Spika Ndugai umejianika na kujiumbua, wewe si mtetezi wa Wabunge wanawake. Filamu yako ya akina Mdee umeshindwa kuilinda

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Mbunge wa Momba, tena wa chama chetu cha CCM, amedhalilishwa Bungeni. Ametolewa nje ya Bunge kwa aibu kuu akiambiwa kuwa 'hajavaa vizuri'. Amri ya kutolewa nje kwa mwanamama huyo Mbunge wa Momba ilitolewa nawe Spika Job Ndugai. Ni baada ya kuombwa muongozo na Mbunge Ameir akidai kuwa mwanamama huyo amevaa suruali 'mbaya' na hivyo kutakiwa akavae 'vizuri'.

Kwakuwa Bunge ni uwanja wako wa kujidai kwa kumimina amri na shurti kama mashuti katika hali ya kutafuta kiki za kisiasa zisizo za kisasa, Mbunge wa Momba alitoka kwa aibu kubwa huku akitwezwa, akidhalilishwa na kubagazwa na kitendo hicho. Akarejea baadaye kuendelea na kikao cha Bunge akiwa amevalia sketi na blauzi ileile. Nje na ndani ya Bunge, baada ya tukio lile, Mbunge huyo hakuwa na amani moyoni mwake. Ameanikwa na kuchorwa kama mwanamke asiye na maadili.

CHADEMA waliposema na kusimamia uamuzi wao wa kuwafukuza uanachama akina Halima Mdee, ni wewe Spika Ndugai ndiye uliyekuwa ukisimama Bungeni mara kwa mara kuwakingia kifua. Ukijitamba kuwa akina Mdee wako mikono salama, umekuwa ukiuaminisha umma kuwa wewe ni mtetezi wa haki za Wabunge hasa wabunge wanawake. Tukio la Mbunge wa Momba limekuumbua na kukuanika.

Unamtoaje Mbunge kwa aibu Bungeni bila hata kujiridhisha? Haki yake ya kujieleza mbona hukumpa? Siasa huhitaji usanii ila wako huu umezidi. Unajichora kama mtetezi wa akina Mdee ambao wako Bungeni bila kuwa na chama chochote cha kisiasa kama Katiba inavyotaka huku ukimdhalilisha Mbunge wa chama chetu tena wa Jimbo la Momba. Filamu yako ya akina Mdee imebuma. Jitafakari!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
 
Bwana ndugai hajawahi kuwa mtetezi wa wanawake popote.

Huyo mdee anayejidai leo kumtetea alishawahi kumuita majina mabaya hata kumfungia mwaka mzima!

Wakati anaingia bungeni na bandage baada ya kupigwa na kuzalilishwa na maafisa magereza baada ya sisi kumchangia yeye hakusema jambo.

Leo mdee na bulaya wamekuwa watu?

Mnafiki mkubwa
 
Huyo mzee anashida kichwani
 
Wachambuzi uchwara washaanza kuchomekea agenda zao.

Hakuna binadamu asiyekosea Job alikosea lakini yule babu aliyeleta hiyo kesi kutokana na umri wake hivo kuaminiwa na Job ndo alisababisha. Kufupisha Job kama kiongozi anatakiwa aombe radhi akina mama ili maisha yaendelee.

Sasa hawa wanasiasa wasije kutwist kwenye angle zingine.
 
Post ya kumchafua Mh.Spika wa digitali el comandante Ndugai.

Ni mwendelezo tu wa kumshambulia na kumtoa thamani.

Kuna kipindi waliokuwa wanakataa bunge lisionyeshwe hakika walikuwa na hoja, kwani kila kinachotokea ndani ya bunge basi kuna watu huku mitaani wanataka kuwa mahakimu wa shughuli za bunge na wabunge wetu.

Huu nao ni mwendelezo wa ujinga tu.
 
  • Thanks
Reactions: mmh
Wachambuzi uchwara washaanza kuchomekea agenda zao.

Hakuna binadamu asiyekosea Job alikosea lakini yule babu aliyeleta hiyo kesi kutokana na umri wake hivo kuaminiwa na Job ndo alisababisha. Kufupisha Job kama kiongozi anatakiwa aombe radhi akina mama ili maisha yaendelee.

Sasa hawa wanasiasa wasije kutwist kwenye angle zingine.
Kumbuka Mbunge ni kioo cha jamii mbali na wajibu wake mkuu wa kutunga sheria na uwakilishi ili Serikali iwajibike kwa wapiga kura walioiingiza madarakani. Hivyo wanapaswa kuwa makini kwa kauli na matendo yao, km mavazi.
 
  • Thanks
Reactions: mmh
Back
Top Bottom