezo au shutuma dhidi ya mwanachama mwenzako, kiongozi wa au watu wenye hadhi kijamii bila kuwa na ushahidi wa kutosha kwa lengo la kuchafua rekodi safi ya mhusika kijamii.

  6. Ni sharti kwa kila mwanachama kutoa maelezo au mchango wake kwa uwazi na ukweli na kutomuogopa yeyote wala kumpendelea yeyote bali kuweka mbele maslahi ya taifa.

  7. Kila mwanachama yupo huru kutoa maoni yake mradi yaliyotajwa hapo juu yanazingatiwa.

   
 6. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #6
  Jul 14, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Amesoma Alama za nyakati Hongera kwa hilo
   
 7. Mnyisunura

  Mnyisunura Member

  #7
  Jul 14, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 69
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Na kumseba vibaya Jakaya Mrisho Kikwete! Huyu lazima asafishwe kokote kule hata kama nae ni f.............
   
 8. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #8
  Jul 14, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Angalieni maneno yenu; JF is not about gossiping is about fact; and with FACT no one can not be told; Kama wewe unaumbea wa hapa na pale ukome maana umbea wako usio na fact utakutokea puani; JF huenda hata si sehemu ya watu wote mliomo humu; wengine dare to go to dar hot wire; michuzi; na kwa global publisher kupata u daku; Hapa ni fact zinakatwa na kama hutaki fact go away while early usisubirie kufulia bure
   
 9. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #9
  Jul 14, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  niko nawe mkuu .watu walikuwa wanangoja ateleze tu aone cha moto
   
 10. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #10
  Jul 14, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Hongera Spika kuonyesha ukomavu
   
 11. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #11
  Jul 14, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nani katunga hizi kanuni?
   
 12. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #12
  Jul 14, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hii forum siku inaleta hoja za hovyo hovyo tu kila mara na sijui inakuwaje watu wanarudia hoja zile zile .Hii hoja iko hapa tangia jana mapema sana lakini bado mtu unarudia kuileta si usome kabla hujaweka haya ma mada ?
   
 13. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #13
  Jul 14, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hana chochote just another opportunist ameona nguvu za umma (wananchi) ziko against amenywea....wengine wanatakiwa wasome direction vinginevyo...aibu..
   
 14. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #14
  Jul 14, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180

  Mi sioni ni kwa vipi mada hii imeingia kwenye thread hii...
  I see as if this is a very different thing, which was supposed to appear on its own.
  Kaitaba kunani mzee!!!
   
Loading...