kurlzawa
JF-Expert Member
- Jan 23, 2018
- 16,707
- 20,606
Ndugui ni stomach defenderSpika Ndugai wewe hutokuwa wa kwanza ktk siasa za dunia kucheza haka kamchezo unakacheza ila mbaya zaidi pale unagusa ndio panaleta mashaka makubwa kwa kila mtu anayewaza vyema.
Huyu Prof Assad unayepambana naye mimi nataka kukuambia tu unapambana kwa hoja zisizo na nguvu kiasi wenye akili badala ya kuku support wamekaa kimya tena kimya kizito kiasi hata wewe unatishika na ukimya huu, ila nataka tu kukwambia wewe ni Spika na utakuwa ndie Spika ila kumbuka kuna mfumo huo kamwe huwezi kuutikisa sana sana unajitikisa mwenyewe kwa hoja ambazo sasa zimetoka kuwa hoja na kuwa maswali magumu yasio na majibu.
Hivi kweli Spika wewe una uchungu na kodi za wa lala hoi kweli? na kama jibu ndio je unafikiri hiki kitu ofisi yako imekianzisha kinaweza kuwa na majibu chanya ya kuwapa wananchi ama unawafanya watanzania waamini kwamba bunge pia linashirikiana na Serikali kuhujumu ofisi ya CAG kwa maslahi binafsi tusioyajua.
Kiukweli hapa ndipo hata Rais nadhani anakosa ujasiri kuungana na wewe kwenye hili suala la CAG. Serikali kwa kuona mbali na kujua dhamana kubwa aliyo nayo CAG inakwepa hoja zako kuepusha kituko cha mwaka ktk taifa. Kiukweli mashaka tunayo ktk hili.
Pili uliwaza nini mpaka kufikiria eti kwa kuwa tu umeamua kutofanya kazi na Prof Assad basi kesho yake atajiuzulu? Kweli kama kuna mtu alikulisheni hili tango pori walahi mtadhurika nalo maana Prof hatojiuzulu na mbaya zaidi hili wazo lenu limeleta maswali mengi kuliko majibu rahisi mnayotoa.
Tatu mimi naamini Rais ni taasisi sasa kumwambia Prof akajieleze kwa Rais bila kuitwa nalo hili limekuacha mtupu ktk mpango wako maana CAG hakuna mahali panasema kwakuwa Bunge hamfanyi kazi naye basi akajieleze kwa Rais hakuna hicho kipengele.
Mwisho mimi naona kuna kitu mkuu wakitafuta ila sina uhakika utakipata na napata shida sana unavyomtisha Prof eti mtamuonesha Bunge sio la kuchezewa sasa mtamuonesha nini?
Well, nashauri wanasiasa na viongozi wote wa vyama na Serikali kupima nafasi zetu na kauli zetu kabla ya kuziongea kwa sababu hakuna marefu yasiokuwa na ncha, pia kuwa kiongozi sio kufikiri utafanya lolote unafikiri utalifanya ipo nguvu zaidi ya bunge ipo nguvu zaidi ya viongozi wapo ktk madaraka na nguvu hii ni msaafu wetu Katiba.
Tukifikiri tutafanya vile tunafanya na kuweka maazimio ambayo kesho yake ni wembe mkali unatukata basi tusilie unapotukata. Kwa hili Mh Spika ninaamini umeanzisha jambo ambalo badala ya kumkosesha usingizi uliemkusudia linakukosesha usingizi mwenyewe na mara zote hubaki kuwa majuto ni mjukuu.
Sent using Jamii Forums mobile app