Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samuel Sitta amedai kuwa kuna mtu/watu wamekuwa wakimtumia ujumbe wa vitisho kupitia simu yake ya mkononi. Akizungumza na TBC Taifa, Spika Sitta alidai kuwa ameshatoa taarifa ya jambo hilo polisi kwani hawezi kupuuzia vitisho hivyo ingawa alidai pia kuwa hao ni watu wanaokerwa na utendaji wake mzuri wa kazi.