BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,099
Je, wale vibosile wenye hisa katika makampuni mbali mbali ya nje ikiwemo Barrick nao watatakiwa kutaja hisa ngapi walizonazo katika mahirika hayo!?
Spika Sitta ameonyesha mfano, wengine wamuige
David Azaria
HabariLeo; Monday,December 24, 2007 @00:02
SIKU kadhaa zilizopita Spika wa Bunge, Samuel Sitta, aliwatahadharisha wabunge kuwa mwaka huu atakuwa mkali na kuwachukulia hatua za kisheria wote watakaochelewesha kujaza na kurejesha fomu za kutaja mali na madeni yao ifikapo Desemba 31. Wakati Sitta akitoa tamko hilo bungeni, aliwataka wabunge wote kwenda kuchukua fomu hizo na kuzijaza haraka na kisha kuzirejesha kama inavyotakiwa.
Agizo la Sitta kwa wabunge wenzake limekuja siku chache tu baada ya kutangazwa kwa mabadiliko kwa Tume ya maadili ya viongozi na watumishi wa umma ambako sasa mali zote zitakazojazwa na viongozi wa serikali na wanasiasa zitahakikiwa na kuchunguzwa tofauti na zamani ambako walikuwa wakiziorodhesha tu.
Kwa hili Sitta anapaswa kupongezwa, lakini kikubwa hapa kinachotakiwa ni utekelezaji kwa sababu kuna maagizo mengi katika nchi hii ambayo yamekuwa yakitolewa na viongozi mbalimbali tena wa ngazi za juu serikalini, lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida baada ya maagizo hayo kutolewa hakuna ufuatiliaji wala uhakiki kama kweli agizo limetekelezwa.
Watanzania watafurahi kama itakapofika Desemba 31, yaani Jumatatu ijayo, wabunge wote watakuwa wametekeleza agizo hilo vinginevyo wawajibike kwa kufuata kifungu cha 15(a) cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, kinachosema kwamba kuwa kiongozi wa umma atahesabika kuwa amekiuka maadili kwa kushindwa bila sababu za msingi kutoa tamko linalotakiwa au kutoa tamko la uongo katika kipengele chochote muhimu.
Tukumbuke kwamba kwa mujibu wa Katiba, Mbunge ambaye ni kiongozi wa umma anayewajibika na Sheria ya Maadili ya viongozi wa umma atakoma kuwa Mbunge ikiwa itathibitishwa kwamba amevunja masharti ya maadili ya viongozi wa umma. Sasa hapa ndipo Watanzania wanaposubiri kuona msimamo wa Sitta kama alivyosema Bungeni hivi karibuni.
Lakini suala hili isiwe tu kwa wabunge. Tunao watumishi wengi wa umma katika maeneo mbalimbali nchini ambao nao wanatakiwa kujaza fomu hizo na kutaja mali zao. Kwa hiyo kwa kuwa Spika Sitta ameanza kuonyesha njia kwa kuwabana wabunge wake ni vyema na viongozi wengine katika maeneo ya wakafuatilia katika kuhakikisha kwamba wanawabana wakuu wao wa idara katika kutaja fomu hizo.
Ni vyema Waziri Mkuu akawabana wakuu wa mikoa na wilaya, wakurugenzi watendaji wa manispaa, halmashauri za miji na wilaya katika kuhakikisha kwamba wanajaza fomu hizo ili ziweze kuchunguzwa na Tume ya maadili ya viongozi na watumishi wa umma. Na kwa kuwa mabadiliko sasa yamefanyika na kuwaruhusu hata wananchi kuhakiki mali zilizotajwa na viongozi katika fomu hizo, basi nao waweze kwenda kuhakiki na kuwafichua wale ambao wana tabia ya kuficha mali zao.
Serikali pekee haiwezi kuwajua mafisadi, wala Tasisisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) hawana uwezo huo, Polisi na hata asasi yoyote ambayo ingeundwa katika nchi hii ama hata kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kulichunguza hili haliwezi kupata mafanikio pasipo kuwashirikisha wananchi ambao ndiyo wanaoishi na viongozi hawa.
Kwa hiyo kufunguliwa kwa milango ya kuingia katika ofisi za Tume ya Maadili ya viongozi na watumishi wa umma kwa mtu yeyote yule kwa nia njema ya kuhakiki mali za kiongozi wake kama ameorodhesha ukweli ama amedanganya, ni moja ya ushirikishwaji wa wananchi katika Serikali yao na hii ni moja ya utekelezaji wa sera ya utawala bora. Hata hivyo, hayo yote hayatafanikiwa kama walio katika mamlaka hawatamuiga Spika Sitta katika kuwasisitizia walio chini yao kuhakikisha wanataja mali zao kabla ya Jumatatu ijayo.
Copyright @TSN 2006 All Rights Reserved