Spika Ndugai, waonee huruma akina Halima Mdee. Jela uliyowaweka inawatesa na kuwatweza, ifike mahali uwaache

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,093
2,000
Amini nawaambieni, akina Halima Mdee (waliokuwa wanachama 19 wa CHADEMA na sasa wanatajwa kama Wabunge wa Viti Maalum) wanapata tabu na mateso makuu. Wanateswa na mioyo yao (kwamba wanaonekanaje mbele ya jamii kuitwa Wabunge huku wakiwa hawana chama chochote cha siasa kwasasa). Wamepoteza au kupunguza marafiki na kuongeza wanafiki; wamepunguza au kupoteza wanaowaamini na kuongeza wanaowatamani.

Huwa nazungumza nao. Huwa nateta nao. Huwa nawashauri. Wanachokisema kinaogofya kuliko chafya kwa ajili ya afya. Wanasema, wanashinikizwa kwa kulizwa kubaki Bungeni na Spika. Wanadai kuwa Spika anawaambia 'hawezi kurekebisha makosa yake kirahisi'. Anawaambia, kama ni mzigo wao waubebe yeye na NEC iliyompelekea majina kutoka 'kusikojulikana' kikatiba na kisheria. Wanasema kwa kuhema kuwa mara nyingi tu wamekuwa wakitaka kuachana na ubunge huo ambao nao wanauita feki ila hawawezi.

Tafadhali Spika Ndugai, waachie akina Halima Mdee. Kulazimisha kuwepo Bungeni si tu ni kinyume na katiba na sheria bali pia ni kinyume na ustaarabu wa kisiasa. Hata kama ni kufa na tai shingoni, tazama na hadhi na heshima ya akina Halima. Tazama wanavyonyooshewa vidole kama ngole; wanavyosemwa vibaya na wanavyoteswa na dhamira zao. Waachie wapate furaha yao; warudishe marafiki zao; wapambanie uanachama wao; wateuliwe na chama chao. Mateso yao yafike kikomo.

Kuwalazimisha akina Halima kuwa Wabunge 'wa upinzani' si sawa hata kidogo. Spika ulizungumzia utaratibu kama ulifuatwa au la ndani ya chama chao kuwafukuza uanachama. Ulijiridhisha kuhusu taratibu kama zilifuatwa katika kupatikana na kuteuliwa kwao? Hata kama unaona haya kwa kuwateua na kuwaapisha katika mkanganyiko na mgagaziko, muda wa kurekebisha bado unao. Ukiwaondoa Bungeni, macho yao yatalia ila mioyo yao itacheka.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Uyui, Tabora)
 
Bwana PGO

JF-Expert Member
Mar 17, 2008
43,133
2,000
Kuwalazimisha akina Halima kuwa Wabunge 'wa upinzani' si sawa hata kidogo. Spika ulizungumzia utaratibu kama ulifuatwa au la ndani ya chama chao kuwafukuza uanachama. Ulijiridhisha kuhusu taratibu kama zilifuatwa katika kupatikana na kuteuliwa kwao? Hata kama unaona haya kwa kuwateua na kuwaapisha katika mkanganyiko na mgagaziko, muda wa kurekebisha bado unao. Ukiwaondoa Bungeni, macho yao yatalia ila mioyo yao itacheka.
Supika alisema na akakiri yuko na faili lake Milembe
 
Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
3,082
2,000
Lema na Lisu lini mnarudi Tanzania?

Walituaminisha wamekimbia nchi na kwenda kulelewa na wanaume wa kizungu kama wakimbizi kwa sababu hapa nchini walikuwa wanatishiwa maisha na mwendazake.

Sasa hivi mwendazake hayupo je ni lini mtaacha kuishi kwa kulelewa na wazungu Ulaya mrudi Tanzania kujenga nchi na kula kwa jasho lenu? Tunahoji haya kwa sababu tunaona mko kimyaaa.

Mkiendelea kukaa kimya watu watajua mlikimbia nchi kwa masilahi yenu na siyo kwa kutishiwa maisha na mwendazake. Kwanza wewe Lema ulilipa lile deni lako la million 400 lililosomwa na spika Ndugai bungeni?

Rudi ulipe madeni ya watu.

Na wewe mzee wa MIGA Lisu rudi hutawakuta Acacia uliokuwa unawatetea sana utakuta kampuni mpya ya madini inayoitwa TWIGA
 
dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
15,243
2,000
... mbona rahisi sana; wajiuzulu huo ubunge feki! As simple as that wanakuwa huru!
 
MAGALEMWA

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
6,312
2,000
Lema na Lisu lini mnarudi Tanzania?

Walituaminisha wamekimbia nchi na kwenda kulelewa na wanaume wa kizungu kama wakimbizi kwa sababu hapa nchini walikuwa wanatishiwa maisha na mwendazake.

Sasa hivi mwendazake hayupo je ni lini mtaacha kuishi kwa kulelewa na wazungu Ulaya mrudi Tanzania kujenga nchi na kula kwa jasho lenu? Tunahoji haya kwa sababu tunaona mko kimyaaa.

Mkiendelea kukaa kimya watu watajua mlikimbia nchi kwa masilahi yenu na siyo kwa kutishiwa maisha na mwendazake. Kwanza wewe Lema ulilipa lile deni lako la million 400 lililosomwa na spika Ndugai bungeni?
Rudi ulipe madeni ya watu.
Na wewe mzee wa MIGA Lisu rudi hutawakuta Acacia uliokuwa unawatetea sana utakuta kampuni mpya ya madini inayoitwa TWIGA
Ujinga ujinga mbele kwa mbele
 
Analyse

JF-Expert Member
Jan 19, 2014
8,417

Mwangalieni na huyu
 
yakowazi

JF-Expert Member
Feb 9, 2012
1,679
2,000
Supika alisema na akakiri yuko na faili lake Milembe

20210416_034059.jpg
 
FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
24,311
2,000
Hili move lote la kichina liliasisiwa pale Lumumba, likapata baraka zote na Mwendazake pamoja na Spika - sasa Spika anaona kuwatema ni kumsaliti mwendazake !! patamu hapo.

Ila ningekuwa mimi ni mwana Covid-19, ningemtafuta Maza fasta nikamwambia kinaga ubaga mwanzo mwisho yaani episode loote lilivyokuwa then namwaga manyanga!! hela si kila kitu hapa duniani kuliko heshima na utu. Nasisitiza ni lazima umtafute maza ili ukishautema ubunge wao kesho na keshokutwa wasikusumbue sumbue kwamba hujalipa kodi tangu Uhuru 1961 wakati wewe umezaliwa miaka ya themanini, au umejenga nyumba yako kwenye chemchem ya gesi.

Halima alijijengea heshima kubwa sana nchini Tanzania, sidhani kuna mtoto wa miaka 5 hadi mzee wa miaka 100 Tanzania ambaye hamjui Halima. Sasa yote hayo yateketee kweli kisa tu kumfurahisha mwendazake na kundi lake dogo... hapana hapana. Halima tapika hilo kitu nafsi yako iwe huru..
 
Odhiambo cairo

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
14,909
2,000
Hili move lote la kichina liliasisiwa pale Lumumba, likapata baraka zote na Mwendazake pamoja na Spika - sasa Spika anaona kuwatema ni kumsaliti mwendazake !! patamu hapo.

Ila ningekuwa mimi ni mwana Covid-19, ningemtafuta Maza fasta nikamwambia kinaga ubaga mwanzo mwisho yaani episode lote namtemea then namwaga manyanga!! hela si kila kitu hapa duniani kuliko heshima na utu. Ni lazima umtafute maza ili ukishautema ubunge wao kesho na keshokutwa wasikusumbue sumbue kwamba hujalipa kodi tangu Uhuru wakati wewe umezaliwa miaka ya themanini, au umejenga nyumba kwenye chemchem.

Halima alijijengea heshima kubwa sana nchini Tanzania, sidhani kuna mtoto wa miaka 5 hadi mzee wa miaka 100 Tanzania ambaye hamjui Halima. Sasa yote hayo yateketee kweli kisa tu kumfurahisha mwendazake na kundi lake dogo... hapana hapana. Halima tapika hilo kitu nafsi yako iwe huru..
Ukweli Ndugai amekosea , na sasa kwa sababu wameshajitungia sheria ya kutokushtakiwa, basi anachofanya ni ulevi na ubabe wa madaraka.
 
Janja weed

JF-Expert Member
Nov 20, 2020
1,097
2,000
Sijawahi kuamini kama huyu mbweha ana akili hata ya kuvukia barabara, yani kiufupi Jobo ni mwendawazimu na wao wenyewe wenye mtu wao wanafahamu ,hilo halina mjadala
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom