Mwanamayu
JF-Expert Member
- May 7, 2010
- 11,650
- 6,859
Wakati shughuli za Bunge zikiendelea tarehe 16/11/2010 wakati wa kumchagua naibu spika Spika, Anne Makinda, amekuwa akivunja kanuni za Bunge. Kwa kufanya hivyo ametupilia mbali kabisa kiapo chake cha pili: Kanuni alizovunja ni ya 5 (2) Spika atawajibika kutilia nguvu Kanuni zote za Bunge, na Mbunge yeyote anaweza kusimama mahali pake na kumwarifu Spika kuwa Mbunge fulani amekiuka Kanuni.
Wakati Mustapha Akuunay wa Chadema alipokuwa anaulizwa maswali wakati wa kuomba kura za unaibu spika, Eng. Manyanya aliuliza swali nje ya hoja na Mustapha akamwambia Spika kuwa Eng. Manyanya amevunja kanuni. Cha ajabu Anne Makinda alikuja juu na kwa jazba akamjibu "Mimi ndio ninasimamia kanuni na ndiye natakiwa kusema ni mheshimiwa yupi amevunja kanuni na sio wewe".
Sasa katika hali hii ni nani amevunja kanuni? Mustapha Akuunay au Spika? Je, Spika anaifahamu kanuni hii? Au Spika ana kanuni nyingine kichwani kwake ambazo ametungiwa na mafisadi kupewa na fisadi mkuu Rostam Aziz kule Njombe ambako walikutana naye
Kanuni ya pili ni 10 (4) Mbunge yeyote atakayechaguliwa kuwa Naibu Spika, kabla ya
vyovyote vile sitatoa siri za Bunge. Ewe Mwenyezi Mungu, nisaidie. ]
Swali kwa wanawake wote Tanzania: je, Anne Semamba Makinda kwa haya anayoyafanya Bungeni mapema namna hii anawakilisha uwezo wenu wa kufanya kazi na jinsi mwanamke anatakiwa kuwa?

kushika madaraka yake, ataapishwa na Spika
Kiapo cha Naibu Spika ambacho kitakuwa na maneno yafuatayo:- ....
Hapa Spika alikisahau kifungu hiki mpaka alipokumbushwa na Katibu wa Bunge kwani alishamwambia Ndugai akavae joho wakati joho linaonesha madaraka ya naibu spika na asingeweza kufanya hivyo bila kula kiapo kwanza. Sasa ni nani muda wote huu atakuwa anamkumbusha kanuni za Bunge? Sheria huwa aiangalii umbumbumbu wa mkosaji wa sheria wakati inatimizwa, sasa Anne Makinda ashughulikiwe kufuata kanuni za Bunge hasa namba 134 na ibara ya 84 (7) (d) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania toleo ya mwaka 2005.
Pia Anne Makinda amekiuka kiapo chake cha pili [kanuni ya 9(20)]kwa kuwa mkali sana au kuwa na jazba pale ambapo mbunge wa upinzani hasa Chadema anapoongea. Jazba kwa wapinzani na kwa upole kwa wale wa CCM ni dhahiri kutokuenda haki kwa wote
[Mimi, Anne Semamba Makinda, naapa kwamba, nitaitumikia vyema na kwa moyo thabiti Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kazi zangu kama Spika wa Bunge, na katika kutimiza wajibu wa cheo hicho nitawatendea haki watu wote kwa mujibu wa Katiba, Kanuni za Bunge na Sheria, Mila na Desturi za Jamhuri ya Muungano na kwa