PhD

JF-Expert Member
Jul 15, 2009
4,083
2,000
Leo Bungeni baada ya kipindi cha maswali na majibu, Spika wa Bunge Job Ndugai amesimama na kumkemea Nape Nauye, Mbunge wa Mtama ambaye hivi karibuni alitoa maoni yake binafsi kuwa wale wabunge 19 waliotimuliwa na CHADEMA sio wabunge halali.

Ndugai, akonekana mwenge wasiwasi na aliyepoteza mwelekeo akaanza kwa kujisifu kuwa yeye ni mzoefu, hivyo asipangiwe cha kufanya.

Ameenda mbali zaidi kwa kutaka kuonesha kuwa akina mama hao 19 wanaonewa na mfumo dume uliopo CHADEMA. Ndugai anasahau yeye na Profesa Lipumba walichowafanyia akina mama wa CUF walipovuliwa ubunge kwa kimemo cha Lipumba.

Mzee Ndugai atabaki katika historia kama SPIKA DHAIFU kuwahi kutokea. Tunazitaka Mamlaka za kulinda Katiba kuhakikisha KATIBA inalindwa.

Ikiwezekana kila NDUGAI atakapoonekana hadharani azomewe kwa aibu anayoiletea Taifa.

=======

1620817816647.png

Siku chache baada ya video kusambaa ikimuonesha Mbunge wa Mtama Nape Nnauye akichangia moja ya mjadala uliohusisha Wabunge 19 wa Viti Maalumu akiwaita (COVID 19) akidai kuwa wamefukuzwa na Chama na jambo hilo liheshimwa na kwa kuwa Katiba iko wazi kwamba hakutakiwi kuwa na watu wasio na chama ndani ya Bunge.

Spika wa Bunge, Job Ndugai amesimama Bungeni leo na kumuonya Mbunge Nape Nnauye na wabunge wengine kuwa makini na maneno wanayoyazungumza.

“Juzi mdogo wangu Nape yalimtoka maneno na yamezunguka sana kwa sababu ni mbunge, ikifika mahali mbunge na Spika mnapishana nadhani haipendezi, kwa hiyo sitapitia hoja zake kwa sababu ana uhuru lakini kitu kimoja hana uhuru kwa sababu ya kanuni ni kuwasema vibaya wabunge wenzake kanuni zinakataza hilo lazima nilikemee, aliwataja kwa majina ya mitaani huko ambayo kwa kweli alikosea sana na niliongea naye naamini aliteleza kwa hiyo sitamsimamisha hapa aseme chochote ninachoombeni waheshimiwa mmsamehe bure aliwakosea sana, tuchunge sana midomo yetu tunapodeal na binadamu wenzetu”-Spika Job Ndugai
 

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
44,329
2,000
Nape Nnauye ni mwanasiasa makini na anajua siasa kuliko Ndugai.

Nape amekuwa kwenye sekretarieti ya chama lakini Job ameishia kwenye ujumbe wa kamati kuu tu sawa na akina Bulembo au yule dada albino ambaye ni mwanamuziki.

Katika hili la covid 19 Nape yuko sahihi!
 

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
4,042
2,000
Nape zamu hii lazima avuliwe uanachama wa ccm, apoteze na hako kaubunge kake, akaungane na wenzake chadema. He is too much. Zamu ile aliomba samahani na akasamehewa (kwa mazungumuzo yake kwenye simu yaliyodukuliwa, wakimsema vibaya aliyekuwa rais wa JMT wakipanga mipango mibaya dhidi ya serikali).

Avuliwe uanachama wake wa ccm na tuone kama atang'ang'ania huo ubunge.
Juzi tulimwona akiwa na akina Lissu kwenye zoom wakiisema vibaya serikali ya awamu ya 6 chini ya mama yetu SSH!
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
40,876
2,000
Tuna katiba mbovu ambayo inampa rais kufanya atakalo, na ndiye pekee mwenye nguvu ya kuamua nini kitekelezwe kwenye katiba. Uwepo wa hao wabunge wa cdm yalikuwa maagizo ya Magufuli, na sasa mama Samia anaogopa kuagiza katiba ifuatwe kwani bado yuko kwenye kivuli cha Magufuli.

Lakini hata hivyo tunategemea kweli katiba itekelezwe wakati hata uchaguzi wenyewe ulinajisiwa? Vyombo vya ulinzi na usalama ni taasisi zinazoshiriki Moja kwa moja kwenye uvunjifu wa katiba kutokana muundo ama ubovu wa katiba yenyewe.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom