Spika Ndugai: Waziri akifanya kafanya, sio lazima awe mwizi

Sasa nataka kuamini Chama kile kipo kwaajili ya kuwasafisha wezi, mafisadi na wafananao! Ni vipi hakujibu tuhuma hizo hizo ambazo wananchi walizijua au kusikia kabla waziri huyo kuzisema?

Ni nani alitunga uongo woooote huo? Kwanini hakujali kabla? Ndio kusema ukiwa CCM hakuna wa kukutisha wala kujali lolote?

Anaposema alikomesha majangili, alitumia mbinu gani? Aweke hadharani ili zisaidie taifa. Isije kuwa uliweka walinzi wa kulinda majangili na hivyo mkala kilaini bila malalamiko wala purukashani na hicho ndicho unachoita KUMALIZA UJANGILI.

Kwa maoni yangu, mheshimiwa anajaribu kutuambia tusitegemee msafi aibuke kutoka kwenye dimbwi la mbolea ya binadamu.........eti wote ni nzi wa kizungu.

Tanzanians, you are on your own...........!
 
Tatizo hakuna wa kumwamini hapo maana Ufisadi ulisemwa wakati huo ukiwa makinikia na wenzako pia mwembeyanga walitajwa. Sasa tunaamini usemi ukiwa upande ule (makinikia) ulikubalika kwa UFISADI sasa upo huku tuhuma zimebaki au umehama nazo?

Ndio siasa zetu za bongo
 
Chenge endelea kuishikilia chama usiachie hata kidogo!

Kumbe Lowassa hagusiki? Maana hakuna anayethubutu hata kumtaja kwa jina ila Nyalandu wanamtaja tu!
 
Tatizo dira ni ipi? Katibu Mwenezi anasema bado ni wajamaa, mwingine anasema viongozi lazima wawe na vitega uchumi vingi, mwingine anasema anataka kurudisha Azimio la Arusha. Mkanganyiko mtupu!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom