Spika Ndugai: Wabunge msitambulishe waume au wake za watu Bungeni

brave one

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
4,876
7,366
Spika wa Bunge, Job Ndugai akizungumza bungeni alipokuwa akiwaonya wabunge kutoleta taarifa za kutambulishwa bungeni waume au wake za watu wakidai ni waume au wake zao, alipokuwa akiongoza kikao cha bunge la bajeti, jijini Dodoma leo.

Ndugai amesema amepokea malalamiko kutoka kwa wananchi wakidai waume zao wametambulishwa bungeni kuwa ni waume wa wabunge.

Ndugai.jpg
 
Sio bungeni tuu mheshimiwa spika

Hata makazini na kwenye jamii kwa ujumla

Kuwe na mkataba ndio utambulisho ufuate, vinginevyo ni fujo tuu kwenye jamii
 
Huyu mzee anavyojifanya kuchongoa mdomo kuhusu wabunge kulana wao kwa wao, halafu kujifanya yeye msafi, mara paap mungu anamuumbua "ANAFIA GESTI AKIWA NA MKE WA MTU" akiwa na kopo la "MAFUTA MAZITO YA GLYCERINE" mfukoni, mafuta mengine kajipaka "NYUMA YA SIKIO".

Kama nawaona wana JF watakavyo mharishia humu.
 
Wamekosa cha kuzungumza hapo pia unapima uwezo wa watu waliopo bungeni kwa sasa.
:D 🤣 🤣 🤣 nakuelewa mkuu, walipitishwa kwa nguvu mwaka jana, matokeo yake ndio hayo. Majuzi, kuna mbunge ana suggest kwamba kiundwe chombo cha kusimamia serikali (unajiuliza, kazi za bunge ni zipi?). Yaani bunge limejaa vilaza sana.
 
Mambo ya utambulisho huko yamekuwa too much. Eti zari naye anatambulishwa mjengoni
Huo mjengo kama unachezewa

Ova
 
Back
Top Bottom